Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Umewaza kitoto sasa,ulimwngu mzima ni dunia tu?? Wakati kuna matilioni ya sayari,nyota zote zipo kwnye dunia? Wakati kuna manyota makubwa mara mabilioni ya dunia .fanya tafiti kabla hujaandika ujinga
Mi nadhani we ndo ungefanya utafiti kabla ya Kujiona una ufahamu wa kila kitu kutoka vitabuni na tv na maigizo, sitarajii kama utakuwa na uwezo wa kufahamu kitu nje ya maandiko ya science.
Mimi nna zaidi ya miaka kumi ya utafiti wa uhalisi dunia na mambo tunayofundishwa na science na dini

Narudia tena hakuna nje ya dunia wala hakuna outer space na hata kama ipo sisi hapa duniani hatuwezi kujua, wala hakuna combo chochote kinachoweza kutoka nje ya dunia,ndio mana science inafanya maigizo ya rocket na kila mwaka kuna movie za outer space zaidi ya 5 ili kugandisha aidia za outer space akilini mwa watu

ifikirie hii dunia kama yai, ipo sealed kama yai, nothing comes in and nothing can go out. Kuingia duniani kuzaliwa tu na kuondoka ni kifo hakuna njia nyengine. Ina ukubwa gani? No one knows, ina umri gani? No one knows.
Wala dunia sio syari wala hairuki na kuelea wala haina mzunguko hata mmoja ipo tuli imetulia milele, lakini kila mtu Ana haki ya kupumbazwa na kuamini anachoona kinafaa kwa akili zake
 
Wewe ulitumia mtazamo gani tofauti na wa kibinadamu, kujua Mungu yupo?

Mtazamo wako huo ulio utumia kujua Mungu yupo, Unaweza kumthibitisha Mungu huyo yupo kwa namna gani?

Na si mawazo yako ya kufikirika tu?
Inaonekana neno "mungu" limekufanya kuwa hauko sawa kisaikolojia....

Nmesoma hii mada muhandishi hakuna sehemu amemtaja Mungu, Lakini tayari kwenye replies zako unataja sana neno Mungu na unamuuliza maswali kwamba amejuaje kuwa Mungu yupo ?

Simamia kwenye mjadala wake, anazungumzia kuhusu chanzo cha binadamu,, Wewe usiende mbali kuanza kumzungumzia Mungu wakati mada inamuhusu binadamu.
 
Duh! Kuna mambo nlikua nakubaliana na wewe ila gafla kuna mambo umeandika nmejikuta sipo pamoja na wewe.. Kuna maswali nkikuuliza hautoweza kunijibu kamwe.
 
Hujawahi sikia mtu kaota fulani kafariki na akafariki? Na huyo mtu hakuwa mgonjwa? Aliona, kusikia au kuambiwa wapi kuwa huo msiba unakuja?
 
Hiyo ni reasoning nzuri. Kama ingekuwa siyo yule aliyetuwezesha kuishi, basi tungekuwa na uwezo wa kukataa kifo, lakini kwakuwa huu uhai tulipewa, basi hatuna uwezo wa kuukatalia tubaki nao; akiutaka mwenyewe anauchukua na hatuweki pingamizi lolote. Kiranga anapotosha sana watu kwa theories zake (sijui anazitoa wapi), namshauri afanye reasoning ya argument hii, huenda atapata kitu hapa.
 
Duh! Kuna mambo nlikua nakubaliana na wewe ila gafla kuna mambo umeandika nmejikuta sipo pamoja na wewe.. Kuna maswali nkikuuliza hautoweza kunijibu kamwe.
Hatuwezi kukubalina kwa kila kitu, viwango vyetu vya ufahamu vipo tofauti, pengine wewe upo mbali zaidi ya mimi au mimi nipo mbali zaidi ya wewe.
Ila kama una swali unaweza kuuliza
 
Kwani tofauti na Mungu ni chanzo kipi kingine ninyi mnakijua?

Mimi nasema hivi👇

Binadamu na dunia Havina mwanzo.
 
Hapa Nina swali ambalo sijibiwi ingawa naona kama ni swali rahisi.

Ili useme hili jambo ni baya ama jema unatumia kigezo gani na kinatokana na msingi upi??
Jambo baya ni kitu chochote kile ambacho wewe hutaki utendewe na binadamu mwenzako.

Jambo zuri ni kitu chochote ambacho unapenda kuona kikifanyika au ukifanyiwa.

Msingi wa mambo haya ni Asili ya kila binadamu alivyo kwamba, Hakuna binadamu anaye taka kufanyiwa kitu asicho penda (kibaya kwake) na kila binadamu hupenda kufanyiwa kitu anacho kipenda (kizuri kwake).

Kuna mambo ambayo Automatically kila mwanadamu anajua ni mabaya.

Mfano mauaji, wizi, ubakaji n.k

Mambo haya hayahitaji kigezo chochote au msingi wowote ili yaonekane ni mabaya.

Kwenye fikra za mwanadamu mambo haya automatically ni mabaya.
Hayo uliyoyaorodhesha hapo Yana shida gani?

1. Ukatili unaujuaje na kwa vipi uwe ni kitu kibaya?
Ukatili ni matendo ambayo Automatically Hakuna mwanadamu yeyote yule anataka atendewe au
ya mtokee.

Ubaya ni matendo yote ambayo kila mwanadamu hayapendi na hataki kabisa yamtokee.
2. Uovu unapimwaje?

Uovu unapimwa kwa matendo yote ambayo wanadamu wengi hawataki kufanyiwa kabisa.
Mfano mauaji, Hakuna binadamu yoyote yule anapenda kufa, Wizi hakuna anaye penda aibiwe. n.k
3. Kwani majanga ya dunia chanzo chake ni Nini?
Majanga ya dunia ya asili au?
 
Unaweza ukawa upo sahihi, ila nakuhakikishia hao jamaa wawili wanajuana[emoji1]na mara zote wanakutana kwenye mada zinazohusisha Mungu na dini.
Hajakosea kujibu ndio mana aliyejibiwa kakaa kimya. Waache
 
Jambo baya ni kitu chochote kile ambacho wewe hutaki utendewe na binadamu mwenzako.
Kwani jambo baya kwako ni Lazima liwe baya kwa mwingine??
Jambo zuri ni kitu chochote ambacho unapenda kuona kikifanyika au ukifanyiwa.
Kanuni gani inatumika kuonesha hili ni jambo zuri??
Msingi wa mambo haya ni Asili ya kila binadamu
Hiyo asili ya binadamu chanzo chake ni nini na chanzo hicho chanzo chake ni Nini?
Kuna mambo ambayo Automatically kila mwanadamu anajua ni mabaya.
Automatically kivipi? Yaani inakuwaje watu kadhaa kwa pamoja waone jambo fulani ni baya ama zuri?
Mfano mauaji, wizi, ubakaji n.k
Ubaya Wa mauji, wizi au ubakaji unatokana na nini? Kwani mtu akiiba, akiua au kubaka tatizo ni nini?
Mambo haya hayahitaji kigezo chochote au msingi wowote ili yaonekane ni mabaya.
Yaani hakuna msingi wa kusema hili ni baya ama ni jema? Si lazima kuwepo kwa kanuni mahsusi itakayotumika kuonesha huyu yupo sahihi ama hayupo sahihi anapotenda jambo linalohisiwa kuwa ni jema ama baya?
Kwenye fikra za mwanadamu mambo haya automatically ni mabaya.
Chanzo cha hizo fikra ni Nini?
Uovu unapimwa kwa matendo yote ambayo wanadamu wengi hawataki kufanyiwa kabisa.
Hayo matendo hupimwa kwa kutumia nini. Akili, nafsi, hisia,fikra, Roho, uzowefu au muongozo usiojulikana??
 
na mara zote wanakutana kwenye mada zinazohusisha Mungu na dini.
Kwa mfano huwa tunakutana uchochoroni kuvuta bangi, basi hadi kituo cha Polisi tukikutana tumekamatwa kwa kuendesha gari hovyo wewe ndiyo ulete habari kuwa huwa tunavuta bangi pamoja??
 
Kwani tofauti na Mungu ni chanzo kipi kingine ninyi mnakijua?

Mimi nasema hivi[emoji116]

Binadamu na dunia Havina mwanzo.
Idadi ya watu duniani inaongezeka kadri muda unavyozidi kwenda, Kwa maana hiyo ilianza na 1 mpaka hapa tulipofikia...Nini unachofahamu kuhusu binadamu huyo wa kwanza kuhusu chanzo chake ?
 
Kwa mtazamo wangu, mabaya na mazuri yanapimwa kwa kutumia hisia na akili.
 
Idadi ya watu duniani inaongezeka kadri muda unavyozidi kwenda, Kwa maana hiyo ilianza na 1 mpaka hapa tulipofikia...Nini unachofahamu kuhusu binadamu huyo wa kwanza kuhusu chanzo chake ?
Maswali ya kimantiki kama hili huwa hawajibu.
 
Kuna viumbe vipo so complicated kuliko binadamu so na huenda wao ni more special kuliko binadamu ... matter of fact ni kwamba huenda pia binadamu ndio kiumbe dhaifu kuliko viumbe vyengine bt how would you know? You can't coz your so dumb kuona wewe upo complicated na special kuliko viumbe vyengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…