Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho


Okay, nadhani ume base sana kwenye assumptions,... Na naelewa sababu ni ukweli kwamba currently hakuna facts za kisayansi ambazo tunaweza kutegemea kama chanzo sahihi 100% cha viumbe.

Naomba niweke tu sawa kwamba, unaposema hayo mambo yangefanyika magically..... Ipo hivi What we often term as magic is, in fact, not magic but merely knowledge that we don't yet understand!
Hujawahi kujiuliza kwamba huenda kila tunachokiona ni cha ajabu labda kina Mjuzi anaejua every detail about it??

Lakini pia unaposema mambo hayapo organized pia inashangaza.... Kwasababu kuna Laws ambazo zipo na lazima viumbe tuzifuate laws hizo,.. mfano Kula, Kulala, Kupumua, Reproduction, ageing, Gender, na physical laws nyingine zinazopelekea results kama having Day and Night, Different seasons... So ulivyosema mambo hayapo organized umeniacha dillema kidogo.
 
Wewe una ongea "ILLUSION" zako hapa halafu kuthibitisha huwezi unabaki kulalamika tu.

Naku uliza hivi, Kitu kama umeweza kujua kipo kwa nini ushindwe kuelezea muonekano wake?

Kama huwezi kuelezea muonekano wake, Huoni una ongea illusion zako zisizo kuwepo?
 
"Ellusion zisizokuwepo" [emoji28][emoji28], Mbona umejileta mwenyewe sasa kwenye point yangu.

Alafu silalamiki nakueleza ili ujijue ulivyo.

Kama kila kitu unahitaji uthibitisho ili uamini au uelewe kichwa chako kitakuja kuburst...Maana kuna mambo mengine hayahitaji uthibitishiwe...Na ukweli hauna haja ya kutetewa ukweli huwa upo tuu siku zote haijalishi unafahamika au haufahamiki...

So nyuzi kama hizi ni za kupotezeana muda tu ndio maana hakuna mwisho wa haya majibizano.

Narudia tena UKWELI huwa hautetewi, ukweli huwa upo tuu.
 

Unajadili mambo pasina maarifa, umesoma logic? unafahamu infinite regress fallacy ni nini?
 

Unafahamu nini kuhusu nadharia ya causality na effect?
 

Unajenga hoja gani aisee, nilikuwa na fikra za aina hii nilipokuwa shule ya msingi ...
 
Kama "Haiwezekani" Dunia isiwe na muumbaji, kwamba lazima awepo aliye iumba "Imewezekana" vipi Mungu asiwe na Muumbaji?

Kama Mungu hana mwanzo, Inashindikana vipi kwa Dunia kutokuwa na mwanzo?

.

Unamzungumzia MUNGU gani kwanza? [emoji23] hoja unazojenga hazimsadifu MUNGU wa WAKRISTO wa WAYAHUDI wala wa WAISLAMU
 

Wataka kutuambia hujui sifa kuu na tofautishi kati ya vilivyo na vyanzo na visivyokuwa na vyanzo?
 

Mimi ni nani?
Mimi ni jina tu.....
Zaidi ya hapo na yanayoendelea ni yeye!!!
 
Okay, nadhani ume base sana kwenye assumptions,... Na naelewa sababu ni ukweli kwamba currently hakuna facts za kisayansi ambazo tunaweza kutegemea kama chanzo sahihi 100% cha viumbe.
Lazima uchukue assumptions fulani kama kuna variables tofauti..., una-assume kama ikiwa hivi outcome itakuwaje kulingana na known facts..., na kama ingekuwa vile basi known facts lazima zingekuwa hivi na sababu hazipo hivi basi haiwezekani ikawa hivi.....
Naomba niweke tu sawa kwamba, unaposema hayo mambo yangefanyika magically..... Ipo hivi What we often term as magic is, in fact, not magic but merely knowledge that we don't yet understand!
There is no such thing as magic..., ndio maana nikasema kwa wale wanaodhani ni muujiza basi mambo yasingekuwa kama yalivyo yaani kuhitaji action fulani ili reaction itokee; a superpower ambayo magically ilitengeneza vitu isingehitaji hivyo vitu vitumie nishati au kuwe na law of the jungle ili huyu aweze kula hiki au kile na kuua kingine for survival, things could have more more abra cadabra...
Hujawahi kujiuliza kwamba huenda kila tunachokiona ni cha ajabu labda kina Mjuzi anaejua every detail about it??
kila ninachokiona cha ajabu au muujiza ninajua kwamba sijajua kinavyofanya kazi na hivyo ninajitahidi kukifahamu sijawahi kuja na jibu rahisi kama ni muujiza kwa kufanya hivyo kila kitu kwangu kingekuwa ni muujiza wala nisingeelewa hata haya ninayoyaelewa....
Lakini pia unaposema mambo hayapo organized pia inashangaza.... Kwasababu kuna Laws ambazo zipo na lazima viumbe tuzifuate laws hizo,..
Kwa muktadha wa hilo jibu nililolitoa ilikuwa ni uzi kwamba vitu vipo organized sababu kuna mtu alivipanga vile..., na mimi jibu langu likawa ana uhakika hivyo vitu vipo organized ? Vitu vitu vilivyo sababu nature / naturally hio ndio a stable state ambayo inatumia minimum energy..., sio sababu mtu amevipanga ukimwaga maji yakwenda kwenye lowest level..., bahari na maziwa yapo kwenye lowest level ukirusha kitu juu kitarudi chini sababu ya gravity..., ukizaliwa utakufa..., ukila lazima uta-excrete n.k.
mfano Kula, Kulala, Kupumua, Reproduction, ageing, Gender, na physical laws nyingine zinazopelekea results kama having Day and Night, Different seasons... So ulivyosema mambo hayapo organized umeniacha dillema kidogo.
Like I said above vipo hivyo sababu ni nature na visingeweza kuwa tofauti na hivyo na sio kwamba mtu / kitu kimepanga viwe hivyo..., ingekuwa ajabu kama kiumbe hai kingeweza kuishi bila kula (kitapata wapi nishati) bila reproduction wala kisingekuwepo..., bila ageing basi kisingekufa wala kungekuwa hakuna sababu ya reproduction sababu specie hio ingejaa gender inabidi iwepo for reproduction reasons..., kwahio the main issue ilikuwa ni kwamba mambo yapo kama yalivyo sio kwamba kuna mtu aliyapanga yawe hivyo bali hio ndio state ambayo ni stable inabidi yawe hivyo..., mfano mzuri ni ziwa..., lipo pale chini na limekaa kwa ule muundo sababu maji yote yanayotoka huku na kule ni pale ndio yanatuhama sababu kuna bonde..... na sio kwamba ilipangwa kwamba hapa yawepo maji na kama litatokea bonde jingine kwa chini zaidi hilo ziwa litahama (naturally)...,

Jua na usiku kama dunia inazunguka at a constant speed kutokana na mvutano na hakuna kitu cha ku-impede hio speed au kuiongeza lazima siku ziwe vilevile na seasons ziwe kama zilivyo sababu ni kama unasafiri baada ya masaa kadhaa utakuwa palepale ulipokuwa jana na juzi sababu safari ni ileile na inakwenda vilevile....

Kwahio point yangu ilikuwa vina-appear vipo hivyo sio sababu mtu alipanga viwe vile bali kuwepo kwake hivyo ni more stable than vingekuwa otherwise
 
Wataka kutuambia hujui sifa kuu na tofautishi kati ya vilivyo na vyanzo na visivyokuwa na vyanzo?
Sio kujua sifa.

Kwanza anza kuelezea na kuthibitisha mwanzo wa hivyo vyanzo.

Kwa nini unadhani kuna mwanzo wa vilivyo na mwanzo?

Pia thibitisha hivyo visivyokuwa na mwanzo, Vimewezaje kutokea tu from nothing?
 
Unamzungumzia MUNGU gani kwanza? [emoji23] hoja unazojenga hazimsadifu MUNGU wa WAKRISTO wa WAYAHUDI wala wa WAISLAMU
Namzungumzia Mungu anaye dhaniwa kuwa ndiye chanzo cha ulimwengu.

Nasema hivi 👇

Mungu huyo hayupo.
 
Unajenga hoja gani aisee, nilikuwa na fikra za aina hii nilipokuwa shule ya msingi ...
Eleza hoja zako basi.

Kama nina hoja za shule ya msingi, Eleza hizo za kwako.

Sio una bwabwaja bwabwaja hapa, Na huja eleza Hoja yeyote.

Una zunguka zunguka tu.
 
"Ellusion zisizokuwepo" [
Huelewi hata maana ya illusion wewe.
Jambo lolote lisilo na Uthibitisho ni Uongo na propaganda tu.

Mawazo ya kufikirika tu.
Na ukweli hauna haja ya kutetewa ukweli huwa upo tuu siku zote haijalishi unafahamika au haufahamiki...
Ukweli unaendana na kujua, uwepo wa uthibitisho (proofs), Evidences, facts na logic.

Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika na mawazo ya kufikirika tu.

Ili kitu kiwe ukweli lazima kithibitishike, na kuwe na evidences zake.

Sio una ongea "imani na illusion" zako hapa una ziiza ukweli.

Hayo ni mawazo yako ya kufikirika tu (maluwe luwe) , imaginations tu.
So nyuzi kama hizi ni za kupotezeana muda tu ndio maana hakuna mwisho wa haya majibizano.

Narudia tena UKWELI huwa hautetewi, ukweli huwa upo tuu.

Nakwambia tena, Ukweli lazima uwe na evidences, proofs na facts.

Maana hata Uongo upo vilevile.
 
Mimi nakumbuka mwanzo wa huu mjadala, kina Infropreneur walisema mambo ya kukisia hayatakiwi. Una hakika na unachokisema na unawezaje kukithibitisha?

Maana unasema ikiwa hivi lazima iwe vile, hoja ya mjadala ni kuwa kabla haijawa hivi kulikuwa na nini?
Kwahio point yangu ilikuwa vina-appear vipo hivyo sio sababu mtu alipanga viwe vile bali kuwepo kwake hivyo ni more stable than vingekuwa otherwise
Kwa nini unaweka hoja yako kwenye urari wa "mtu". Unaposema "sio sababu mtu alipanga viwe vile..." huoni kama unaufanya mjadala uwe chini ya kiwango??

Tunachotaka kujua hiyo "stability" ya huu mfumo mzima inatokana na nini? Mfumo umezuka tu ama kuna muumbaji wake?
 
Mimi nakumbuka mwanzo wa huu mjadala, kina Infropreneur walisema mambo ya kukisia hayatakiwi. Una hakika na unachokisema na unawezaje kukithibitisha?
Unachukua sentensi moja moja na kuibadilisha nimesema assumptions ni lazima katika kujenga premise hata kwenye equation Mfano kama ni number inaweza ikawa ni positive au negative kwahio hata usipojua kama ilikuwa ni negative au positive unasema tu-assume ilikuwa negative lakini sababu jibu ni Positive haiwezekani moja ikawa ni negative sababu negative x negative ni positive iwapo moja tu ni positive basi jibu lisingekuwa negative (kwahio logic inakuleta kwenye ukweli baada ya ku-eliminate all the impossibles au vitu ambavyo they do not add up)
Maana unasema ikiwa hivi lazima iwe vile, hoja ya mjadala ni kuwa kabla haijawa hivi kulikuwa na nini?
Sababu imekuwa hivi tunavyoona sasa basi lazima kipindi kile ilikuwa vile; haiwezi ikawa kama mwingine anavyosema sababu arguments zake they do not hold water...., tuki-pencil kila ambacho hatujui kwamba ni magic hakuna sababu hata ya kuchunguza; ni either hatujui.., Au tunajua yale ambayo ni factual kutokana na kufanya research; forming hypothesis na baadae experiments kuhakikisha kama tunachosema kina ukweli na kama kuna kitu hakipo sawa kuendelea na uchunguzi mpaka kufikia sehemu ambapo things add up....
Kwa nini unaweka hoja yako kwenye urari wa "mtu". Unaposema "sio sababu mtu alipanga viwe vile..." huoni kama unaufanya mjadala uwe chini ya kiwango??
Mtu angepanga iwe vile na ana uwezo wa kupanga iwe vile dunia / mambo yasingekuwa this mechanical na inefficient; yaani ingekuwa 100 percent efficient..., na huenda yale ambayo zamani tulidhani binadamu hawezi kuyafanya au kufanyika sababu ni magical kwamba mfano mama kubeba mimba (ila kumbe hata test tube inaweza kufanya hicho na mtoto kukua nje ya tumbo la mama; Au moyo kwamba ni kitu delicate sana (ila kumbe mashine tu inaweza ikafanya pumping) and the list goes on and on.....
Tunachotaka kujua hiyo "stability" ya huu mfumo mzima inatokana na nini? Mfumo umezuka tu ama kuna muumbaji wake?
Stability ndio hio nimekwambia imefikia hapo through years of adaptation mfano sababu mimea inahitaji jua kukamilisha Photosynthesis majani yake yanakaa perfectly ili kuvuna jua..., sumaku zinajipanga north pole na south sio sababu zikae vile bali sababu unlike attracts; mbegu za mapera ni ngumu ngumu sio ili zipendeze bali mpandaji wake kwa miaka mingi alikuwa ni mnyama anayekula na akijisaidia mapera yanaota; Maua yana nectar au vitu vinavyovutia aina za wadudu ili waweze kusaidia propagation yake.... Na vile vilivyo-succeed katika ecosystem iliyopo ndio vipo leo vingine naturally vilikuwa au vitakuwa extinct
 
Walau tuwe na "focus" ya mjadala.

Binadamu amekuwaje hivyo alivyo??

Wapo ambao wana mkatale tu kuwa binadamu hakuumbwa.

Lakini wapo watu kama kina Infropreneur ambao wao Wanasema binadamu yupo tu Wala hana mwanzo wala mwisho.

Wapo kina Logikos ambao wao wanatumia nadharia nyingi za kisayansi kuonesha kuwa hali Iko hivi kwa kuwa tu Iko hivi na kwa kuwa haiko kivingine basi hakuna sababu ya kutafuta ilikuwaje kabla au ingekuwaje kama isingekuwa hivi ilivyo Sasa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…