Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Wapo kina Logikos ambao wao wanatumia nadharia nyingi za kisayansi kuonesha kuwa hali Iko hivi kwa kuwa tu Iko hivi na kwa kuwa haiko kivingine basi hakuna sababu ya kutafuta ilikuwaje kabla au ingekuwaje kama isingekuwa hivi ilivyo Sasa!!
Na hicho ndicho ulichotoa kwenye nilichosema ?

Nimekwambia mwanzo wa viumbe hai vyote ni unicellular wala hakuna ajabu ya Binadamu kuwa hivi kama hakuna ajabu ya Tembo au Mkaritusi kuwa kama vile ulivyo.., ukiangalia mambo from simplicity hata hayo ambayo ungeyaona ni complicated utakuwa umeya-simplify sana...

Ni Hubrus tu ya binadamu na kujipa moyo na ku-justify uharibifu wake wa ecosystem kwa viumbe vingine kujipa moyo kwamba yeye ndio muhimu zaidi na yupo hapa kutawala wengine... (Huenda tungekuwa tunaongea Ki-bacteria au Ki-Simba au Tembo huena na wenyewe wana-think the same)..., Anyway any specie ipo pale for their survival....

Na building blocks za viumbe hai vyote ni zile zile (elements)
 
Majdala Unapoendelea naendelea Kuwaza tu... Huu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ukoje.

Kuanzia kinywa kinachokula, koromeo linalomeza chakula, ulimi unaoonja ladha ya chakula, jinsi tumbo linavyogawanya virutubisho kwenda sehemu mbalimbali za mwili, Kwa kweli inastaajabisha.

Ukiangalia viungo vya mwili kama Ini, Kongosho, Figo, Moyo, mapafu, mishipa ya damu, ubongo, hata bandama jinsi vinavyofanya kazi kwa mpangilio, halafu kuwe hakuna mbunifu wake, inashangaza sana!!
 
Ukitaka Kuelewa Sisis Binadamu ni nani na Purpose yetu ......Nenda kafanye Research ya Sauti (Sound) na Ubongo na vinavyohusika na Ubongo.

Ukijua Ndani ya Mwili wako Sauti inatoka Wapi mpaka Ukaweza kuumba maneno basi umemaliza Ku Decode your Origin.
 
Ukitaka Kuelewa Sisis Binadamu ni nani na Purpose yetu ......Nenda kafanye Research ya Sauti (Sound) na Ubongo na vinavyohusika na Ubongo.

Ukijua Ndani ya Mwili wako Sauti inatoka Wapi mpaka Ukaweza kuumba maneno basi umemaliza Ku Decode your Origin.
Kwa ivo sauti inakotoka ndiko kwenye ufunguo wa kumaliza utata wa asili ya binadamu uliko?
 
Tatizo watu wengi hutaka kuonesha kwamba binadamu hana upekee wowote ule dhidi ya "wanyama" wengine kama yeye.

Wenye hoja hii Wanasema binadamu anajikweza tu, ila hana tofauti yoyote ile na chura au kunguru.
 
hata magar yakitazamana saiv jinsi yalivyo mengi barabarani yatakuwa yanasema hivi hivi kuwa sisi (magari) hatuna mwanzo wala mwisho tupo tupo tuu hatueleweki na tutaendelea kuwepo barabarani siku zote ...hayo magar hayajui kuwa kuna gari la kwanza lililo vumbuliwa na kiumbe ambaye ni binadamu..... bila shaka haya magari yatakuwa yanajidanganya tuu pasipokujua aliyeyavumbua (binadamu) akitaka anayatoa barabarani muda wowote na kuyaharibu au kuyatengeneza tena kama atakavoona yeye mwenyewe
Huu mfano haufananii wala
 
Huu mfano haufananii wala
Ukizama Kwa ndani utaelewa. Alichokuwa anamaanisha kuwa hakuna kitu kisicho na muumbaji/mtengenezaji wake.

Lakini hivyo vlivyoumbwa/kutengenezwa haviwezi kujua viliumbwaje/vilitengenezwaje.

Kabla ya kuumbwa viumbe haviwezi kujua vilikuwaje au kabla ya kutengenezwa haviwezi kujua vilikuwaje kabla.
 
Logikos kwa ivo unataka kutuambia hizo "elements" chanzo chake ni nini??
Sio kudhani tu inaweza ikawa proven scientifically kwamba elements zinaweza kutokea kwa particle accelerators na nuclear reactions...

Nyingine zinaweza kupatikana kutokana na mlipuko na ndio maana hata theory ya Big Bang ina-make sense, kwahio utaona yote haya ukiweza kuya-create kwenye laboratory unaweza ukapata jibu la nadharia yako...

Mfano watu walikuwa wanashangaa kwamba hizi almasi kuna mtu alizitengeneza ila kumbe ukichukua carbon hata kwenye maabara kwa pressure kubwa na heat unapata almasi bila shida yoyote....

Ila shida ya going on that road utaniuliza nani alileta huo mlipuko...; Kwahio mantra yangu ni kwamba kuna Known Knowns (vitu ambavyo tunajua tunavijua) na kuna Known Unknowns (vitu ambavyo tunajua hatuvijui) and in all that scenario hakuna chenye jibu la kwamba ni Magic....

Kwahio cha kushangaza zaidi ni with all these knowledge we now have na uwezekano wa kuchunguza kwa kutumia nyenzo mbalimbali watu bado tunaamua kushikilia mazingaombwe...... (and that is a Big shame sababu hata our fore fathers wangefanya hivyo huenda bado tungekuwa tunazikwa na wafalme ili twende kuwatumikia huko waendako)
 
Nikiangalia maumbile ya binadamu na jinsi anavyoishi kwenye hii dunia, najiuliza imekuwaje amekuwa alivyo na jinsi hakuna kiumbe kingine kinachofanana na Binadamu kiutendaji wake.

Ukiangalia Kwa mfano, hivi kweli hakuna mbunifu wa binadamu ambaye ndiye aliyebuni uke ukae kwa mfumo ambao unaweza kuingiliwa na uume.

Hakuna mbunifu aliyebuni mji wa uzazi Kwa mwanamke na kuweka mbegu Kwa mwanaume? Kisha ukifanyika uingilianaji mimba inatungwa.

Baada ya binadamu kuzaliwa ukiangalia kwa makini unaanza kujiuliza, hakuna kweli mbunifu aliyejua kuwa binadamu Ili aishi atahitaji kula hivyo akamuumba akiwa na mdomo?

Mfumo wa kula mpaka kupata haja hakuna mbunifu wake kweli? Yaani mfumo wa mmeng'enyo wa chakula upo tu Wala haukukusudiwa kuwepo ila upo tu. Kweli?

Fikiria macho, masikio, ngozi, na viungo vingine vya binadamu vinavyofanya kazi. Waza kuwa hapa unaposoma hii mada macho, masikio yako yaache kufanya kazi itakuwaje?

Bado nawaza imekuwaje binadamu hana Mwanzo Wala mwisho??
Jibu lake ni ....yupo muumbaji
 
Ukizama Kwa ndani utaelewa. Alichokuwa anamaanisha kuwa hakuna kitu kisicho na muumbaji/mtengenezaji wake.

Lakini hivyo vlivyoumbwa/kutengenezwa haviwezi kujua viliumbwaje/vilitengenezwaje.

Kabla ya kuumbwa viumbe haviwezi kujua vilikuwaje au kabla ya kutengenezwa haviwezi kujua vilikuwaje kabla.
Huwezi kujua uliumbwaje, maana ukifahamu tu, utaacha kumpatia maua yake aliyekuumba.
 
chanzo cha wewe ni wazazi wako na chanzo chao ni wazazi wao vivyo hivyo kwa wazazi wa wazazi wako,,,wewe ni mwanzo na tena ni mwisho yaani wewe ndio ALPHA NA OMEGA,piga makofi tafadhali
 
Sio kujua sifa.

Kwanza anza kuelezea na kuthibitisha mwanzo wa hivyo vyanzo.

Kwa nini unadhani kuna mwanzo wa vilivyo na mwanzo?

Pia thibitisha hivyo visivyokuwa na mwanzo, Vimewezaje kutokea tu from nothing?

Oops [emoji23]

Unachokiri kutokukijua ndicho kilichobeba majibu ya maswali yako
 
Sio kujua sifa.

Kwanza anza kuelezea na kuthibitisha mwanzo wa hivyo vyanzo.

Kwa nini unadhani kuna mwanzo wa vilivyo na mwanzo?

Pia thibitisha hivyo visivyokuwa na mwanzo, Vimewezaje kutokea tu from nothing?
Unafahamu nini kuhusu nadharia ya muda, maada na nafasi?
 
Back
Top Bottom