hateeb10
JF-Expert Member
- Dec 8, 2022
- 2,920
- 1,223
Unajua ukiangalia nature kwa jicho la Nishati utaona kwamba kila kitu kinataka kuwa kwenye equilibrium kuna mada mtu mmoja alishasema kwamba mambo yapo organized na hivi ndio nilivyomjibu......
Organized ? Una uhakika mambo yapo organized ?
Ukiagusha sumaku mwisho wa siku zitajipanga sio sababu ya kutaka kuwa organized bali sababu unlike attracts and like repels....
Maua yapo vile sio wewe umpe mpenzi wako bali nyuki anavyochukua chakula aweze kuyachamvua hence propagation...; ukimwaga maji yatatafuta level yake...., (Nature abhors a Vacuum) kwahio kila kitu kipo kama kilivyo sababu kulivyo kwake ni state ambayo inatumia nishati minimum (efficient)
Haya mambo yangefanyika magically tungekuwa hatuhitaji kula, wala kuua vingine ili sisi tuishi..., Yaani kuchukua miezi kadhaa ili kitu kikue (kuku kulalia yai / badala ya kufanya mengine) n.k. Hayo yote yangefanyika bila kuhitaji process zote hizo; Pia ukiangalia sana kila kitu hai unachokiona ni hydrogen, oxygen, carbon, and nitrogen. Na hata wewe leo ukiweka chupa tupu na kuifunika baada ya muda utaona life form humo ndani (hio sio necessarily kwamba wewe ndio ulitengeneza) na kuna vitu ambayo hapo kale vilikuwa havipo (new species) je Mungu ameamua kurudi kuumba au anaumba kwa hatua.....
Mimba anashika mama sababu ni efficient na ana viungo vya kuweza kulea huyo mtoto mwanaume hata kwa bahati mbaya DNA ikikosea na akawa ana Organs mbili hio itakuwa kama kilema na huenda organ ya pili isifanye kazi lakini ikifanya kazi na akawa more efficient huenda wenye organ moja wataisha either kwa manual selection kwamba watu kuona kwanini niwe na mwenza na nisimalize mtoto mwenyewe hence binadamu wa mume na mke kuisha naturally au huenda wasidumu sababu watu watawaona kama kituko hence wasipate partners au kuwauwa..., au kutokea vita kuuwana baina ya hawa na wale.... (hapo nakupa short version ambayo haiitaji miaka trillion kadhaa au umri mwingine wa dunia kama huu wa leo ili major changes kutokea.....
Hakuna mtu aliyesema hakuna intervation iliyotokea huenda kuna some exact voltage ilitokea katika kipindi fulani cha maturity ambacho huenda hakikatokea tena kwamwe..., ndio maana nikasem tuki-rewind tena huenda mambo yasiwe kama yalivyo sasa (sababu kuna so many variables) ila ikishatokea ndio hivyo kama kilichotokea ni more efficient (kwa utumiaji wa nishati) basi kitaendelea hivyo kuliko kile kilichotokea kabla....., ila mazingira yakibadilika na kukawa kuna happenstances za aina fulani zinazotokea mara kwa mara basi usishangae matokeo ya kitu fulani yakawa hivyo na kuendelea (Kumbuka DNA inajicopy) information inakuwa transferred sasa kama information inasema HUYO NI MKE, HUYO NI MKE, HUYO NI MKE na bahati mbaya kwenye ile K ikaprinti M na kuwa MME badala ya MKE copies za coming informations zote zitakuwa MME sasa kama MME atakuwa more efficient unategemea what will happen....
Hata kama ODDS ni Moja katika Occurences MILIONI 30 na dunia ina miaka kama milioni Hamsini huoni kama uwezekano wa kilichotokea kutoa is a highly possibility (tena kutokutokea itakuwa ni jambo la kushangaza yaani ni kama UNA-BET kwamba jambo linalotokea mara moja kwa miaka 30 halitatokea kwenye miaka 50
Ndio maana nikasema hivi does nothingness really exists na kwa wale wanaoamini kwamba kulitokea mlipuko mdogo (Big Bang) ambayo explosion hio huenda ilicreate elements as we know them..., sasa uwepo wa hizo elements na game of chance ulipelekea kuungana tofauti tofauti au kutengana na na mwisho wa siku huenda life form ilianzia hapo
Cha kujiuliza hio volume ilitokea wapi na universe ina mwisho au universe ilikuwa haipo bali hii explosion inavyoexpand ndio inacreate volume au kuna explosions nyingi nyingi zimetokea sehemu tofauti tofauti (Huo ndio uzuri wa sayansi sio kusema kwamba wanajua kila kitu bali wanatafuta majibu kwa kile wasichokijua na kuendelea na utafiti na wakigundua kwamba walikosea wanasem tulikosea) Tofauti na watu wa Imani wakiona walikuwa wamekosea wanatafuta explanation iendane na maelezo yao ya awali au kusema tu ni Magic....
Wote tukiwa na mtizamo wa kutafuta ukweli tutafika mbali lakini tukiwa na mtizamo wa kusema ni magic au fulani alitwambia hivi huenda mpaka leo tungekuwa hatujengi Sky Scrappers kwa kuongopa kumkasirisha Mungu (ili eti tusiadhibiwa kama watu wa Babeli na Mnara wao)
Okay, nadhani ume base sana kwenye assumptions,... Na naelewa sababu ni ukweli kwamba currently hakuna facts za kisayansi ambazo tunaweza kutegemea kama chanzo sahihi 100% cha viumbe.
Naomba niweke tu sawa kwamba, unaposema hayo mambo yangefanyika magically..... Ipo hivi What we often term as magic is, in fact, not magic but merely knowledge that we don't yet understand!
Hujawahi kujiuliza kwamba huenda kila tunachokiona ni cha ajabu labda kina Mjuzi anaejua every detail about it??
Lakini pia unaposema mambo hayapo organized pia inashangaza.... Kwasababu kuna Laws ambazo zipo na lazima viumbe tuzifuate laws hizo,.. mfano Kula, Kulala, Kupumua, Reproduction, ageing, Gender, na physical laws nyingine zinazopelekea results kama having Day and Night, Different seasons... So ulivyosema mambo hayapo organized umeniacha dillema kidogo.