Bila Rais Samia Suluhu, Freeman Mbowe angeozea jela. Upinzani fuateni sheria


Hivi wewe na akili yako unafikiri mbowe ni gaidi😂 hivyo basi kesho anaenda kulipua gas station… kesi za kijinga sana
 
Nimeshindwa kuendelea kusoma pale uliposema huyu bibi ni mchamungu! Huyu mwongo, mwizi wa kura na mdini ni mchamungu? Labda mungu sio Mungu
 
Kumbuka pia bila Magufuli kufa Samia asingekuwa rais, unataka twende kwa mtindo huo??? Kwamba bila Mkapa Magufuli asingekuwa rais!!!
 
Daah yaani kweli DPP anamsamehe gaidi ? Jamani tafuteni njia nyingine za kudeal na mbowe tulishasema sana hapa katiba mpya hata iweje itachelewa tu ila ni lazima ije tu hata kama ni kesho, hizi kesi za mchongo na kujifanya eti mna huruma ni kupoteza muda na rasilimari za taifa letu
 
Kwani huwa IPO Sheria ya kubambikia🤪,au nikutake ukasome PGO
 
" amri ya Rais Samia Suluhu Hassan kama amiri jeshi mkuu." imetolewa lini tuonyesha barua badala ya kudanganya watu
 
Bila Samia mbowe asingekamatwa
Mbowe ilikuwa ni lazima akamatwe ili wananchi wajue yanayoendelea sirini sirikalini.
Na ilikuwa ni lazima atolewe mahabusu ili sirikalini kutulie.
SSH anafanya safari nyingi lakini zote zisingeleta tija kama Mbowe angeendelea kuwa ndani.
Yes, ametolewa.
Sasa wananchi waungane pamoja kusaka uhuru wa kweli!!
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Hayaaa
Wewe Cheka. But ishu ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni tiba sahihi kwa mkwamo wa taifa letu.
Siku vikipatikana tutakuwa mbali kama Singapore na Malaysia.
Keep laughing...
 
Mwanahabari wa Taifa , ninaamini ukichoandika kimetoka kwenye uvungubwa moyo wako. Usijali wana JF wanaoponda waraka huu, ila nakuhakikishia Mbowe ataufuata kama ulivyo maana akipuuza na akafanya makosa ni yeye ndiye atakamatwa tena.
 
Naona mtoa post unasumbuliwa na bawasiria dalili moja ni kuwashwawashwa mak... Njo dm nikupe daw pia nikukumbushe mahakama aijamkuta mbowe na hatia bali ana kesi ya kujibu hivyo basi kesi ilikuwa imefika robo sasa ulikuwa upande wa mbowe kujibu ndipo dpp kamwaga manyanga
 
Bagonza sio njaa kama wewe ndugu.
 
Kidumu kilishatoboka zamani, hao usiowapenda wamevunja Sheria Gani za nchi hii zaidi ya nyie kuwaonea Kwa kuwabambikia kesi kinyume na Sheria🤔
Muulize jaji aliyetoa hukumu kuwa walikuwa na kesi ya kujibu. Halafu, sasa si Mbowe yupo huru, ana haki ya kufungua mashitaka ya kuonewa. Au hana?

Allah amzidishie Mama Samia Suluhu kila la kheri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…