ndugu muhammad aliwalingania watu dini(mila)ile ile ya manabii waliopita kama vile ibrahimu.
Allah anamuambia mtume..
[ AL I'MRAN - 95 ]
.قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ
[ AL - AN-A'AM - 161 ]
Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa waswashirikina"
hapo muhammad anaambiwa aseme kwamba hiyo dini ama njia aliyokuja nayo ndio njia ile ile iliyokuwa ya ibrahimu.
Sasa ndugu robert huwezi kuniambia kwamba muhammad alikuja na dini mpya wakati qurani imathibitisha dini aliyohubiri muhammad ni ile ile ya nabii ibrahimu.
Labda wewe ulete uthibitisho kutoka kwenye hii qurani kwamba muhammad alihubiri dini mpya tofauti na ile dini ya manabii waliopita ?
Waarabu kutokuujua uislamu hiyo sio hoja kwamba haukuwepo kabla yao,sisi leo kutokujua historia ya tanu sio hoja kwamba tanu haikuwepo.
Sisi leo kutokujua historia ya vita vya maji maji na washiriki wake hiyo sio hoja kwamba vita ya maji maji haikuwepo.
Kutokujua jambo haimaanishi halikuwepo ama halipo,kutokujua ni jambo moja na kuwepo ni jambo jingine ndugu robert.
Kutokuwatambua manabii hiyo sio hoja kwamba hawakuwepo manabii kabla yao,manabii walikuwepo akina ibrahimu,musaa,issa,yussuf na wengineo hata kama wengi wao hawakutambua historia hiyo muhammad ndio kaja kuendeleza pale paliposahaulika.