Bilionea Warren Buffett: Nikifariki mali zangu wapewe wenye uhitaji

🥴🥴, kila nikifiria hayo mabilioni yanayo kopwa na serikali.. Alafu yanako enda hayaeleweki..
 
Kwanini urithi?

Kwanini atoe akifa...

Atoe sasa akiwa hai, sehemu fulani kwa hao wahitaji...

Kwa tunaoamini Mungu, tumeambiwa tutoe sadaka kwa wahitaji...

Ikiwa na maana tukiwa hai sio wafu...
Buffett haongozwi na imani zenu hizo ambazo mnatoa sadaka kisa mmeelekezwa vitabuni na kutishwa mtachomwa moto ila mkitoa misaada mtapunguziwa adhabu ya kaburi.

Buffett anaongozwa na humanity, sio dini. Ametoa msaada tangu 2006 sababu ya ubinadamu sio sababu ya dini. Na kachelewa kuanza kutoa misaada mikubwa sababu alichelewa kuwa billionaire. Utajiri wake kaupata kwa savings na reinvestments hasa kwenye hisa. Ni utajiri wa kuupata miaka 30 baadae sio wa kukurupukia. Huna cha kumshauri wala kumpangia Buffett na rafiki yake Charlie Munger aliyefariki juzi.

Inashangaza kuona mtu from nowhere anampangia tajiri wosia wake uweje. Chukua wewe hizo nguo zako gawa kwa wasiojiweza ushindie mashuka ili ukifa uende mbinguni.
 
Mshenga umekuja kumsemea...

Utajiri unasiri nyingi, wewe unaona na macho yako hayo ya nyama...
 
Usilolijua ni usiku wa giza...
Swali la kujiuliza ni masikini ni nani? Anahitaji nini hasa?...Je kuwapa masikini mali ni kuwapa uwezo endelevu?.
Anayekupa samaki na hakufundishi anavyovua hao samaki sidhani kama ana nia ya dhati ya kukupa msaada endelevu "sustainable support"
Usiwafundishe wanao uongo uleule uliofundushwa.
 
Na kitendo cha kujiondoa Berkshire Hathaway kwa kuuza hisa ni kuua kampuni sababu investors watapoteza confidence wauze hisa na zishuke thamani. Assume mtu kaweka share Mohamed Enterprises alafu ghafla anasikia Mo Dewji anataka auze hisa zote, si inazua taharuki. Kama mmiliki au mwanzilishi haamini tena kwenye kampuni, sembuse wewe uliyedandia mbele ya safari.
 
hana lolote anatafuta attention kwenye media kwanza mjitoaji wa kweli hasemagi
 
🥴🥴, kila nikifiria hayo mabilioni yanayo kopwa na serikali.. Alafu yanako enda hayaeleweki..
Yaani majizi haya hayawezi kupeleka popote zaidi ya kujenga majumba na kuandika mahawara na ndugu
Yaani hawawezi kufungua biashara na kuajiri watu 1000
Ndio maana kuona mswahili ana biashara za wazi ni wachache sana maana wengi ni majizi hawawezi kuwa na mfano wa kina Bakhresa au MO na wengine

Usishangae kuona wenye asili za nje ndio wanaongoza kwa sababu utajiri wao unajulikana kwa historia zao

Sasa sisi anahaha mpaka anaamua kuwapa hao hao matajiri wawekeze kificho
 
Mkuu hakuna tajiri atakeye kupa Chanzo cha mali zake, au mbinu alizo tumia kupata huo utajiri ..
 
Ni kweli mkuu ✍️✍️.
 
Mshenga umekuja kumsemea...

Utajiri unasiri nyingi, wewe unaona na macho yako hayo ya nyama...
Hata umaskini una siri nyingi tu. Hata kuzaliwa kwako kuna siri nyuma ambayo wewe mwenyewe huijui.
Kwanini unadiscredit nia njema ya tajiri kisa "utajiri una siri". Kwahiyo kwa sababu utajiri una siri basi matajiri wanatakiwa wagawe mali zao wakiwa hai kisha wawe ombaomba ndio siri za utajiri zitafichuka.

Juzi hapa kwenye uzi wa Nayce Mushi wa Tilisho kuna watu wenye negativity ya mafanikio yake walikuwa na maneno ya chuki na roho mbaya nao walisema mafanikio ya mwanamke yana siri nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…