Hili ndilo tatizo la mijadala ya humu JF. Kuna watu wanatakatifusha Kanuni zao bila ya sababu!!
“Kila kitu lazima kina chanzo chake”
In ver simple logic ina maana sentensi hii itatengeneza series ya infinity.... yaani kila kilichopo kimeundwa na aliyeunda kaundwa na yeye kaundwa pia.... infinity
Sentensi yenyewe ni KANUNI tayari
Labda sasa mtuambie maana ya hiyo sentensi
Unapaswa kujua kwamba kiini cha mgogoro wa “infinity” kilianzia hapa.
Ni tabia ya kibinadamu kutaka kujua kila kitu kwa kujiuliza maswali...... it called intelligence
Kitambo sana kabla yetu watu walianza kujiuliza haya mswali ya nani kaumba binadamu na mpangilio huu, nani kaumba dunia na mpangilio huu, nani kaumba ulimwengu na mpangilio huu nk nk?...... yaani inaonekana haiwezekani vikajipangilia vyenyewe tu kwa mpangilio huu wa ufanisi na complexity ya hali ya juu kabisa(hapa kanuni ikaanza kuibuka kwamba “LAZIMA” kuna aliyeumba na HAIWEZEKANI vikajiumba)
Jawabu likawa ni Mungu maana fikra(kanuni) zilikua zinakataa kwamba hayupo ambaye kaumba vyote
Lakini baada ya dhana ya Mungu muumba wa vyote kuibuka lakini bado binadamu akaanza kupata maswali mapya...... sasa na huyu Mungu mwenye uwezo mkubwa namna hii katokea wapi? Nani kamuumba na yeye?(muendelezo wa kanuni)
Ukiangalia hiyo series ya maswali inajengwa na kanuni ya swali la kwanza ambalo lilitokana na kwamba “haiwezekani” huu ulimwengu ukawa ulitokea tu “LAZIMA” kuna aliyeutengeneza
Alipopatikana aliyeutengeneza kanuni ikamuhusu na yeye pia...... kwamba “haiwezekani” huyu mungu akawa ametokea tu from no where kama ilivyokuwa haiwezekani ulimwengu ukatokea from no where
Ukweli ni kwamba BINADAMU HAJUI KILA KITU na hana majibu ya maswali yoko
Binadamu anachofanya kwa mambo asiyo yajua huwa anatengeneza theories mbali mbali kama big bang theory
Au anamtengeneza “mungu” ili kupata majibu rahisi kwa mswali yaliomshinda
KILA KITU LAZIMA KINA CHANZO ni KANUNI na ndio maana hata wewe unauliza kwanini watu tuamini eti binadamu hajulikani alipotokea wala hajulikani aliyempangilia?
Ni kanuni ya ndio ina kusukuma kutokubaliana na wanaotuaminisha binadamu hajulikani alipotoka