Binadamu hana jipya hapa duniani zaidi ya kuwa ni mfugo unaosubiri kuliwa tu

Binadamu hana jipya hapa duniani zaidi ya kuwa ni mfugo unaosubiri kuliwa tu

Mzee huna jipya hapa duniani wewe ni mazao tu yanayosubiri kuliwa aidha na Mungu au Shetani.

Wewe toka povu tu na kujifanya mjuaji ila huo ndio ukweli.

Hakuna theory hapa wala nukuu ya kitabu chochote maalifa binafsi yanatosha.
Poa ngoja tuamue kutembea na hiyo nadharia yako bila kupinga;

Tuongeze nadharia ya mfano kwamba labda mchicha ukiula wewe binadamu, mchicha unakuwa sehemu ya binadamu na unafaidi ile experience ya kuwa binadamu. Utaishi nyumba nzuri utaendesha magari etc
Mchicha hautapenda kuliwa na mbuzi kwa sababu ona experience ya kuwa mbuzi sio tamu kivile, analala sehemu chafu, anapigwa jua,hathaminiwi etc. Kwa hiyo bora mchicha uliwe na binadamu na sio mbuzi. Uuexperience ubinadamu na sio umbuzi.

Kwani we unajuaje kwa nini ukila mchicha unaona zaidi? Ni kwa sababu mchicha ukiingia mwilini mwingi unajaa kwenye macho kwanza baadae ndo uende na kwingine. Kama tu ambavyo mshamba mwingine yeyote[toka shamba] <'pun intended'😂🤣🤣🤣🤣> akifika mjini au sebuleni ni macho ndo yanakuwa active zaidi! Kwa hiyo ndugu hata kama mchicha kiukweli ukawa hauna uwezo huo[kiuelewa/akili]. Tambua kwamba kwa binadamu ndivyo ilivyo, tumeumbwa na uelewa na utambuzi kujitambua na kutambua. Ukiliwa na Mungu utauexperience umungu[uhai], ukiliwa na shetani utauexperience ushetani[kifo]

Tuendelee na moto wetu 'Hakuna theory hapa wala nukuu ya kitabu chochote maarifa binafsi yanatosha.'💪. Nimeupenda.
 
Hapa umeandika upumbavu tupu, kitendo cha wewe kuandika, binadamu mfugo, unaofugwa na "KILE KINACHOITWA" Tayari huamini uwepo wake, Kama Hakuna Mungu, anawezaje kuwepo.
 
Hiki kitu nilikuwaga nakiwaza Sana nlipokuwa form 2 kwasababu nilikuwa mtu WA kusali Sana
...

Kinachowachanganya watu Ni Ile notion ya kwamba Mungu/shetani wasio Na mwili nao wanakula.??

Ebhu fikiria Sisi binadamu tusingekuwepo, huyo Mungu ana thamani gan??
Yaani ndiyo ...Ni Sawa ameumba manyota yote Na madunia lakini kama Sisi hatupo kumtambua Na kumsifu Yani Ni Kazi Bure Tu maana hayo madunia hayajitambui Na kumsifu...

Yaani Ni Sawa uwe sharobaro kwenye kisiwa ambacho unaishi pekeyako...
Hata uvae Nguo Za Bei kiasi Gani au hata uvae mashati ya dhahabu Na Boxa ya almasi, kama hamna watu wa kukuona Na kusifia Ni Sawa Tu Na ukivaa magunia,hamna tofauti..

Swali la muhimu ni Je? Kati ya sharobaro Na watu wa kumsifia yupi Ni wa muhimu??
Jibu Ni watu wa kumsifia...maana watu wa kusifu wanaweza kuwepo bila sharobaro mtaani lakini sharobaro hawezi kuwepo bila watu wa kumsifia...

Hivo hivo jiulize..Kati ya chakula Na mlaji Nani Ni muhimu?
Jibu Ni chakula, maana vyakula vinaweza kuota,kusitawi, Na kuzaliana bila kuwepo walaji lakini walaji hawawezi kuwepo bila chakula..

Kwahyo Kwa hiyo mifano Mungu Ni sharobaro au mlaji Na Sisi Binadamu Ni chakula au wanakijiji wa kumsifia sharobaro.
Kwahyo in conclusion, Sisi binadamu Ni wa muhimu Kuliko Mungu
 
Huyu kaka kaongea point Sana ..Hivi ulishajiuliza swali, kwanini Hawa kina Mungu Na shetani wanatumia Muda na resources nyingi Sana ili kutuvutia upande Wao?
Mungu anatumia makanisa,wachungaji,kwaya, Misikiti,vitabu, mashehe mpaka makundi kama Al Shabaab ili kujipatia wafuasi binadamu.
Shetani yeye anatumia Pesa,ngono,ulevi,mziki Ni. ili kujipatia wafuasi.(Mungu anatumia mbinu chafu Zaidi)

Yaani Hawa kina Mungu Na shetani wanatumia Muda Na gharama Sana kutupata.

Hii Hali lazima ilete swali🤔🤔..wao wanapata faida Gani???

Hivi ukiona mfanyabiashara anayenunua dhahabu shilingi laki 1 halafu anauza efu 50 utamuitaje??
Sijui Kwa wewe ila Mimi ntamuita kichaa.

Sasa kama binadamu tunaakili ya kutofanya biashara isiyo Na faida

Je, Hawa kina Mungu Na shetani Ni wajinga kiasi Gani mpaka watumie resources zote Hizo bila faida???

Kwahyo Msiseme Mungu anaweza kuishi bila binadamu..

Maana kama Ni hivyo Na anafanya vyote hivyo bila faida basi yeye Ni kichaa ....

Kwahyo inabidi mchague Kati ya kusema Mungu hufanyA vyote hivyo Kwa faida Na anatula Sisi binadam ili yeye aendelee kuwepo...Au Mungu Ni kichaa
 
Ukijua Mungu ni nan na shetani ni nan na umuhimu wao Kwenye maisha wala hutapata tabu
 
lakini kweli, nikiona wazee walivyochoka kwa uzee, kuna muda natamani nife nikiwa na nguvu zangu
tumetofautiana kidogo tuu...mimi natamani sana nionje raha ya uzee nizeeke nione vijana wanavyohangaikia maisha niwashauri...lakini niwe mzee mwenye pesa
 
Huyu kaka kaongea point Sana ..Hivi ulishajiuliza swali, kwanini Hawa kina Mungu Na shetani wanatumia Muda na resources nyingi Sana ili kutuvutia upande Wao?
Mungu anatumia makanisa,wachungaji,kwaya, Misikiti,vitabu, mashehe mpaka makundi kama Al Shabaab ili kujipatia wafuasi binadamu.
Shetani yeye anatumia Pesa,ngono,ulevi,mziki Ni. ili kujipatia wafuasi.(Mungu anatumia mbinu chafu Zaidi)

Yaani Hawa kina Mungu Na shetani wanatumia Muda Na gharama Sana kutupata.

Hii Hali lazima ilete swali🤔🤔..wao wanapata faida Gani???

Hivi ukiona mfanyabiashara anayenunua dhahabu shilingi laki 1 halafu anauza efu 50 utamuitaje??
Sijui Kwa wewe ila Mimi ntamuita kichaa.

Sasa kama binadamu tunaakili ya kutofanya biashara isiyo Na faida

Je, Hawa kina Mungu Na shetani Ni wajinga kiasi Gani mpaka watumie resources zote Hizo bila faida???

Kwahyo Msiseme Mungu anaweza kuishi bila binadamu..

Maana kama Ni hivyo Na anafanya vyote hivyo bila faida basi yeye Ni kichaa ....

Kwahyo inabidi mchague Kati ya kusema Mungu hufanyA vyote hivyo Kwa faida Na anatula Sisi binadam ili yeye aendelee kuwepo...Au Mungu Ni kichaa
sasa tufanyaje ili ivyo vitu visiendelee kutumaliza...?
 
sasa tufanyaje ili ivyo vitu visiendelee kutumaliza...?
Fanya venye roho yako inapenda...ukisikia njaa Kula, ukitaka kulewa Lewa, ukimiss Kanisa nenda kasali Kwa Moyo wote, ukimiss ngono fanya, Fanya chochote unachopenda usiwe mtumwa wa Hawa kina Mungu Na shetani.
fanya venye roho yako inajiskia As long as huvunji Sheria Za Jamii unayoishi
 
tumetofautiana kidogo tuu...mimi natamani sana nionje raha ya uzee nizeeke nione vijana wanavyohangaikia maisha niwashauri...lakini niwe mzee mwenye pesa
Yap,..... ukiwa na pesa sawa...usipokuwa nazo...hao vijana ndio watakaokushaiuri na kukidharau...ni mbaya sana.
 
Kama unavyomfuga kuku na muda wwote unaweza kumchinja, sisi ndivyo tulivyo anytime tunachinjwa tu.

“The gods envy us. They envy us because we’re mortal, because any moment may be our last. Everything is more beautiful because we’re doomed. You will never be lovelier than you are now. We will never be here again.”​

Achilles[emoji91]
 
Mmimi huamini binadamu ni mazao. Sisi ni malighafi lwa kazi fulani za Mungu. Alitupanda anajuwa kazi yetu.

Inawezekana waliotuumba wako kwenye visayari wanakuja kututembelea na vile vispaceship
 
Wewe ni useless kwenye ulimwengu,ni mtu uliyekata Tamara,ni mjinga,Kama ndio unavyowaza,yaani,ulizaliwa,unakula,mwisho kufa na kuzikwa basi!!!huchangii chochote duniani!!
Hutaki kuwa Dangote,Bakheresa,Diamond,Bill gate,martin Luther king,Michel faraday(aliyegundua umeme,unaoutumia kuchaji cm yako,fala wewe).
Sasa kama watu wote wangewaza kama wewe!!hii sayansi na maendeleo angeleta nani!?
Upo duniani kuleta mchsngo wowote,katika nyanja mbali mbali,Ili siku ukiondoka uiache Dunia vzr zaidi ya ulivyoikuta,
Wote tutakufa,we have nothing to loose!!sasa Kuna ubaya gani ukitafuta ukwasi,magsri,majumba,mifugo ukawa nayo Mengi!!mpaka kizazi chako Cha sita kizikute!!ubaya upo wapi??acha kuwa mbinafsi!!?pigika utakaowaaacha wafaidike!ufe ukiwa umepigika,au haujapigika,utaoza tu!!?so why not
Fantastic Broo
 
Huyu kaka kaongea point Sana ..Hivi ulishajiuliza swali, kwanini Hawa kina Mungu Na shetani wanatumia Muda na resources nyingi Sana ili kutuvutia upande Wao?
Mungu anatumia makanisa,wachungaji,kwaya, Misikiti,vitabu, mashehe mpaka makundi kama Al Shabaab ili kujipatia wafuasi binadamu.
Shetani yeye anatumia Pesa,ngono,ulevi,mziki Ni. ili kujipatia wafuasi.(Mungu anatumia mbinu chafu Zaidi)

Yaani Hawa kina Mungu Na shetani wanatumia Muda Na gharama Sana kutupata.

Hii Hali lazima ilete swali🤔🤔..wao wanapata faida Gani???

Hivi ukiona mfanyabiashara anayenunua dhahabu shilingi laki 1 halafu anauza efu 50 utamuitaje??
Sijui Kwa wewe ila Mimi ntamuita kichaa.

Sasa kama binadamu tunaakili ya kutofanya biashara isiyo Na faida

Je, Hawa kina Mungu Na shetani Ni wajinga kiasi Gani mpaka watumie resources zote Hizo bila faida???

Kwahyo Msiseme Mungu anaweza kuishi bila binadamu..

Maana kama Ni hivyo Na anafanya vyote hivyo bila faida basi yeye Ni kichaa ....

Kwahyo inabidi mchague Kati ya kusema Mungu hufanyA vyote hivyo Kwa faida Na anatula Sisi binadam ili yeye aendelee kuwepo...Au Mungu Ni kichaa
You running into the state which has been written with red pen [red]Danger
 
Binadamu hana jipya lolote hapa duniani zaidi ya kuwa ni mazao au mifugo inayofugwa na kile kinachoitwa Mungu ili apata chakula kitakacho muhakikishia uwepo wake.

Kama unavyoona unafuga ng'ombe,mbuzi,kondoo,kuku,bata n.k ili tu mwisho wa siku upate kitoweo.

Pia kama unavyohangaika kulima mazao mbalimbali au kununua chakula ili tu uweze kula na kuishi hapa duniani kwa raha mustarehe.

Basi hivyo ndivyo ilivyo hata kwa Mungu, naye kapanda mifugo yake hapa duniani ambayo ni sisi binadamu ili aweze kujipatia chakula chake naye aweze kusavaivu.

Tofauti ya wewe na Mungu katika kula kile mlichikitengeneza ni kwamba binadamu unakula mwili uwe wa mboga,matunda,mnyama au ndege wakati Mungu anakula nafsi ya binadamu na kuachana na mwili.

Ni hivi wakuu, nafsi ya binadamu ni chakula cha Mungu alichojitengenezea ili aweze kusavaivu. Yaani ni hivi, Mungu anategemea sana nafsi zetu tofauti na tunavyofikilia.

Kama ulivyo wewe vitu vilivyohalibika huli, basi na kwa Mungu ipo hivyo hivyo nafsi zilizohalibika naye hali. Ndiyo maana ukitaka kumuuzi Mungu wewe chafua nafsi yako tu. Kama ulivyo wewe hupendi kupata hasara kwenye mifugo yako na mazao yako, basi hivyo ndivyo ilivyo kwa Mungu naye hapendi kupata hasara kweye mazao yake(nafsi).

Shetani na Mungu wanasifa zinazofanana kwa hiyo wote wanategemea nafsi za binadamu ili waweze kusavaivu. Chanzo cha mgogoro na ugomvi usioisha kati ya Mungu na shetani ni kutegemea nafsi za binadamu ili waweze kusavaivu.

Shetani anahitaji nafsi nyingi kama chakula chake na Mungu naye anahitaji nafsi nyingi kama chakula chake. Kumbe mgogoro kati ya Shetani na Mungu ni mgogoro wa kimaslahi.

Ndiyo maana kwa Shetani nafsi ya binadamu ni kitu cha muhimu sana kama ilivyo kwa Mungu kuwa nafsi ni kitu cha muhimu sana kiliko kitu chochote hapa duniani.

Wazee ipo hivi, leo kuku au ng'ombe wako anapoambiwa umemfuga ili umchinje anaweza akabisha mpaka basi, basi hivyo ndivyo ilivyo hata wewe nikikuambia kuwa hapa duniani huna jipya zaidi tu umefugwa ili nafsi yako iwe chakula aidha cha Mungu au Shetani basi utabisha mpaka utachanganyikiwa.

Dini,sala,swala,dua au maombi ni mbolea tu ya kumwagilia na kuboresha na kufanya chakula cha Mungu(nafsi yako) iwe safi. Kama wewe unavyohudumia mifugo yako na mazao yako ili yasihalibika basi hivyo ndivyo ilivyo kwa sala na swala kwa binadamu.

Mungu na Shetani hawawezi kuwepo kama nafsi za binadamu hazipo. Maana wote wanategemea nafsi hizi ili waweze kusavaivu. Ndicho chakula chao.

Mzee huna jipya hapa duniani wewe ni mazao tu yanayosubiri kuliwa aidha na Mungu au Shetani.

Wewe toka povu tu na kujifanya mjuaji ila huo ndio ukweli.

Hakuna theory hapa wala nukuu ya kitabu chochote maalifa binafsi yanatosha.
umekunywa gongo gani asububi ya leo
 
Back
Top Bottom