Bila Rais Samia Suluhu, Freeman Mbowe angeozea jela. Upinzani fuateni sheria

Sheria zipi unataka zifuatwe. Kwani Mbowe hajatolewa kisheria. Na wewe unapoandika fuata sheria
 
Mahakama ilimkuta na kesi ya kujibu hajajibu na haijamsafisha Rais kamhurumia aka futa kesi. Sqsa mnapiga madomo MaCHADEMA hivyo hovyo tuu.
 
Ile kesi MBOWE angeshinda tu na serikali imejitia aibu sana kwa kubambikizia watu kesi
 
Jopo la utetezi la wasomi lililokuwa linaongozwa na adv Peter Kibatala lina kesi ya kujibu kwa unyanyasaji mliowafanyia mashahidi wa mchongo kwa kuwavua nguo hadharani na kuwasabishia ugonjwa wa kwenda msalani mara kwa mara.ILA MLIFANYA KAZI KUBWA SANA.MUNGU ATAWALIPA KWA KAZI YENU ILIYOTUKUKA.
 
Mbona hawakumtoa sasa Mbowe?
 
Kaka yangu Freeman Mbowe unatambua kabisa Mahakama kuu chini ya Jaji Tiganga ilikukuta na hatia ya kufadhili na kutenda ugaidi Tanzania ( Ulikuwa na kesi ya kujibu).

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Huelewi au unapotosha maksudi! Unaandika Mahakama kuu chini ya Tiganga ilikukuta na hatia ya kufadhili ugaidi - je baada ya kukutwa na hatia alipewa adhabu gani?
Baada ya kuona uongo na upotoshaji wako utakuwa dhahiri unaweka kwenya mabano - ulikuwa na kesi ya kujibu!
Labda nikueleze tu kuwa- kuwa na kesi ya kujibu si kwamba una hatia. Unaweza ukatengenezewa shtaka na wakaletwa mashahi wakisema hakika tulimuona huyu anavunja nyumba na kubeba mali kadhaa. Kwa ushahidi wa watu kama watatu hivi, mahakama itaona una kesi ya kujibu. Ujue wakati upande wa mashtaka unatoa ushahidi wako wewe huupingi kwa kutoa ushahidi wako, bali kwa kuonyesha kuwa labda taratibu hazikufuatwa na hivyo ushahidi kuchakachuliwa nk.
Ukishaonekana una kesi ya kujibu, ndipo sasa na wewe unaleta ushahidi wako kupinga yale yaliyosemwa na washtaki na kuthibitisha ushahidi wako. Kwa mfano katika mfano huo hapo juu wa watu kusema ulionekana unavunja na kubeba vitu, wewe unakuja na ushahidi kuwa katika saa hiyo wanayosema, ulikuwa kwenye ndege unaelekea London na unatoa uthibitisho wa ticket na boarding pass ya ndege hiyo, passport yako. Ukiweza unatafuta orodha ya wasafiri waliopanda ndege hiyo unaiwasilisha mahakani - mahakama inakuona huna hatia na unaachiwa huru.
Nadhani umeelewa
 
Yote tisa umeyaandika, moja kubwa ni kitendawili cha kuachiwa na Serikali bila masharti wakati mahakama, kwa ushahidi uliotolewa, ana kesi ya kujibu
Hiki siyo kitendawili - ilishaonekana wazi kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa na ya kuchonga. Ebu fikiria kwa nini akina Kidando walitaka kujua mashahidi wa utetezi ni akina nani na anwani zao? Unajua waliponyimwa waliingia gizani bila kujua nani wataitwa, Unakumbuka pia kuna ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na wakati huo huo na upande wa utetezi akina Kibatala nao wakasema watatumia ushahidi huo huo? Uliwahi kujiuliza mantiki yake?
Ebu fikiria kwa mfano kama Rais angeitwa mahakamani kuja kuthibitisha kauli yake kuwa katika kesi ile tayari kuna wenzake Mbowe walishahukumiwa na wanatumikia kifungo chao! Kama asingejibu ilikuwa ni siasa angejibu nini. Kumbuka angesimamia hoja yake kuwa kuna watu walisha fungwa ingebidi awataje na kesi ilikuwa namba ngapi. Na kama yeye angeaminika, then ushahidi wote uliotangulia ungeonekana ni wa uongo maana kuanzia mpepelezi mkuu nk walisema hakuna aliyekwisha fungwa katika suala hilo'
Contradiction zote hizi ndizo zililazimisha kutumika kwa busara kumaliza kesi hiyo
Kumbuka kuwa wengi walioongea kesi na Rais, walimuomba itumike busara kuimaliza. Suala la msamaha Mbowe mwenyewe alilikataa maana msamaha hutolewa baada ya kuoneka na una hatia na kufungwa.
 
Jibu swali la Wakili - Kama gari linabeba watu 5, na ninyi mlikuwa 7 je ni nani alimkalia Kigai ?
 

Kumbe bila Samia angeozea huko? Ndiyo maana katiba mpya ni jambo la dharura sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…