Bilioni 11 za Rais Samia zamtetemesha RC Shinyanga, afanya maamuzi magumu

RC anasema hivi kwa sababu yeye sio " accounting officer" wa mkoa. Hata hayo ya kumuondoa afisa ni maneno ya jukwaani. Mwenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Katibu Tawala wa Mkoa. RC hapitishi matumizi yeyote mkoani na ha saini hundi yeyote. Wenye mamlaka hayo ni makatibu tawala na wakurugenzi. Hapa ameingilia kazi za wenzake.
Amemuacha mkurugenzi kwa sababu anajua kuwa bila yeye hakinunuliwi kitu hata afanye nini. Wanachoweza kufanya watendaji wakipata amri kama hizi ni kuzipeleka kwa madiwani ili watoe baraka zao. Minutes za kikao cha madiwani na kibali cha Katibu Mkuu wa Tamisemi kitamchomoa kwenye tundu la sindano. Kama alivyo chomoka yule wa Vieiti. Wakimkatalia nayo ni vizuri. Hata wakikaa kimya, ataweza kuchomoka kwa kusema anangoja maelekezo kutoka wizarani. Akitekeleza tu mzigo wote utakuwa wake hasa itakapogundulika kuwa vifaa alivyonunua havina viwango.
Wanasiasa wabaki kwenye siasa na waheshimu wenye taaluma zao.

Amandla...
 
Rc Shy kachemka nahoji uhalali was vyeti vyake na vetting itakuwa ina chenga chenga procedures za manunuzi hazikwepeki hiyo siyo pesa ya mtu binafsi aache mihemko
 
Utawala bora ni Upi?
Watoto wasiende shule kwa wakati?
Mkuu, unaweza ukaona ni heri akatafutwa mzabuni au mkandarasi kwa njia ya mkato ili watoto waende shule, lakini siku ikibainika kuna shaka katika matumizi ya fedha, huyo huyo afisa manunuzi anayelazimishwa atumie njia za mkato ndiye atakayeswekwa ndani kwa kile watakachokiita 'kukiuka taratibu za manunuzi ya umma'

Mbaya zaidi mahakamani huwa hakuna utetezi kwamba ulitumia busara mradi ukamilike haraka watoto waende shule, sana sana huwa kuna mashtaka kwamba ulivunja sheria za manunuzi, na atafungwa afisa manunuzi, sio mkuu wa mkoa. Na tena sisi wenyewe huwa tunakuja kusaga kunguni kwamba afisa manunuzi alileta kampuni za ndugu zake!
 
Huyo RC kelele tuu na kama alifuata utaratibu hana ujanja wa kumfukuza kazi atarudishwa na atalipwa haki zake zote
 
Peleka vyako mkuu,
Mimi vyangu genuine vipo chini ya mchago kitambo ila kwa kauli ya Rc Shy kwakweli kaonyesha kupwaya Sana even if wanatumia force ac/ single source lakini PPA zifuatwe ninaongea by experience ni hili
 
Acha kutia watu hofu,Nia njema lazima ionekane hata kama itachelewa
 
Hongera Rais Samia mimi nichadema ila nakukubali Sana
 
Safi Sana
 
Mimi vyangu genuine vipo chini ya mchago kitambo ila kwa kauli ya Rc Shy kwakweli kaonyesha kupwaya Sana even if wanatumia force ac/ single source lakini PPA zifuatwe ninaongea by experience ni hili
Hizo regulation lazima ziakisi malengo ya mradi,
 

Rais ni taasisi na ndiye anayeunda serikali; amechaguliwa na wananchi anaongea na kutenda kwa niaba ya wananchi kwa hiyo tukisema Rais Samia ametoa fedha ni sahihi tu kwa kuwa hatuzungumzi Rais kama mtu binafsi bali ni taasisi.
 
Rais ni taasisi na ndiye anayeunda serikali; amechaguliwa na wananchi anaongea na kutenda kwa niaba ya wananchi kwa hiyo tukisema Rais Samia ametoa fedha ni sahihi tu kwa kuwa hatuzungumzi Rais kama mtu binafsi bali ni taasisi.
Hana fedha za kugawa kwa wananchi msilazumishe kufurahisha nafsi zenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…