Bila Upelelezi kukamilika hakuna kukamata, ukiachiwa na Mahakama hakuna kukamatwa tena

Hapo nimeelewa baada ya kuona aina ya makosa ambayo haya husiki nahiyo sheria.

Chakuangalia hapo ni jinsi ya kuzuiya ubambikaji wa kesi maana mtu akiwa na chuki anaweza kukubambikia kesi ambayo haihusiani na hayo mabadiliko sheria na msoto wa rumande unabaki palepale, otherwise nampongeza mama kwa hili.
 
Mama anaupiga Mwingi ila asije kubadili gia angani kama umeme wa 27,000/=
 
Vyema! Lakini haikua haki ya mtanzania kuondolewa kwa vifungu kandamiz vya sheria?
 
Bado haija solve tatizo effectively ikiwa uwepo mahabusu za Polisi nao hautaangaliwa. Usishangae watu wakakaa kwenye mahabusu za Polisi miaka na miaka wakisubiri kufikishwa Mahakamani.
mahabusu za polisi mwisho kukaa ni siku 14
 
Hapo naona kama unafuu mdogo sana coz kama wakiwa na Nia mbaya na wewe watakushtaki kwa hayo makosa mengine yasiyokuwa na dhamana na blabla nyingine
 
Bado kuna shida, maana wata weka watu mahabusu miaka tele bila kufikishwa mahakamani
 
Wanaompinga Mama ni vichaa na watu wabaya tu,

Wasiopenda kuona WATANZANIA wakiwa wamoja wakati wote,

Wasiopenda watu waishi kwa raha mstalehe kwenye nchi yao,

Tunayo nafasi ya kujenga Taifa bora sana tukiwa na Mama Samia,
Bado kwenye muungano hakujakaa sawa kabisa..katiba bado inapwaya..tume ya uchaguzi ina pwaya pakubwa.

Kwa hili nalipongeza bunge


#MaendeleoHayanaChama
 
Akikosea atakosolewa,akifanya vizuri atasifiwa.......tupunguze unafiki wa kisiasa
 
Hapo naona kama unafuu mdogo sana coz kama wakiwa na Nia mbaya na wewe watakushtaki kwa hayo makosa mengine yasiyokuwa na dhamana na blabla nyingine
Tena wakati wa mwendaake hata ukimpasha ukweli kiongozi kwa mapungufu yake, unatafutiwa kesi ya uhujumu uchumi.
Kuna waliofia jela kwa kubambikwa kesi, mfano mzee Shamte wa TPSF.
 
Huyu ndo rais aliyetumwa na MUNGU,inchi Ina visheria vidogo vidogo ambayo vinaumiza Sana,mama take them off
 
Serikali hii hii ya ccm ndiyo iliyotunga nakutumia sheria mbovu miaka na miaka alafu serikali hii hii inakuja kurekebisha hiyo sheria alafu unataka tushangilie.Kwa akili za ovyo hizi tuna safari ndefu sana zakufikia kuiwajibisha serikali inapotenda isivyo stahili.Kwasababu siamini kua tunapaswa kutenda mabaya kwanza kisha badae ndo tuyarekebishe baada ya wananchi wengi kuumia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…