Bila wazungu, maisha yangekuwa magumu sana hapa duniani

Kwa hiyo ata kizazi hiki bado kinaendelea kumlaumu mzungu?
Hawezi kukwepa lawama, kwa sababu ameweka mifumo migumu sana. Neo colonialism ni hatari zaidi ya colonialism.

Kuna makala moja ya Prof. Lumumba niliona anaelezea kuwa Afrika ishayakanyaga kiasi kwamba kutoka inahitaji mapambano sio ya kawaida.

Waafrika kama wangesimama pamoja enzi za Lumumba, Gaddafi, Mgabe na wenzao labda wangeweza kutafakari.

USA kwanza aliiweka Afrika nzima kwenye utegemezi wa dollar. Pesa ya Afrika kwa mataifa mengi jau. Mataifa ya Afrika yakanasa kwenye mtego wa mikopo na misaada.

Viongozi wa Afrika waliokuja na ajenda ya benk ya Afrika, na currency ya Afrika walizimwa.

Waafrika wakanasa kwenye mfumo wa elimu ya kikoloni. Elimu inayozalisha machawa, na watu ambao wanawashangaa na kuwatukuza wazungu. Kama sio teknolojia kukua mpakaleo waafrika bado wangekuwa wanajazana mtaani kuwashangaa wazungu.

Waafrika wamejengewa taswira ya inferiority naimekomaa, wanaamini wao ni inferior na wazungu ni superior. Waafrika wanaamini hamna kitu wanaweza kufanya isipokuwa wazungu tu


Mambo ya ajabu sana.
 
Mkuu maendeleo ya Dunia yamepitia stage mbali mbali mpaka kufukia hatua hii ya wazungu anyway anayemaliza ndio ataonekana na mtu atakayeshinda vita ndio mwandishi wa historia.
Historia wakati mwingine inadanganya na inawafanya watu waridhike na walichonacho.
 
Waafrika tuna visingizio vingi sana
 
Maisha yanekuwa magumu kwa sababu zao,

Kabla hawajaja afrika, maisha yalikuwa Safi tu na machifu walikuwa wanarawala, kulima na kufanya kazi zao vzr
Bila wao nyumba za block zingekuwepo kweli?
 
Sio Tu Africa, hapa hapa Tanzania, humu humu jukwaani Asilimia 99 hawajui historia ya waswahili na mambo waliofanya, namna walivyokuwa wakisafiri duniani etc.

Enzi hizo wazungu wanajisifia kuto kuoga tayari huku waswahili wanajenga Coral rag architectures, nyumba za Ghorofa kutumia limestone na material za baharini ambazo Hadi Leo miaka zaidi ya 1000 baadae zipo, unatumia technology ya kuletewa Inajenga nyumba ikikaa miaka 50 unajisifia imara, babu yako kajenga imekaa miaka zaidi ya 1000 unamuona mpuuzi na unamtukuza ambaye kacopy tech ya babu yako na kui dilute.
 
Leo hii sisi waafrika, tunauza nini nje zaidi ya malighafi?
 
Waafrika tuna visingizio vingi sana
Kwenye visingizio kuna watu wamefanya tafiti na wamejiridhisha. Unadhani miaka yote hii hakuna watu wanatamani kuiona Afrika imeendelea?

Kwa nini hawafanikishi. Lazima kuna vikwazo wanapitia na hivyo vikwazio wewe pengine unaona ni visingizio.

Sometimes no explanation can make you understand, but a real experience.
 
Mfano mdogo tu, kitu gani kimekuzuia wewe kutengeneza injini ya pikipiki?
 
Mfano; Uganda, Cameroon, Je ni sahihi mtu kukaa madarakani zaidi ya miaka 40 wakiamini hakuna wengine wenye uwezo huo?
Hakuna mahali kwenye katiba yao kuna ukomo wa uongozi, kama ingekuwepo tungesema si sahihi. Hata Gaddafi alikaa miaka 40 ila wananchi waliendelea jumtaka aendelee kukaa, hata waliyokuja kumwondoa walikiri walifanya kosa
 
Nadhani kinachotufanya waafrika tunaonekana wajinga ni ubishi, kutokukubali kujifunza kwa wengine, wivu, ukosefu wa ushirikiano, ukabila, Imani potofu. Wenzetu kama wachina walikuwa maskini lakini angalia tabia zilizowafanya hadi wameendea kujifunza, ushirikiano, heshima, ubunifu, uzalishaji, Imani potofu hamna kama Africa.

Nadhani kwa jicho nililinalo kama wabongo na waafrica wengine tutaendelea na hii tabia basi umaskini ni rafiki yetu hata miongo na Karne zijazo.
 
Hakuna mahali kwenye katiba yao kuna ukomo wa uongozi, kama ingekuwepo tungesema si sahihi. Hata Gaddafi alikaa miaka 40 ila wananchi waliendelea jumtaka aendelee kukaa, hata waliyokuja kumwondoa walikiri walifanya kosa
Naona hata mzee Kagame amekaa muda mrefu madarakani lakini nadhani Rwanda ameiweka kwenye msitari madri alivyoweza.

Lakini pamoja na kutokuwa na zuio la ukomo, suala la kiongozi kukaa madarakani akiamini hakuna mwingine kama yeye ni kudhihirisha kuwa hajatimiza wajibu wake kama kiongozi.

Kiongozi bora huzalisha viongozi bora zaidi. Watakaolinda mifumo ya taifa.
 
Hakuna mahali kwenye katiba yao kuna ukomo wa uongozi, kama ingekuwepo tungesema si sahihi. Hata Gaddafi alikaa miaka 40 ila wananchi waliendelea jumtaka aendelee kukaa, hata waliyokuja kumwondoa walikiri walifanya kosa
Ile kukaa muda mrefu ni kuwanyima wengine wenye maarifa mazuri zaidi yako kutoshika nafasi.
Tunajua ukeketaji si mzuri, kwa hiyo si vizuri kuwaachia watu waendelee kukeketana kwa sababu ni utamaduni wao.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…