Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Kwani unajua chanzo cha punda na kusudi la kuwepo?
 
Sifahamu chochote kuhusu chanzo chake.

Kama una kifahamu tueleze.

Si lazima binadamu wa kwanza awe na chanzo.
Umeanza kwa kusema haufahamu chochote kuhusu chanzo cha binadamu, mwishoni umemaliza kwa kusema....

"sio lazima kuwe na chanzo" Hapa naona unachanganya mambo mno,
Hii inanipa picha kuwa najadili na mtu mwenye upeo wa kifikra wa namna gani


Lakini pia umesema kama nafahamu nkueleze, Lakini nkikueleza pia unapinga...Kwanini upinge kitu ambacho umekiri wazi kuwa haufahamu ?

Kwanini usifanye tafiti kuhusu ambayo huwa tunakwambia ? Lakini unapinga papo kwa hapo kuonyesha kuwa hauwezi kuwa na mtazamo tofauti na ulionao

Nasema hivi kwasababu tumekutana kwenye uzi mwingine huko.
 
Na chanzo cha jua ni kipi?

Jua hilo, lilitokea tu from nothing?
Sasa hapo jua ndilo lenye majibu sahihi.

Mimi naamini hii dunia ni kipande kilichopasuka kutoka juani. Kikaenda masafa marefu ambako kilibahatika kupoa kwakua kilikua mbali na jua ambalo lina moto wa hatari.

Baada ya kupoa, wale bakteria ambao wanaishi ndani ya hicho kipande, wakaanza kuchomoza kwakua hakuna joto la kuwaunguza. Hapa maana yangu ni, mazingira ambapo dunia ilienda kutulia yanaruhusu uwepo wa bakteria ambao sisi tunaita viumbe hai hawa ambao wanaonekana.

Nasema hivi kwakua nipo huku mashambani. Sehemu zilizochomwa moto hata pasipowekwa mbegu ya aina yoyote, pakimwagiliwa maji, panaota majani/mimea.

Hili linatosha kunithibitishia kuwa dunia ni kipande cha jua kilichopoa na bakteria ambao ni sisi viumbe hai, tukachomoza na kuendelea na maisha kwakua hakuna kikwazo cha kutuangamiza tukapotea.

Huu ni mtizamo wangu
 
Kwa hiyo kumbe ndoto ni michezo ya ubongo tu[emoji1][emoji1][emoji1]basi ubongo una ujinga mwingi sana
 
Mkuu kutokufahamu jibu la jambo fulani hakukufanyi uamini tu chochote unachoambiwa bila uthibitisho, hivi unafahamu kwamba si lazima mtu ajue jibu la 1÷0 ili ajue kwamba jibu haliwezi kuwa 1, yeye akisema ni Undefined maana yake hakuna jibu hivyo hahitaji kuthibitisha chochote ila wewe ukisema jibu ni 1 basi utatakiwa ulete uthibitisho wa hilo jibu

Au vile vile pia haihitaji mtu amjue rais wa marekani ili ajue kwamba rais wa marekani hawezi kuwa John Magufuli, sasa huwezi kusema eti kwa sababu humjui rais wa marekani basi uwaamini hata wanaokuambia kuwa ni John Magufuli, wakati hakuna uthibitisho na unaona kabisa ni kitu ambacho hakiwezekani

So vivyo hivyo haihitaji mtu kujua chanzo halisi au sahihi cha Ulimwengu ili ajue kwamba chanzo chake siyo Mungu, sasa huwezi kusema eti kwa vile hujui chanzo cha Ulimwengu basi wanaosema kuwa chanzo chake ni Mungu ndio wako sahihi wakati nao hawajathibitisha, by the way mimi naamini Mungu yupo ila nilikuwa namsaidia tu Jamaa kujibu
 
Napinga, Kwa vile Mnashindwa kuthibitisha uwepo wa hicho chanzo.

Mnaishia kusema tu kipo, Na mnafahamu kipo ila kukithibitisha Hamuwezi.

Sifahamu chanzo cha dunia, ila mnapo anza kusema kitu fulani ndicho chanzo Halafu ninyi wenyewe Hamuwezi kukithibitisha hata na ninyi hamfahamu vilevile.

Mnacho jaribu kufanya ni kuhalalisha mawazo yenu yaonekane yana ukweli bila uthibitisho.


Kwanini usifanye tafiti kuhusu ambayo huwa tunakwambia ? Lakini unapinga papo kwa hapo kuonyesha kuwa hauwezi kuwa na mtazamo tofauti na ulionao
Nimefanya tafiti na kubaini hakuna chanzo chochote kile cha ulimwengu na Binadamu.
Nasema hivi kwasababu tumekutana kwenye uzi mwingine huko.
 
Naona tumo kwenye njia yenye tanuri la fikra pofu na kutoka humo ni Lazima watu wakubali kujitoa kwenye ugoto wa fahamu zao Kwa kuukubali ukweli wenye kweli ndani yake?
 
Nimefanya tafiti na kubaini hakuna chanzo chochote kile cha ulimwengu na Binadamu.
Kwanza kumbuka kuwa hoja hapa tunazungumzia binadamu na siyo kitu kingine chochote.

Hebu elezea huo utafiti uliufanya kwa kutumia mbinu zipi za kiutafiti??
 
Kwahiyo nkikupa njia za kufuata ili upate uthibitisho upo tayari ?
 
Uliyotaja kwa nyani pia yapo mkuu
 
Naona tumo kwenye njia yenye tanuri la fikra pofu na kutoka humo ni Lazima watu wakubali kujitoa kwenye ugoto wa fahamu zao Kwa kuukubali ukweli wenye kweli ndani yake?

Mkuu unge uweka huo ukweli hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…