Bila Upelelezi kukamilika hakuna kukamata, ukiachiwa na Mahakama hakuna kukamatwa tena

Bila Upelelezi kukamilika hakuna kukamata, ukiachiwa na Mahakama hakuna kukamatwa tena

Hizi loophole ziko kila mahali suluhu ya kweli haiwezi kuletwa na kuziba matundu machache.
 
Wadau nimekutana na hili andiko, tulisome, tujadiliane tuone lina ukweli kiasi gani?

-----------------------

BILA UPELELEZI KUKAMILIKA HUWEZI KUSHITAKIWA / UKIACHIWA HURU NA MAHAKAMA HUWEZI KUKAMATWA TENA

Bunge limepitisha Mabadiliko muhimu ya Sheria kupitia muswada wa mabadiliko ya Sheria mbalimbali Na. 7 wa mwaka 2021 ambapo kifungu cha 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kimefanyiwa mabadiliko.

Kifungu hiki kipya cha 131A kinamkataza Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), Polisi, au yeyote mwenye mamlaka ya kushitaki, kutokupeleka kesi mahakamani pasipo upelelezi kukamilika. Hii ilipelekea mtu kukaa na kesi kwa miaka mingi huku kila siku akiambiwa na waendesha mashitaka kuwa upelelezi haujakamilika.

Pia kwenye mabadiliko haya, ikiwa utashitakiwa na mahakama kukuachia huru, basi polisi hana mamlaka ya kukukamata tena na kukufungulia kesi upya. Kitendo hiki kilikuwa kinawafanya watu watoke mbio sana mahakamani mara baada tu ya kuachiwa huru.

Kwa msingi huu Mwendesha mashtaka wa serikali, Polisi, na wengine wote wenye mamlaka ya kushitaki, ikiwa hajakamilisha upelelezi hana haki ya kufungua kesi mahakamani hadi pale atakapokamilisha upepelezi na pia hawezi kukukamata ikiwa umepatikana huna hatia na mahakama.

Unaweza ukaniuliza ikiwa wamekatazwa kupeleka kesi mahakamani kabla upelelezi haujakamilika, ina maana sasa watuhumiwa watasota sana selo mpaka polisi wakamilishe upepelezi wa makosa yao?

Jibu ni hapana, mabadiliko hayo hayo kifungu cha 131A (2) kinasema kuwa ikiwa upelelezi haujakamilika na hivyo kutomwezesha mtu kupelekwa mahakamani basi anatakiwa aachiwe kwa kupewa dhamana wakati polisi ama mamlaka nyingine ikiendelea kukamilisha upelelezi wa makosa yake. Hautakiwi kuwekwa selo au kukaa polisi ikiwa upepelezi wa kosa lako haujakamilika.

Hata hivyo, katazo hili la kutopeleka kesi mahakamani bila upelelezi kukamilika linahusu makosa yote isipokuwa makosa ya kubaka (rape), wizi wa kutumia silaha (armed robnery), kumiliki silaha kinyume cha sheria, kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, makosa ya kujeruhi sana (grievious harm), kosa la kuhatarisha usalama wa taifa, usafirishaji dawa za kulevya, na jinai nyingine ambazo hadhi yake husikilizwa tu na mahakama kuu. Kama kesi yako imefunguliwa mahakama kuu basi kosa hilo haliguswi na mabadiliko haya, utaratibu wa kawaida wa mashauri ya jinai utafuatwa.

Kifungu cha 131A(3) cha mabadiliko haya kinatoa msisitizo kwenye kifungu cha 170(6) cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kwamba kama makosa ambayo adhabu zake kama mtu angekuwa anahukumiwa na mahakama angehukumiwa kulipa faini ya Tshs 200,000/= basi mtu huyo anatakiwa akiri kosa kwa maandishi, kisha alipe faini hiyo kwenye akaunti za serikali, na aachiwe huru.

---------------------
 
MISWADA huwa inajadiliwa na inapitishwa na Baraza la mawaziri kwanza ndiyo inaenda bungeni.
kwaiyo hili hiwe tayari kutumika ni ikishapitishwa na bunge,au ikitoka bungeni inarudishwa kwa rais haisaini ndio iwe sheria rasmi?
 
Kwenye aya ya kwanza umeharibu.
Ungeweza kuandika bila mapambio.

Hata hivyo, hizo kesi ulizotaja ambazo mtuhumiwa huweza kukamatwa bila hata ushahidi kukamilika ndio kesi zinazowakumba walio wengi.

Sijaona kipya.
 
Wanaompinga Mama ni vichaa na watu wabaya tu,

Wasiopenda kuona WATANZANIA wakiwa wamoja wakati wote,

Wasiopenda watu waishi kwa raha mstalehe kwenye nchi yao,

Tunayo nafasi ya kujenga Taifa bora sana tukiwa na Mama Samia,
Bado haija solve tatizo effectively ikiwa uwepo mahabusu za Polisi nao hautaangaliwa. Usishangae watu wakakaa kwenye mahabusu za Polisi miaka na miaka wakisubiri kufikishwa Mahakamani.
 
Bado hapo kuna mwanya wa kuwakomoa watu. Wale ambao polisi watakaotaka kuwatesa, watafunguliwa mashtaka ya ujambazi wa silaha, au unawekewa silaha ili ionekane unamiliki silaha isivyo halali.

Wakishakutesa wanavyotaka wataondoa shtaka la kumiliki silaha kinyume cha sheria.
 
Hii ni hatua njema sana. Mana kuna kesi za kijinga kijinga ambazo watuhumiwa wanasota sana rumande au mahakamani bila upelelezi kukamilika
 
Sasa hapo ndio wamefanya nini,kwani polisi wanashingwa kukusingizia kuwa kosa lako lipo katika makosa ya ubakaji,kumiliki nyara za Serikali au ukahararisha usalama wa Taifa???
 
Mbona unamsififia Rais kwa kitu kingali kipo bungeni kama muswada?
 
Mama abarikiwe sana.
Uozo wa polisi ulifikia mahali pabaya sana, hasa kubambika kesi.
Cha kusikitisha na kuonyesha uozo wa Polisi ni hii kesi ya Mbowe.

Afisa, nasema Afisa wa polisi anajiharishia ovyo akiulizwa utekekezaji wa kazi yake ya upelelezi.
Shame!
 
Namtafakari mwalimu wangu Mh. Biwalo Mganga J. katika utekelezaji wa haya mabadiliko maana alijitahidi sana kufafanua athari fulani fulani wakati akiwa DPP
 
Tatizo sio sheria kuandikwa au kubadilishwa...je itatekelezwa?
 
Wanaompinga Mama ni vichaa na watu wabaya tu,

Wasiopenda kuona WATANZANIA wakiwa wamoja wakati wote,

Wasiopenda watu waishi kwa raha mstalehe kwenye nchi yao,

Tunayo nafasi ya kujenga Taifa bora sana tukiwa na Mama Samia,
Shika adabu yako wewe,Una maana sisi Sukuma Gang ni vichaa?
 
Back
Top Bottom