Kaka yangu Freeman Mbowe Pole na hongera kwa kuachiwa huru leo 04|03|2022 kwa amri ya Rais Samia Suluhu Hassan kama amiri jeshi mkuu.
Karibu tena uraiani,Watanzania sasa ni wamoja pengine kuliko wakati wowote wa historia ya Taifa hili.
Pole pia tumetaarifiwa unatatizo la kiafya,Tunakuombea kwa Mungu urejee katika utimamu wako wa kiafya.
Mhe Freeman Mbowe nikutonye kidogo, hivi majuzi Viongozi wa kidini Tanzania waliomba kukutana na Rais wao kipenzi Mhe Samia Suluhu Hassan.
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa Uchamungu wake alionao aliwakubalia na akawaita moja kwa moja Ikulu,Wakala na kunywa pamoja nae.
Pamoja na Mambo mengine viongozi wa dini Tanzania wakiongozwa na mufti mkuu wa Tanzania walikuombea kwa Mama Samia Suluhu Hassan uachiwe huru bila masharti hata kama wewe ni gaidi kweli.
Viongozi wa dini Tanzania wanataka nchi yao waliopewa na Mungu iwe sehemu salama kwa kila mtu kuishi ukiwemo wewe Freeman Mbowe.
Kaka yangu Freeman Mbowe unatambua kabisa Mahakama kuu chini ya Jaji Tiganga ilikukuta na hatia ya kufadhili na kutenda ugaidi Tanzania ( Ulikuwa na kesi ya kujibu).
Leo tunashuhudia unyenyekevu kwa Mungu na Taifa alionao Mama yetu Samia Suluhu Hassan ameamua bila wewe wala chama chako kumwomba msamaha kukuachia huru tena bila masharti yeyote.
Mhe Freeman Mbowe naomba uelewe tu Tanzania imepata Rais Mpole na mnyenyekevu ever, Rais Mchamungu na Mtulivu wa moyo.
Rekodi zinaonesha tangu Taifa hili liwe huru hajawahi kupatikana rais Mahiri na jasiri mwenye huruma kama Mhe Mama Samia Suluhu Hassan.
Kwa unyenyekevu naomba kukutaarifu tu kuwa wewe sio "Mwamba" kama wanavyokuita Chadema wenzio,Binafsi nakushauri na kukusihi kuwa makini na kheshimu mamlaka zilizopo utakuwa salama.
Freeman Mbowe Wewe ni raia kama raia wengine na ukirudia kosa utashughulikiwa kama rais wengine kwani kwenye Taifa hili hakuna aliye juu ya sheria.
Watanzania tunataka siasa zenye tija kwa kizazi hiki na kizazi kijacho na kamwe hatutavumilia utoroshaji wowote wa amani yetu kwa tuko tayari kuilinda kwa gharama yeyote.
Wito wangu kwako, muheshimu na kumshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa dini wa Taifa hili kwani bila hawa ungekuta watoto wengine wasio wako.
Mhe Freeman Mbowe bila Rais Samia Suluhu Hassan hakika amini ungeozea jela huku Wale wanaoishi nje wakiendelea kunywa na kula kuku za bure kwa hisani ya wazungu.
Mwisho, Mtanzania popote ulipo bila kujali itikadi ya Chama wala dini yako shituka sasa, Huyu Rais ni Chaguo la Mungu shime tumuunge mkono popote kwa chochote kwani haya anayoyafanya ni hitaji la Mungu mwenyewe hata baba askofu Dkt Benson Bagonza ataungana na Mimi.
Mungu mbariki Rais Samia Suluhu
Mungu ibariki Tanzania yetu.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
View attachment 2138435
View attachment 2138436