Ndio! SERIKALI huwa ina miliki mpaka hoteli na mikoa ambayo SERIKALI ina hoteli nyingi ni mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO.
SERIKALI inajishughulisha na kila aina ya BIASHARA HALALI inayofanyika nchini na nje ya nchi. Ndio maana ikaitwa SERIKALI.
SERIKALI inafanya BIASHARA HALALI yoyote ile inayofanyika nchini, sema huwa kuna utaratibu wake wa kufanya BIASHARA.
Hauwezi kuona AFISA MASOKO WA SERIKALI au AFISA UGAVI WA SERIKALI ndio utambue kuwa sehemu fulani ni sehemu ya kibiashara ya SERIKALI.
Ndio! Baadhi ya HOTELI zinakuwa zinamilikiwa na watu [ na sio kumilikiwa, zinakuwa zimepangishwa ] lakini GOLD CREST ilikuwepo hata kabla ya huyu jamaa hajapangisha. GOLD CREST ni ya siku nyingi sana.
Kwa mfano, HOTELI YA KEMPINSKI ilikuwa ni hoteli inayomilikiwa na SERIKALI na hata ilipokuja kuuzwa kwa mtu binafsi mwaka 2000 ilitangazwa hadi kwenye VYOMBO VYA HABARI kama REDIO na MAGAZETI YA SERIKALI na hata BUNGENI ilishawahi kujadiliwa hii.
Hii HOTELI YA KEMPINSKI ilivyouzwa kwa mtu binafsi ndio ikaitwa HOTELI YA KILIMANJARO yaani THE KILIMANJARO na aliyeinunua akaipangisha kwa wamiliki wa hoteli za HYATT REGENCY.
Hii HOTELI YA KILIMANJARO [ HYATT REGENCY ] alivyoingia RAIS MAGUFULI madarakani alitaka kuirudisha SERIKALINI lakini thamani yake ilikuwa ni kubwa mara tano ya bei waliyoiuza mwaka 2000.
Hii HOTELI YA KILIMANJARO [ HYATT REGENCY ] ilikuwa ina thamani ya shilingi USD 200,000,000 za kimarekani ambazo ni sawa na shilingi TSH 520,000,000,000 za kitanzania. Kwahiyo SERIKALI ikashindwa kuirejesha hoteli iliyokuwa inamiliki kwa kipindi cha miaka ya nyuma.