Bilioni 650 za DP World Zamkuna Makala. Zaongeza Ufanisi wa Bandari ya Dar kutoka Makasha 7,000 Hadi Makasha 20,000

Kagame alimwambia JK ninaweza kuiendesha Tanzania kwa kutumia hiyo bandari peke yake. Samia amekuja na kutimiza maneno ya dhihaka ya Kagame kivitendo.

Hakuna linalomea ghafla tu kama uyoga, lolote lenye tija pana hupewa muda na uhuru wa kufanya kazi.
 
Kwani kutamka unalipia bei gani? Kwani Nchi zote zilizoendelea kushinda Rwanda zote Zina Bandari?
 

..IGA inagusa bahari na mito ambayo inalindwa na sheria ya rasilimali ya 2017.

..Nilipozungumzia uwazi nilikuwa nazungumzia kutangazwa kwa zabuni ya uwekezaji bandarini ktk maeneo aliyopewa Dpw na Adani.
 
..IGA inagusa bahari na mito ambayo inalindwa na sheria ya rasilimali ya 2017.

..Nilipozungumzia uwazi nilikuwa nazungumzia kutangazwa kwa zabuni ya uwekezaji bandarini ktk maeneo aliyopewa Dpw na Adani.
Sio lazima kutangazwa Kwa sababu kina njia kadhaa za kupata Mkandarasi hata single source inakubalika kisheria
 
Imesaidia nini kwenye pato lako? Hizi bandari nimenunua kwa matumizi yangu binafsi.
 
Mdogo wangu kama hujui mambo Kaa kimyaa.
Umesema meli zinakaa siku 3? 😂😂

Hii nchi wajinga ni wengi sana ndio mana hata kuitetea huwezi
 
Guluguja Makala
 
Haya yote ni kujidhalilisha kwani TPA walishindwa wapi kufanya wanachofanya DP kwa muda mfupi tu wa miezi 6 ambapo hakuna miundombinu iliyobadilika bado kila kitu ni kama walivyokuta? Inasikitisha.
 
..IGA inagusa bahari na mito ambayo inalindwa na sheria ya rasilimali ya 2017.

..Nilipozungumzia uwazi nilikuwa nazungumzia kutangazwa kwa zabuni ya uwekezaji bandarini ktk maeneo aliyopewa Dpw na Adani.
Bandarini ni maji pekee yanayoweza kuwekwa kwenye kundi la rasilimali, huwezi ukaiweka mitambo na makasha yanayobeba bidhaa katika kundi la rasilimali.

Hivyo ni kosa kuiweka bandari katika rasilimali kwani ni sehemu ndogo tu yenye kujumuishwa kwenye kundi hilo.

Bandari ni kitegauchumi cha nchi, haiingii kwenye kundi la hiyo sheria ya 2017.

Zabuni iliyompa Adani tenda ya kuendesha magati namba 8-11 umewahi kuisikia?.

Hiyo IGA ya DPW ilivuja kimakosa tu.
 

..tuko pamoja kwamba bahari na mito ni moja ya rasilimali zinazolindwa na sheria ya mwaka 2017.

..sasa ile IGA ilikuwa inakwenda kinyume na hiyo sheria na kama sijakosea serikali baada ya kupitisha IGA walitaka kuifanyia marekebisho sheria ya mwaka 2017.

..sijasikia zabuni ya gati alizopewa Adani, wala zabuni ya Dp W. Ndio maana nasema hakuna UWAZI, na hilo ni kosa kisheria. Na waliokiuka sheria bila shaka walisukumwa na IFISADI.

..mambo yetu hatufanyi kwa uwazi na hiyo italeta shida ktk kupima ikiwa tunapata, au tunapigwa ktk uwekezaji unaofanyika.

..Dpw na Adani wako kutengeneza faida, hawajakuja kutufadhili, tunapaswa kuwachukulia kwa tahadhari.
 
Huwezi kuiweka bandari katika kundi la rasilimali kwa kigezo cha maji peke yake, vipi kuhusu meli na makontena?, vipi kuhusu zile machine za kupakia na kushusha mizigo?. Hoja kwamba bandari ni rasilimali ni upuuzi mtupu ndio maana hata mahakama iliitupilia mbali.

Hatutakiwi kusikia suala la zabuni za Adan wala DPW kwa mujibu wa sheria ni makosa hata kufahamu kinachoandikwa kwenye mikataba na kujadiliwa, kibiashara DP World anaweza kuwa katupendelea katika masharti fulani ya kibiashara tofauti na alivyoingia makubaliano na mataifa mengine ndio maana ya usiri wa mikataba.

Uelewa wetu kuhusu mikataba ni ule wa kisiasa, wa jumla jumla tu. Tofauti na sheria za kimataifa zinavyofanya kazi.

Unaposaini mikataba maana yake pande mbili zinafikia makubaliano ya pamoja kimaandishi na ukiwa ndio muongozo rasmi wa kibiashara, kunakuwa na kujishusha ili muafaka ufikiwe na kila kitu kunakuwepo kwenye hiyo mikataba.

DPW au Adani anaweza kuwa kajishusha katika kutoa huduma fulani na hataki habari hizo zimfikie mdau mwingine wa biashara ya shipping zaidi ya Tanzania. Unapoweka wazi na kuanza kujadili yanayoandikwa ni kosa kwa mujibu wa sheria za kimataifa zinazotawala biashara.

Hakuna suala la uwazi lkwenye kusaini mikataba ya kimataifa, hizo ni siasa zetu zenye kuongozwa na fikra kwamba tunaibiwa au tunanyonywa, it is a stupid socialistic mentality.
 

..unasema uongo.

..zabuni kwamba TPA wanakodisha gati # 8 - 11, pamoja na gati nyingine, ilipaswa kutangazwa ili makampuni mbalimbali yaweze kuomba na kushindanishwa.
 
..unasema uongo.

..zabuni kwamba TPA wanakodisha gati # 8 - 11, pamoja na gati nyingine, ilipaswa kutangazwa ili makampuni mbalimbali yaweze kuomba na kushindanishwa.
Umeshajiuliza kwanini wanasheria wetu wanashindwa kesi na tunalipa mabilioni ya pesa huko nje?.

Sababu ni kuingiza siasa kwenye masuala ya kisomi yenye taratibu nyingi ambazo hatuzifahamu lakini tunajidai kujua kila kitu.

Mkataba wa kibiashara kati ya DPW na Tanzania huwezi kuuanika kama habari za mechi za simba na yanga. Kuna favors nyingi za kibiashara ambazo pande mbili zinazoingia kwenye mkataba zinapeana na huwezi kuziandika magazetini.

Sio masuala mepesi kama tunavyodanganyana humu JF, IGA iliweza kusambaa kwa sababu mle hakuna masuala nyeti ya kibiashara ni miongozo ya kawaida tu.

Ila huu mkataba uliosainiwa pale ikulu mbele ya Samia na yule mwakilishi wa DPW huwezi kuusambaza mitandaoni bila ya kushtakiwa.
 
Yaani billion 600 na point zimeongeza ufanishi mara tatu zaidi wakati serikali yetu kabla ilishatumia zaidi ya trilion 2 kurekebisha hapo bandari na utendaji haukuongezeka kiivyoo..
Watanzania tumerogwaa *****..
 

..ZABUNI ni kitu tofauti na mkataba.

..Zabuni lazima iwe wazi, na mchakato wake uwe wa ushindani.

..Mkataba ndio baadhi ya maudhui yake yanakuwa ya siri. Sio mkataba wote unakuwa wa siri.
 
..ZABUNI ni kitu tofauti na mkataba.

..Zabuni lazima iwe wazi, na mchakato wake uwe wa ushindani.

..Mkataba ndio baadhi ya maudhui yake yanakuwa ya siri. Sio mkataba wote unakuwa wa siri.
Hapakuwa na haja ya kutangaza zabuni kulingana na mazingira ya uwekezaji mzima ulivyo. DPW anafanya biashara nzima ya logistic kwa maana ya kuufuata mzigo unaotoka huko DRC kuja bandarini na kwenda huko nje.

Sio kila biashara inaanza kwa zabuni yake kuwekwa wazi, inategemea na nature ya biashara nzima ipo vipi.

Tanzania na DPW haziruhusu mkataba mzima kuanikwa hadharani sawa na ile biashara ya adani ya magati namba 8 mpaka 11.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…