Bila Upelelezi kukamilika hakuna kukamata, ukiachiwa na Mahakama hakuna kukamatwa tena

Bila Upelelezi kukamilika hakuna kukamata, ukiachiwa na Mahakama hakuna kukamatwa tena

Hakuna kitu hapo, sisi tunataka katiba mpya haya mengine ni kutaka tu kutuondoa kwenye reli na katu hatutoki.

Sheria nyingi hizi za kidhalimu zilitungwa na serikali ya ccm lengo kubwa likiwa ni kuwakomoa wapinzani, hakuna kitu kingine.

Kuna kipindi mbunge moja wa ccm wa jimbo la Kishapo alipatikana na silaha haramu kinyume cha sheria lakini hakufanywa chochote sasa tuchukulie kama angekuwa ni wa Chadema....malizieni wenyewe.

Samia anatafuta tu namna ya kuungwa mkono na nchi wafadhili kwa sababu nchi iko taabani kiuchumi ndio maana anafanya haya pamoja na kuyafungulia magazeti waliyoyafungia wenyewe. Wadanganye wajinga huko huko ccm.
 
Tunaposema kila Mtanzania amuunge mkono Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan tunamaanisha mambo kama haya, Niwe mkweli tu tangu Uhuru Mama huyu ni watofauti sana hebu ona alichofanya kwenye magazeti na hii,
===
Bunge limepitisha Mabadiliko muhimu ya Sheria kupitia muswada wa mabadiliko ya Sheria mbalimbali Na. 7 wa mwaka 2021 ambapo kifungu cha 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kimefanyiwa mabadiliko.

Kifungu hiki kipya cha 131A kinamkataza Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), Polisi, au yeyote mwenye mamlaka ya kushitaki, kutokupeleka kesi mahakamani pasipo upelelezi kukamilika. Hii ilipelekea mtu kukaa na kesi kwa miaka mingi huku kila siku akiambiwa na waendesha mashitaka kuwa upelelezi haujakamilika.

Pia kwenye mabadiliko haya, ikiwa utashitakiwa na mahakama kukuachia huru, basi polisi hana mamlaka ya kukukamata tena na kukufungulia kesi upya. Kitendo hiki kilikuwa kinawafanya watu watoke mbio sana mahakamani mara baada tu ya kuachiwa huru.

Kwa msingi huu Mwendesha mashtaka wa serikali, Polisi, na wengine wote wenye mamlaka ya kushitaki, ikiwa hajakamilisha upelelezi hana haki ya kufungua kesi mahakamani hadi pale atakapokamilisha upepelezi na pia hawezi kukukamata ikiwa umepatikana huna hatia na mahakama.

Unaweza ukaniuliza ikiwa wamekatazwa kupeleka kesi mahakamani kabla upelelezi haujakamilika, ina maana sasa watuhumiwa watasota sana selo mpaka polisi wakamilishe upepelezi wa makosa yao?

Jibu ni hapana, mabadiliko hayo hayo kifungu cha 131A (2) kinasema kuwa ikiwa upelelezi haujakamilika na hivyo kutomwezesha mtu kupelekwa mahakamani basi anatakiwa aachiwe kwa kupewa dhamana wakati polisi ama mamlaka nyingine ikiendelea kukamilisha upelelezi wa makosa yake. Hautakiwi kuwekwa selo au kukaa polisi ikiwa upepelezi wa kosa lako haujakamilika.

Hata hivyo, katazo hili la kutopeleka kesi mahakamani bila upelelezi kukamilika linahusu makosa yote isipokuwa makosa ya kubaka (rape), wizi wa kutumia silaha (armed robnery), kumiliki silaha kinyume cha sheria, kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, makosa ya kujeruhi sana (grievious harm), kosa la kuhatarisha usalama wa taifa, usafirishaji dawa za kulevya, na jinai nyingine ambazo hadhi yake husikilizwa tu na mahakama kuu. Kama kesi yako imefunguliwa mahakama kuu basi kosa hilo haliguswi na mabadiliko haya, utaratibu wa kawaida wa mashauri ya jinai utafuatwa.

Kifungu cha 131A(3) cha mabadiliko haya kinatoa msisitizo kwenye kifungu cha 170(6) cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kwamba kama makosa ambayo adhabu zake kama mtu angekuwa anahukumiwa na mahakama angehukumiwa kulipa faini ya Tshs 200,000/= basi mtu huyo anatakiwa akiri kosa kwa maandishi, kisha alipe faini hiyo kwenye akaunti za serikali, na aachiwe huru.

Kwa sasa tatizo sio sheria, bali utekelezaji.
 
This is also rubbish to some extent. If a police or for that matter the system wants to "screw" you, they will simply open your case file in the Hgh court! then you are done.................Rubbish!
How possible the High court can accept the cases which are not in her jurisdiction?
 
Serikali hii hii ya ccm ndiyo iliyotunga nakutumia sheria mbovu miaka na miaka alafu serikali hii hii inakuja kurekebisha hiyo sheria alafu unataka tushangilie.Kwa akili za ovyo hizi tuna safari ndefu sana zakufikia kuiwajibisha serikali inapotenda isivyo stahili.Kwasababu siamini kua tunapaswa kutenda mabaya kwanza kisha badae ndo tuyarekebishe baada ya wananchi wengi kuumia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Daaah
 
Hii ikipita itakuwa poa sana.
Police walikuwa wakitumia udhaifu wa sheria kujikusanyia pesa za haramu
 
Hii itapunguza kesi zisizokua na ulazima wa kupelekwa mahakamni ili hali miongozo yake ya faini ipo wazi...
 
Tatizo lipo kwahawa polisi kuelewa mama Hana shida PGO ndomaisha yao lakini hawaijui
 
Wanaompinga Mama ni vichaa na watu wabaya tu,

Wasiopenda kuona WATANZANIA wakiwa wamoja wakati wote,

Wasiopenda watu waishi kwa raha mstalehe kwenye nchi yao,

Tunayo nafasi ya kujenga Taifa bora sana tukiwa na Mama Samia,
Nakuunga mkono kwa 100% . Nakupa heko mama yetu mpendwa

Sent from my CPH2121 using JamiiForums mobile app
 
Mmh, kumbe nyie mna chuki binafsi na huyo mama! Nimeamini Sasa wanaosema wanaomchukia,chuki zao ni sababu ya dini tu na ukabila! Lol
Profile yako kama ndiyo wewe
Basi si mchezomchezo

Ova
 
Imekaa vizuri
Kamilisha upelelezi mpeleke mtu mahakamani

Ova
 
Mtu akifanya unaloona zuri apongezwe na akikosea akosolewe, tatizo letu wabongo hatupo hivyo yani sisi tuna option mbili tu tukuchukie mazima(tukufanye shetani) au kukupenda mazima(tukufanye malaika).
Sio kweli
 
Makosa yote yawe na dhamana, vingenevyo ni cosmetics changes tu.
 
This is also rubbish to some extent. If a police or for that matter the system wants to "screw" you, they will simply open your case file in the Hgh court! then you are done.................Rubbish!
Only fools will appreciate these changes.
 
Back
Top Bottom