Binadamu walifanya Ibada hata kabla ya hizi Dini

Mi nimekuuliza huyu mtu ni nani unaleta swali lisilo eleweka. Na effect ya dini kwenye imani potofu ni kubwa sana. Watu waliishi kwa imani za ajabu sana miaka ya nyuma. Waliamini kafara na njia zingine za ajabu katika maisha. Mfano mdogo ni namna watu wa Amerika kusini walivyokua wakiishi, nadhani umeshaona kwenye filamu ya Apocalypto, kama bado itafute. Dini zimesaidia sana
 
kwanza futa hiyo dhaifu. Kozi nawe unasema kitu ambacho huna uhakika nacho (Kama unavyoamni) mada inayojadiliwa unaelewa au unakuja na yako...
 
Dini nini?Ni wapi asili ya neno hilo Dini?Katika asili yake neno Dini linamaana ipi kiswahili?
 
Eti filamu maarifa yako madogo sana. Endelea kukaza kichwa siku ukiijua kweli utafurahi. Kafara gani walifanya.

Emu. Ondoa dini uliyonayo kwasasa utaishi au hutapoteza mwelekeo.
 
Lengo la kuwepo dini, lilikuwa ni kuimarisha ustaarabu wa kidunia kwa kuwajengea hofu watu kwa sababu miaka ya nyuma kulikuwa na unyama au ukatili mkubwa kimauaji, ingawa wapo waliotumia kibiashara pia.​
 
Sasa hivi ukatiri upo au haupo? Ustaarabu upo au haupo na dini zipo au hazipo?
Kwahiyo unakubali kuwa dini hizi mbili zilikuja kwa sababu ya utawala na biashara
 
Nitajie mtume mmoja ambae ni mweusi katika hiyo orodha yako. Mnadanganywa sana kupitia dini, na kwa sababu mmedangangwa kwa njia ya imani basi mko tayari kuua ndugu zenu kwa kisingizio cha kulinda dini. Ukristo na uislam zote ni dini za kibinadamu, sio dini za Mungu. Dini ni moja tu inayotambulika na Mungu, nayo ni kutenda mema na kusaidia wale wasiojiweza na kuliitia jina lake MUNGU, basi. Mengine ni mbwembwe zenu tu ambazo hazina maana.
 
Sasa hivi ukatiri upo au haupo? Ustaarabu upo au haupo na dini zipo au hazipo?
Kwahiyo unakubali kuwa dini hizi mbili zilikuja kwa sababu ya utawala na biashara
Ukatili upo ingawa si kama wa miaka hiyo ya kale, pia ustaarabu umeongezeka ingawa si wote ni wastaarabu; lakini pia dini imewezesha watu kutawaliwa na kufanikisha malengo ya watu wengine kiuchumi.

Dr Livingstone alieneza imani ya kikiristu ukanda wa huku kwetu lengo ni kupingana na biashara ya utumwa iliyokuwa ikifanywa na waarabu, kwa kuwaambia hii ni dhambi; lakini kwa upande mwingine wao wakifanya yao katika kuwanyonya hawa waafrika.

Kwa hiyo, dini zililetwa ili kutimiza malengo ya watu kwa kuwajengea watu hofu; na ukishakuwa na hofu ni rahisi kutawaliwa na mambo mengine kuendelea.

Miaka ijayo, hizi dini zote zitapotea; kwa sababu wengi wataanza kujua ukweli.​
 
kwanza futa hiyo dhaifu. Kozi nawe unasema kitu ambacho huna uhakika nacho (Kama unavyoamni) mada inayojadiliwa unaelewa au unakuja na yako...
Dhaifu wakati hoja yako ni dhaifu sana tena huwezi kuongea mbele ya watu wenye akili
 
Nani amekufundisha kuwa jina la mwabudiwa wako kuwa ni Mungu?
Katika Imani ninayoifuata Mimi nawajua mitume Kwa majina Yao zaidi na Wala siwajui Kwa utaifa Wala ukabila wao zaidi.
Labda wewe niambie dini uliyojichagulia kuifuata ya kutenda mema na kuwasaidia wasiojiweza imeletwa na nani? Kupitia njia hiyo ya dini yako nadhani kulikuwa na Mtume mweusi na ndio maana umeshikamana nayo,je unaweza kutuambia Mtume wako mweusi alikuwa anaitwa nani? Au Kinjeketile Ngwale alikuwa ni Mtume wako?
 
Mimi sidanganyiki. Naamini katika Mungu mmoja, Mungu wa haki na amani. Asie mbaguzi. Asiyesema kuwa bila kumfuata muhamad au Yesu basi huendi mbinguni. Nasisitiza kuna Mungu Mmoja tu wa Haki na Amani na Mungu hana dini.
 
Suala la wewe kujua majina ya mitume wako ni utumwa tu na hakuna maana yoyote. Funguka kijana, badili tabia na acheni kutisha watu.
 
Dhaifu wakati hoja yako ni dhaifu sana tena huwezi kuongea mbele ya watu wenye akili
Sahihi kama ulizaliwa unajua uko sahihi. Kama unakubali ushoga kwakuwa unapata chochote kitu me nikiupinga lazima unione mwenda wazimu πŸ™
 
Amen . Ubarikiwe
 
Sahihi kama ulizaliwa unajua uko sahihi. Kama unakubali ushoga kwakuwa unapata chochote kitu me nikiupinga lazima unione mwenda wazimu πŸ™
naona hauna hoja unaleta mifano haipo kabisa..sijalazimisha ila nimejibu kama hukubali basi haina haja ni free kuamini au kutoamini.

Ila anayejiamini kabisa angebaki na mitazamo yake sio kuleta mada ambayo ukipewa majibu hutaki
 
😁 Living stone akasemaje? Hakuna aliyekomesha utumwa afrika tofauti na Mwaafrika mmoja aliyekuwa anahishi marekani mwisho wake nae aliuawawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…