Bingwa wa kusilimisha Wakristo ameingia Qatar Wakristo wengi wahofiwa kusilimu. Eneo la FIFA lapambwa kwa maneno ya Mtume Muhammad S.A.W

Bingwa wa kusilimisha Wakristo ameingia Qatar Wakristo wengi wahofiwa kusilimu. Eneo la FIFA lapambwa kwa maneno ya Mtume Muhammad S.A.W

PONGEZI; QATAR IMEUPA HESHIMA UISLAM NA UTAMADUNI WA KIARABU

Anaandika, Robert Heriel
Shahidi.

Historia Jana imeandikwa. Tukio la kihistoria katika ukanda wa mashariki ya Kati sio tu limeipa heshima Nchi ya Qatar bali limeupa uislam utukufu na heshima kubwa Duniani. Waislam na jamii zote za kiarabu siku ya Jana wameionyesha dunia kuwa inawezekana dunia ya maadili na ustaraabu/uungwana Kwa kuunganisha tamaduni nzuri zenye manufaa zinazolinda utu wa binadamu.

Uislam hauna mvuto katika mawaidha au mahubiri katika majukwaa ya kutangazia dini au katika propaganda. Lakini Jambo la hakika ambalo uislam unaweza kujivunia na ambalo ndio mvuto wa uislam ni Desturi, sheria na matendo yao.

Qatar wameonyesha mfano Bora Wakuigwa sio tuu na Waislam wengine ulimwenguni bali pia hata na siye tusio Waislam.

Michezo ya mwezi mmoja haiwezi kubadilisha na kuvunja sheria na utamaduni wetu, hivyo ndivyo Qatar walivyofanya.

Ingawaje wapo wenye chuki na Waislam kwa kuwashutumu mambo mabaya kama ugaidi, roho mbaya, ukatili n.k. Lakini hayo mambo hatuyaoni katika ulimwengu halisi wa Kiislam.

Uislam umejengwa katika kufuata Muongozo Mkuu ambao ni Quran, ingawaje niliandika kuwa Quran ilikopi na kuiba maandiko ya kiyahudi Jambo ambalo ni kweli kabisa lakini ninachowasifu Waislam ni uwezo na msimamo wao wa kufuata yale yaliyoandikwa humo kwenye kitabu Chao bila kujali yaliibiwa au hayakuibiwa.

Na wanaweza kutuambia Sisi Wakristo au Mayahudi kuwa ni kweli Sisi Waislam tuliwaibia maandiko yenu kwa sehemu, lakini tunayafuata Kwa 100% hayo maandiko, vipi nyie (Mayahudi na Wakristo) ambao ndio wamiliki halali wa hayo maandiko mnafuata yaliyoandikwa humo yaani kwenye Torati, Zaburi na Injili?

Swali hilo ndilo Waislam wangeweza kujivunia nalo. Ni Sawa na Wazungu au wachina kuiba Teknolojia ya mataifa mengine na kuibadilisha kidogo sio kosa, huo ni ujanja, na Akili. Hivyo ndivyo waislam walivyofanya Kwa upande wa Dini.

Niwapongeze Qatar na Waislam wote Duniani Kwa kuonyesha msimamo thabiti. Na hicho ndicho kinahubiri na kuwasilimisha watu zaidi kuliko kupigapiga kelele kwenye maredio au Television kama Sisi Wakristo.

Matendo ni muhimu zaidi kuliko kelele kelele.
Kataa ushoga hadharani hasa viongozi wa kitaifa.
Kataa mapombe kunywewa hadharani,
Kataa watu kukaa nusu uchi au kutokuvaa Kwa adabu.
Na Sheria Kali zimewekwa.

Wakristo na mataifa mengine tunayomengi ya kujifunza kutoka kwa Waislam. Hata kama tunawaona kama Watoto wa Kambo, au watoto wa hawara lakini wanamazuri yao mengi tu.

Kuhusu tabia mbaya za mtu binafsi ambazo zinachafua Uislam hiyo ni kawaida kuwepo lakini haimaanishi Uislam ni mbaya au dini mbaya.

Hata Shetani alitoka mbinguni kwa Mungu Baba, hivyo haimaanishi mbinguni kuna wadhambi. Isipokuwa zinatokea Error.

Hongereni Sana Watoto wa Mama Mdogo, hongereni Waislam.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam
LICHA YA YOTE HAYO JUZI WALIKASIRIKA TIMU YA ECUADOR KUMUABUDU YESU MBELE YAO BAADA YA KUIFUNGA QATAR. WALILAANI KICHIZ. WAPENDE WASIPENDE YESU ATAABUDIWA TU MBELE YAO.
64749889-11439779-image-a-75_1668967664521~2.jpg


Cc battawi
 
Zamani mlikuwa mnasema Quran ni maneno ya uongo Sasa hivi mnakubali kuwa ni maneno ya ukweli ila mnasema Muhammad amekopi

Mmebakiza point Moja tu kuelewa kuwa Quran ni ufunuo kutoka kwa Mungu muumba mbingu na aridhi (Allah)

By the way Allah anawashangaa Wayahudi na wakristo Kila mmoja wenu anamwambia mwenzake amepotea wakati wote mnasoma kitabu kimoja

Quran 2:113.
Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo. Na Wakristo husema: Mayahudi hawana lao jambo. Na ilhali wote wanasoma Kitabu hicho hicho (Biblia). Na
 
Hapa pongezi ni kwa Qatar sio dini tu! Zipo nchi za kiislamu lakini zina uhuru ila Qatar wamesimamia imani yao bila kuyumba mbele ya pressure ya dunia!

Wametufundisha kuwa ulaya na Marekani sio viranja wa utamaduni wa dunia. Kila Taifa lina utaratibu wake na uheshimiwe.
 
Kuna watu humu wamefurahia sana Qatar kufungwa 😁😁, sababu kuu ni waisilam/waarabu na haswaa kilichowachukiza zaidi ni kupiga marufuku ushoga, pombe, nguruwe n.k
 
Mimi siwezi kukusifia tuu nikaacha kukukosoa madhaifu, huo utakuwa unafiki.

Nikikuponda ujue nitatoa na sifa nzuri Kama unazo.

Ninamacho mawili hivyo kila ninachokiangalia nakiangalia katika pande mbili, Hasi na chanya.
Mimi sio Wale wenye jicho moja wanaoona mambo katika mrengo au upande mmoja tuu.

Kwa hiyo wewe na watu wa Aina yako sioni shida mkiwaza Kwa namna hiyo kwani kabla sijaandika tayari nilijua wapo wasomaji wenye akili zenye single Phase kama wewe. Ungekuwa na Double phases ungeelewa Taikon ni mtu wa Aina gani
huna lolote lamaana usijipe vyeo.
 
Ni kweli dini ya Kikristo inachezewa Sana lakini IPO Imara Kwa sababu inatoa Uhuru Kwa watu kufanya vile watakavyo bila kuwahukumu.
Msingi Mkuu wa Ukristo ni Kristo mwenyewe.
Ukristo umejengwa katika falsafa za Yesu Kristo

Tofauti na Uyahudi uliojengwa katika Falsafa za Musa kwenye Torati.
Huwezi ichezea Torati Kwa maana yenyewe haina falsafa hizo lazima uchapike.

Sasa Uislam umebeba baadhi ya falsafa za Torati ndio maana sio rahisi kuona uislam unacheweza.
Kitu imara hakijawahi kuchezewa hata siku moja.
Huo Uhuru wa kufanya unacho kitaka ndio kumeuangamiza ukristo barani Ulaya.

Kadiri mnavyo ruhusu ichezewe hovyo hovyo ndivyo hadhi yake inazidi kushuka.

Kitu chochote kikikosa udhibiti huwa kinaleta uharibifu.
 
Hapa pongezi ni kwa Qatar sio dini tu! Zipo nchi za kiislamu lakini zina uhuru ila Qatar wamesimamia imani yao bila kuyumba mbele ya pressure ya dunia!

Wametufundisha kuwa ulaya na Marekani sio viranja wa utamaduni wa dunia. Kila Taifa lina utaratibu wake na uheshimiwe.

Kweli kabisa.
Sio ajabu Mpaka sasa mataifa ya Magharibi bado wanachokochoko na kuwaonea wivu na kujaribu kuwachafua Qatar.

Tunalakujifunza.
Qatar wamekataa kujidharau na kudharau tamaduni zao
 
Zamani mlikuwa mnasema Quran ni maneno ya uongo Sasa hivi mnakubali kuwa ni maneno ya ukweli ila mnasema Muhammad amekopi

Mmebakiza point Moja tu kuelewa kuwa Quran ni ufunuo kutoka kwa Mungu muumba mbingu na aridhi (Allah)

By the way Allah anawashangaa Wayahudi na wakristo Kila mmoja wenu anamwambia mwenzake amepotea wakati wote mnasoma kitabu kimoja

Quran 2:113.
Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo. Na Wakristo husema: Mayahudi hawana lao jambo. Na ilhali wote wanasoma Kitabu hicho hicho (Biblia). Na

Shida yenu Waislam ni kudhani dini yenu haina mapungufu. Hilo ndio tatizo Lenu KUBWA.

Sisi wapenda ukweli bila ushabiki tunafahamu kila dini inamadhaifu yake mengi tuu.

Kukataa huko ndiko kunaifanya dini iwe na dosari.
 
Kuna watu humu wamefurahia sana Qatar kufungwa [emoji16][emoji16], sababu kuu ni waisilam/waarabu na haswaa kilichowachukiza zaidi ni kupiga marufuku ushoga, pombe, nguruwe n.k
Wao kwann wazuie watu wengine wasiabudu miungu yao? Jinsi wao wanavoona miungu ya wengine ni takataka ndivo ivo wanaona mungu wao ni takataka....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni unafiki. Jee huyo Allah alikuwa wapi wakati Qatar wanacharazwa mabao 2-0 na Equador nchi ambayo asilimia 92% ni Wakristu (80% Roman Catholics, 11% walokole).
Mashoga acheni makasiriko. Hizo laana zenu mtaenda fanyia huko kwenu. Qatar mkaangalie mpira tu.
 
Hao ni mabinti wa Islamic republic of Iran,wamevua hijab, hawataki upuuzi na maijabu
Sio tatizo kwa sababu wapo pia mabinti wa kiiran wamevaa hijabu hawataki kabisa upuuzi wa kuacha vichwa wazi.
 
Anakuja kuendeleza kitu ambacho hakikuwepo kwenye jamii yake?
ndugu muhammad aliwalingania watu dini(mila)ile ile ya manabii waliopita kama vile ibrahimu.

Allah anamuambia mtume..


[ AL I'MRAN - 95 ]
.قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ

[ AL - AN-A'AM - 161 ]
Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa waswashirikina"

hapo muhammad anaambiwa aseme kwamba hiyo dini ama njia aliyokuja nayo ndio njia ile ile iliyokuwa ya ibrahimu.

Sasa ndugu robert huwezi kuniambia kwamba muhammad alikuja na dini mpya wakati qurani imathibitisha dini aliyohubiri muhammad ni ile ile ya nabii ibrahimu.

Labda wewe ulete uthibitisho kutoka kwenye hii qurani kwamba muhammad alihubiri dini mpya tofauti na ile dini ya manabii waliopita ?
Unaposema Uislam ulikuwepo, niambie kabla ya Muhammad kuwepo au alivyokuwa mdogo waarabu walikuwa wanaujua huo uislam?
Waarabu kutokuujua uislamu hiyo sio hoja kwamba haukuwepo kabla yao,sisi leo kutokujua historia ya tanu sio hoja kwamba tanu haikuwepo.

Sisi leo kutokujua historia ya vita vya maji maji na washiriki wake hiyo sio hoja kwamba vita ya maji maji haikuwepo.

Kutokujua jambo haimaanishi halikuwepo ama halipo,kutokujua ni jambo moja na kuwepo ni jambo jingine ndugu robert.
Walikuwa wanatambua manabii wapi?
Kutokuwatambua manabii hiyo sio hoja kwamba hawakuwepo manabii kabla yao,manabii walikuwepo akina ibrahimu,musaa,issa,yussuf na wengineo hata kama wengi wao hawakutambua historia hiyo muhammad ndio kaja kuendeleza pale paliposahaulika.
Uislam na Quran mungu wake ni Allah na siku ya Ibada ni ijumaa. Torati, zaburi, na injili ya Wakristo na mayahudi Mungu wao ni Yehova na siku Yao ya kuabudu ni Siku ya Saba, SABATO/jumamosi.
 
Shida ni hilo neno kuiba, japo hatujui unamaanisha nini in deep mind ila ukweli ni kwamba Mungu wa Taurat na Injili, Quran nk ni huyohuyo mmoja isipokuwa kutokana ni upotofu wa binadam hizo injili zilikuwa corrupt katika baadhi ya vipengele hivyo ikashushwa Quran ili kuweka bayana. Anyway kama inashindikana kukubaliana hatulazimishani wewe sema injili iliibwa sisi tuseme tuseme haikuibwa bali ni maandiko pia ya Allah (there shall be no compulsion in religion 2:256) halafu baada ya hapo turudi kwenye thread yako ambayo inaujumbe safi ndani yake.
 
Japokuwa umeisifia qatar kwa walichokifanya na kupeleka kongole kwa waislamu umefanya uungwana sana mkuu.

Ila naomba nichangie katika point ya kwamba "UISLAMU KUNA MAANDIKO UMEIBA KUTOKA KATIKA TAURATI,ZABURI NA INJILI".

Ukisoma uislamu ama qurani utaona kabisa mkuu kwamba hivo vitabu vya taurati,zaburi na injili ni katika vitabu vya kiislamu kablya ya qurani.

Hivyo kama rafiki zetu wakristo mnaaema hivyo ni katika vitabu vyenu basi na sisi ndugu zenu waislamu tunasema hivyo ni katika vitabu vyetu pia vya kiislamu.

Na wala uislamu haujaficha kwamba umeiba maandiko ya taurati ama zaburi hapana bali uisilamu umeweka wazi katika qurani kama ifuatavyo.

نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ

[ AL I'MRAN - 3 ]
Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili.

Kumbe yule Allah aliyeshusha qurani ndiyo huyo huyo aliyeishusha taurati na injili.

Hivyo waislamu sio tu kitabu chao ni qurani bali torati,zaburi na injili ni katika vitabu vyao pia kwa sababu Qurani inaonesha kwamba hivyo pia vilishushwa na Allah yule yule wa qurani.

Ila kama kuna tafiti zinaonesha kwamba uislamu uliiba maandiko ya tauratina injili hizo tafiti zitakuwa ni maoni tu lakini kiuhalisia uislamu umekiri wazi kwamba sio kwamba umeiba maandiko kwenye taurati na zaburi hapana bali hizo taurati na zaburi ni sehemu ya vitabu vya kiislamu.

Hivyo qurani imekuwa huru kuelezea yale ambayo yamo katika injili kwa sababu injili na qurani ni marafiki wa baba mmoja.
Hapana hii nakupinga kwa nguvu kabisa,yaani torat kitabu cha wayahudi na kilichoandikwa miaka kibao kabla ya Yesu na kiliandikwa kwa kiebrania,halafu wew wa juzi na dini yako ya kiarabu unakuja kulazimisha watu waamini kuwa torati ni kitabu cha kiislamu hivi waislamu mnamatatizo gani vichwani mwenu!?
 
Back
Top Bottom