Bila Upelelezi kukamilika hakuna kukamata, ukiachiwa na Mahakama hakuna kukamatwa tena

Bila Upelelezi kukamilika hakuna kukamata, ukiachiwa na Mahakama hakuna kukamatwa tena

Tunaposema kila Mtanzania amuunge mkono Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan tunamaanisha mambo kama haya, Niwe mkweli tu tangu Uhuru Mama huyu ni watofauti sana hebu ona alichofanya kwenye magazeti na hii,
===
Bunge limepitisha Mabadiliko muhimu ya Sheria kupitia muswada wa mabadiliko ya Sheria mbalimbali Na. 7 wa mwaka 2021 ambapo kifungu cha 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kimefanyiwa mabadiliko.

Kifungu hiki kipya cha 131A kinamkataza Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), Polisi, au yeyote mwenye mamlaka ya kushitaki, kutokupeleka kesi mahakamani pasipo upelelezi kukamilika. Hii ilipelekea mtu kukaa na kesi kwa miaka mingi huku kila siku akiambiwa na waendesha mashitaka kuwa upelelezi haujakamilika.

Pia kwenye mabadiliko haya, ikiwa utashitakiwa na mahakama kukuachia huru, basi polisi hana mamlaka ya kukukamata tena na kukufungulia kesi upya. Kitendo hiki kilikuwa kinawafanya watu watoke mbio sana mahakamani mara baada tu ya kuachiwa huru.

Kwa msingi huu Mwendesha mashtaka wa serikali, Polisi, na wengine wote wenye mamlaka ya kushitaki, ikiwa hajakamilisha upelelezi hana haki ya kufungua kesi mahakamani hadi pale atakapokamilisha upepelezi na pia hawezi kukukamata ikiwa umepatikana huna hatia na mahakama.

Unaweza ukaniuliza ikiwa wamekatazwa kupeleka kesi mahakamani kabla upelelezi haujakamilika, ina maana sasa watuhumiwa watasota sana selo mpaka polisi wakamilishe upepelezi wa makosa yao?

Jibu ni hapana, mabadiliko hayo hayo kifungu cha 131A (2) kinasema kuwa ikiwa upelelezi haujakamilika na hivyo kutomwezesha mtu kupelekwa mahakamani basi anatakiwa aachiwe kwa kupewa dhamana wakati polisi ama mamlaka nyingine ikiendelea kukamilisha upelelezi wa makosa yake. Hautakiwi kuwekwa selo au kukaa polisi ikiwa upepelezi wa kosa lako haujakamilika.

Hata hivyo, katazo hili la kutopeleka kesi mahakamani bila upelelezi kukamilika linahusu makosa yote isipokuwa makosa ya kubaka (rape), wizi wa kutumia silaha (armed robnery), kumiliki silaha kinyume cha sheria, kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, makosa ya kujeruhi sana (grievious harm), kosa la kuhatarisha usalama wa taifa, usafirishaji dawa za kulevya, na jinai nyingine ambazo hadhi yake husikilizwa tu na mahakama kuu. Kama kesi yako imefunguliwa mahakama kuu basi kosa hilo haliguswi na mabadiliko haya, utaratibu wa kawaida wa mashauri ya jinai utafuatwa.

Kifungu cha 131A(3) cha mabadiliko haya kinatoa msisitizo kwenye kifungu cha 170(6) cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kwamba kama makosa ambayo adhabu zake kama mtu angekuwa anahukumiwa na mahakama angehukumiwa kulipa faini ya Tshs 200,000/= basi mtu huyo anatakiwa akiri kosa kwa maandishi, kisha alipe faini hiyo kwenye akaunti za serikali, na aachiwe huru.

" umepatikana huna hatia na mahakama"

Usikurupuke; hawaachiwagi Kwa sababu hawana hatia, rather mashahidi hawaonekani!

Hakiku aki declare huna hatia that is judgement, Hakuna mtu wa kukukamata labda rufaa.
 
Issue kubwa ni kuyapa dhamana hayo makosa yaliyoorodheshwa ndo itakua mukide...
 
Mtu akifanya unaloona zuri apongezwe na akikosea akosolewe, tatizo letu wabongo hatupo hivyo yani sisi tuna option mbili tu tukuchukie mazima(tukufanye shetani) au kukupenda mazima(tukufanye malaika).
Mtu anakopa mabillion ya Pesa kwa ajili ya kilimo,kwenye bajeti unasikia pesa iliyokwenda wizara ya kilimo ni 3%then anakwenda kukopa tena
 
Bila kuwa hivyo hizo sheria singetokea. Kwa sababu ya kuchukiwa anajaribu kufanya yanayolalamikiwa ili apendwe sasa. Aende mbele zaidi.
1. Amtoe mbowe bila masharti.
2. Pige chini miguru,weka Lukuvi
3. Piga February weka Kaleman
Na mengine
Hivi kosa la feb ni lipi
 
Binafsi siwezi kumpenda mtu aliyetuweka utumwani miaka 60. Samia na chama chake wameifanya Tanzania iwe nchi ya mqfukara, watumwa na makondoo.

Miaka 60 baadaye anatudanganya kuwa anarudisha uhuru wetu. Lakini kujitungia katiba yetu itakayotupa mamlaka kamili ya kuamua hatima yetu anasema hataki. Basi tu hataki. Anataka aweke visheria vinavyoweza kuvunjwa bila madhara.
 
Mama yuko vizuri sana,ila ana haribu yote mazuri aliyo anzisha kwa mfumko wa bei kwa bidhaa zote.Akirekebisha mfumko ni bonge la rais.
 
Wanaompinga Mama ni vichaa na watu wabaya tu,

Wasiopenda kuona WATANZANIA wakiwa wamoja wakati wote,

Wasiopenda watu waishi kwa raha mstalehe kwenye nchi yao,

Tunayo nafasi ya kujenga Taifa bora sana tukiwa na Mama Samia,
Very stupid of you.
 
This is also rubbish to some extent. If a police or for that matter the system wants to "screw" you, they will simply open your case file in the Hgh court! then you are done.................Rubbish!
Ni kweli kabisa wanatumia umbumbumbumbu wa watu, sijaona kipya hapo coz even internationally mtu anaburuzwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. Huku Africa tatizo kubwa ni viongozi kupenda kuwadjughulikia wote ambao wanatofautiana nao kimisimamo na kiitikadi kwa kuwabambikia kesi.
 
Ni kweli kabisa wanatumia umbumbumbumbu wa watu, sijaona kipya hapo coz even internationally mtu anaburuzwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. Huku Africa tatizo kubwa ni viongozi kupenda kuwadjughulikia wote ambao wanatofautiana nao kimisimamo na kiitikadi kwa kuwabambikia kesi.
Umemaliza kazi! asante
 
Hakika Rais Samia ameletwa Tanzania kuliponya Taifa,

Kitendo cha kukutana na Tundu Lissu Brussels Ubelgiji ni kiwango cha juu kabisa cha Uzalendo kwa Taifa,

Tumuunge mkono Rais wetu kwa haya kwani anastahili sana,
 
Back
Top Bottom