Bingwa wa kusilimisha Wakristo ameingia Qatar Wakristo wengi wahofiwa kusilimu. Eneo la FIFA lapambwa kwa maneno ya Mtume Muhammad S.A.W

Bingwa wa kusilimisha Wakristo ameingia Qatar Wakristo wengi wahofiwa kusilimu. Eneo la FIFA lapambwa kwa maneno ya Mtume Muhammad S.A.W

Shida ni hilo neno kuiba, japo hatujui unamaanisha nini in deep mind ila ukweli ni kwamba Mungu wa Taurat na Injili, Quran nk ni huyohuyo mmoja isipokuwa kutokana ni upotofu wa binadam hizo injili zilikuwa corrupt katika baadhi ya vipengele hivyo ikashushwa Quran ili kuweka bayana. Anyway kama inashindikana kukubaliana hatulazimishani wewe sema injili iliibwa sisi tuseme tuseme haikuibwa bali ni maandiko pia ya Allah (there shall be no compulsion in religion 2:256) halafu baada ya hapo turudi kwenye thread yako ambayo inaujumbe safi ndani yake.
Achaneni na huo uongo wenu,hakuna kitu kilichoshushwa zaidi ya binadamu kuandika kwa mkono wake tena kukopi baadhi ya maandiko kutoka biblia na kujimilikisha nyie pia hata biblia kimeandikwa na binadamu kwa msaada wa roho wa Mungu.
 
Achaneni na huo uongo wenu,hakuna kitu kilichoshushwa zaidi ya binadamu kuandika kwa mkono wake tena kukopi baadhi ya maandiko kutoka biblia na kujimilikisha nyie pia hata biblia kimeandikwa na binadamu kwa msaada wa roho wa Mungu.
Sasa wewe unatafuta darasa lingine, hapa tunazungumzia msimamo wa Qatar na kuhusu maandiko kuibwa au kutoibwa. Halafu umejijibu mwenyewe. Haijalishi yawe yameandikwa kwa mkono au la ila mwisho wa siku yameshushwa kama ulivyosema kutoka kwa Mungu kupitia malaika wake labda terminology ya kushushwa ndo inakuchanganya.
 
PONGEZI; QATAR IMEUPA HESHIMA UISLAM NA UTAMADUNI WA KIARABU

Anaandika, Robert Heriel
Shahidi.

Historia Jana imeandikwa. Tukio la kihistoria katika ukanda wa mashariki ya Kati sio tu limeipa heshima Nchi ya Qatar bali limeupa uislam utukufu na heshima kubwa Duniani. Waislam na jamii zote za kiarabu siku ya Jana wameionyesha dunia kuwa inawezekana dunia ya maadili na ustaraabu/uungwana Kwa kuunganisha tamaduni nzuri zenye manufaa zinazolinda utu wa binadamu.

Uislam hauna mvuto katika mawaidha au mahubiri katika majukwaa ya kutangazia dini au katika propaganda. Lakini Jambo la hakika ambalo uislam unaweza kujivunia na ambalo ndio mvuto wa uislam ni Desturi, sheria na matendo yao.

Qatar wameonyesha mfano Bora Wakuigwa sio tuu na Waislam wengine ulimwenguni bali pia hata na siye tusio Waislam.

Michezo ya mwezi mmoja haiwezi kubadilisha na kuvunja sheria na utamaduni wetu, hivyo ndivyo Qatar walivyofanya.

Ingawaje wapo wenye chuki na Waislam kwa kuwashutumu mambo mabaya kama ugaidi, roho mbaya, ukatili n.k. Lakini hayo mambo hatuyaoni katika ulimwengu halisi wa Kiislam.

Uislam umejengwa katika kufuata Muongozo Mkuu ambao ni Quran, ingawaje niliandika kuwa Quran ilikopi na kuiba maandiko ya kiyahudi Jambo ambalo ni kweli kabisa lakini ninachowasifu Waislam ni uwezo na msimamo wao wa kufuata yale yaliyoandikwa humo kwenye kitabu Chao bila kujali yaliibiwa au hayakuibiwa.

Na wanaweza kutuambia Sisi Wakristo au Mayahudi kuwa ni kweli Sisi Waislam tuliwaibia maandiko yenu kwa sehemu, lakini tunayafuata Kwa 100% hayo maandiko, vipi nyie (Mayahudi na Wakristo) ambao ndio wamiliki halali wa hayo maandiko mnafuata yaliyoandikwa humo yaani kwenye Torati, Zaburi na Injili?

Swali hilo ndilo Waislam wangeweza kujivunia nalo. Ni Sawa na Wazungu au wachina kuiba Teknolojia ya mataifa mengine na kuibadilisha kidogo sio kosa, huo ni ujanja, na Akili. Hivyo ndivyo waislam walivyofanya Kwa upande wa Dini.

Niwapongeze Qatar na Waislam wote Duniani Kwa kuonyesha msimamo thabiti. Na hicho ndicho kinahubiri na kuwasilimisha watu zaidi kuliko kupigapiga kelele kwenye maredio au Television kama Sisi Wakristo.

Matendo ni muhimu zaidi kuliko kelele kelele.
Kataa ushoga hadharani hasa viongozi wa kitaifa.
Kataa mapombe kunywewa hadharani,
Kataa watu kukaa nusu uchi au kutokuvaa Kwa adabu.
Na Sheria Kali zimewekwa.

Wakristo na mataifa mengine tunayomengi ya kujifunza kutoka kwa Waislam. Hata kama tunawaona kama Watoto wa Kambo, au watoto wa hawara lakini wanamazuri yao mengi tu.

Kuhusu tabia mbaya za mtu binafsi ambazo zinachafua Uislam hiyo ni kawaida kuwepo lakini haimaanishi Uislam ni mbaya au dini mbaya.

Hata Shetani alitoka mbinguni kwa Mungu Baba, hivyo haimaanishi mbinguni kuna wadhambi. Isipokuwa zinatokea Error.

Hongereni Sana Watoto wa Mama Mdogo, hongereni Waislam.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam
Dini inayolindwa kwa mtutu wa bunduki sio kwa kuamini bali kwa vitisho. Angalia kinachoendelea Iran, Afghanistan....
 
Sasa wewe unatafuta darasa lingine, hapa tunazungumzia msimamo wa Qatar na kuhusu maandiko kuibwa au kutoibwa. Halafu umejijibu mwenyewe. Haijalishi yawe yameandikwa kwa mkono au la ila mwisho wa siku yameshushwa kama ulivyosema kutoka kwa Mungu kupitia malaika wake labda terminology ya kushushwa ndo inakuchanganya.
Hivi unaelewa maana ya neno kushushwa au kuteremshwa!?
 
Ulaya wanashindwa waadhibu vipi Qatar kwa msimamo wao

Kila kukicha wanasema migrant worker, human rights wakati wao ndio walipiga kura na kuichagua wakijua fika ni nchi yenye tamaduni zake na sheria zake
Waache wajifunze tamaduni za wengine maana wengi wamezoea wakisafiri ni ulevi na uzinzi tu hawajui kuna mengi ya kujifunza
 
Nasikitika sana Vatican kuanzisha.

Ushetani.
Masssonic.
ISlamic.

Shetani YUPO KAZINI.
Hii jumapili yenyewe ni ushetani wa Vatican.
 
ROBERT HERIEL saa zingine unakuwa na ushindani mwingi saa zingine unakuwa na fikra yakinifu

Uislamu ni zaidi ya unachokiona qatar, ila kuna mifumo ya kuupa mgongo uislamu kwa wakiristo kutengenezewa bongo movies za ugaidi na majini ili kufanya watu wengine wasitake kusikia kuhusu mafundisho ya uislamu,
 
wewe unacho tafuta nikubishanatu sikuzote kuhusu dini yauisilamu. walahuna jingine kwasababu Kama ni pongezi ungepongezatu mambo yakaisha lakini wewe kwakua unahila umeingiza mambo yako mengine. ila kwakua tusha kujua endeleatu ukichoka utaacha.
Tukiwaambia dini yenu inaendeshwa na mihemko na akili hamna mnakuwa mbogo,kila dini inamapungufu yake na mbona wakristo wanakubali lakini ninyi mkiambiwa kitabu cha mwarabu kilikopi visa vingi kutoka biblia mnakata,mnabaki kulazimisha kuwa uislamu ulikuepo kitambo bila hata uthibitisho wa kina?
 
Tukiwaambia dini yenu inaendeshwa na mihemko na akili hamna mnakuwa mbogo,kila dini inamapungufu yake na mbona wakristo wanakubali lakini ninyi mkiambiwa kitabu cha mwarabu kilikopi visa vingi kutoka biblia mnakata,mnabaki kulazimisha kuwa uislamu ulikuepo kitambo bila hata uthibitisho wa kina?
ok poa.
 
Japokuwa umeisifia qatar kwa walichokifanya na kupeleka kongole kwa waislamu umefanya uungwana sana mkuu.

Ila naomba nichangie katika point ya kwamba "UISLAMU KUNA MAANDIKO UMEIBA KUTOKA KATIKA TAURATI,ZABURI NA INJILI".

Ukisoma uislamu ama qurani utaona kabisa mkuu kwamba hivo vitabu vya taurati,zaburi na injili ni katika vitabu vya kiislamu kablya ya qurani.

Hivyo kama rafiki zetu wakristo mnaaema hivyo ni katika vitabu vyenu basi na sisi ndugu zenu waislamu tunasema hivyo ni katika vitabu vyetu pia vya kiislamu.

Na wala uislamu haujaficha kwamba umeiba maandiko ya taurati ama zaburi hapana bali uisilamu umeweka wazi katika qurani kama ifuatavyo.

نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ

[ AL I'MRAN - 3 ]
Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili.

Kumbe yule Allah aliyeshusha qurani ndiyo huyo huyo aliyeishusha taurati na injili.

Hivyo waislamu sio tu kitabu chao ni qurani bali torati,zaburi na injili ni katika vitabu vyao pia kwa sababu Qurani inaonesha kwamba hivyo pia vilishushwa na Allah yule yule wa qurani.

Ila kama kuna tafiti zinaonesha kwamba uislamu uliiba maandiko ya tauratina injili hizo tafiti zitakuwa ni maoni tu lakini kiuhalisia uislamu umekiri wazi kwamba sio kwamba umeiba maandiko kwenye taurati na zaburi hapana bali hizo taurati na zaburi ni sehemu ya vitabu vya kiislamu.

Hivyo qurani imekuwa huru kuelezea yale ambayo yamo katika injili kwa sababu injili na qurani ni marafiki wa baba mmoja.
Uislamu ulianzishwa na wakatoliki thus maandiko yanaendana
 
Uislamu ulianzishwa na wakatoliki thus maandiko yanaendana
Kusema sio tatizo kwa sababu kila mtu anaweza kusema analojisikia,ishu ni evidence za uhakika za kinachosemwa.

Mimi kusema kwamba uislamu wameanzisha wakatoliki mbona sioni tatizo juu ya kauli hiyo,ishu ni evidence zenye kueleweka za kutilia nguvu usemi huo.
 
Hili tulishahadili Mkuu.

Uislam ni Dini ya kiarabu, na kitabu Chao ni Quran, Mungu wao ni Allah, Waandishi wake ni waarabu.

Uyahudi ni Dini ya Wayahudi na waisrael.

Hawa wanavitabu vingi, kitabu chao kikuu ni Torati, ingawaje vipo vitabu vidogo kama Zaburi, waandishi wake ni mayahudi wenyewe. Mungu wao ni Yehova.

Ukristo ni Dini ya kimataifa lakini imejengwa zaidi na Wazungu, ingawaje wao wameiba maandiko ya Kiyahudi na wahusika wa kiyahudi Kama walivyofanya Waarabu. Vitabu vyao wame- combine Torati, Zaburi na Injili.
Mungu wao Yehova mwenye ushirika na Yesu Kristo.

Huo ndio muhtasari wa dini hizo tatu zenye Asili ya Abrahamu.

Ukristo na uislam hauwezi kukataa kuwa haujafanya copy na ku-paste baadhi ya visa vya Mayahudi.
Labda ushabiki uendekezwe Ila huo ndio ukweli
Inaelekea una kichwa kigumu!!...upo Kama memory card,kilichowekwa humo ndiyo kitakacho-play miaka nenda Rudi,jifunze kupokea vitu vipya!
 
Anakuja kuendeleza kitu ambacho hakikuwepo kwenye jamii yake? Embu kuwa Serious na tumia logic kidogo Mkuu.

Unaposema Uislam ulikuwepo, niambie kabla ya Muhammad kuwepo au alivyokuwa mdogo waarabu walikuwa wanaujua huo uislam? Walikuwa wanatambua manabii wapi?

Ni Sawa atokee Nabii huku Afrika alafu aseme yeye ni muendelezo wa uislam au Ukristo ilhali Afrika hakukuwa na mambo hayo.

Uislam na Quran mungu wake ni Allah na siku ya Ibada ni ijumaa. Torati, zaburi, na injili ya Wakristo na mayahudi Mungu wao ni Yehova na siku Yao ya kuabudu ni Siku ya Saba, SABATO/jumamosi.

Huoni hapo unazungumzia vitu viwili tofauti?

Waislam muwe waungwana tuu Kama Wakristo kuwa mumechukua baadhi ya maandiko yote ya Wayahudi na kuyatumia katika kuunda dini zenu. Hakuna atakayewalaumu. Na mtakuwa mnasema Ukweli.

Lakini hizo garagaja zenu ndizo zinawaharibia, Na kuonekana ninyi ni waongo na uislam ni Uongo.

Unasema uislam ulikuwepo kabla ya Muhammad, haya tuambie ulikuwepo eneo gani Kwa ushahidi wa Aya.

Alafu usijekutaja kina Musa, Yakobo, Daudi, Suleiman, Issa Kwa sababu HAO ni Wayahudi na Mungu WA Wayahudi anafahamika kuwa sio Allah Bali ni Yehova.

Na sheria za Yehova na Allah ni vitu viwili tofauti.
Kwenye uislam hakuna kabila Wala jamii,uislam unatambua binaadam ni wamoja,ndiyo maana hata nabii Adam Allah anamtaja Kama nabii wake,kadhalika nuhu... ambao hawakuwa wayahudi(Kama unavyowaita na kuwaona ni chanzo Cha Imani)....na uislam Hauna siku maalum ya ibada,siku zote ni za ibada,ndiyo maana kuna swala Tano,usiwe unajadili vitu usivyo na elimu navyo,mwerevu na mwenye hekima hujifunza kwanza Jambo asolijua ndiyo akalinenea
 
Uislamu ndio mfumo bora wa haki kwa watu wote kuelekea ustawi wa jumla. Angalau wao wamepunguza au kuondoa ile gap Kati ya mtawala na mtawaliwa kupitia dini,hata msikitini cheo chako ubakia nje nyote mnakua daraja SAwa wakati wa ibada,hawana mambo ya viti vya mbele ni wenye elf 10. Watawala wa kiislamu wanawatendea haki wanaowaongoza thus nchi za kiislamu wananchi wao awaisomi Sana number na hata hizi za kiafrica zenye unasaba na uislamu wananchi wao awaisomi Sana number kama hizi nchi zingine za kiafrica ambazo wananchi wake wanachomeka jikoni. Hivi mfano maisha ya mateso na suluba anayopitia mtu mweusi afrika tangu anazaliwa hadi kifo sababu ubinafsi wa watawala ipo haja ya kwenda tena kuchomwa motoni siku ya mwisho. Maana maisha ya wengi msoto mwanzo mwisho jela si jela kuzimu si kuzimu, hivi kwa msoto huu kipi kipya mtu ataogopa kuzimu. Maana maisha tu ya mtaani ya jela yana nafuu maana jela upo uhakika wa kula na kulala bure.
 
Walioko ulaya wanafunga ndoa kanisani ni waislam?
Wapo wanaofunga ndoa msikitini South Africa, ingia You Tube ujionee.

Siku mkijua imani ni Mtu binafsi na matendo mema ndipo mtajua kuwa hamjui.

Kila siku tuhuma na kesi kwa Mapadri, Wachungaji, Mashehe kulawiti na kuf**a watoto lakini mnabaki kujumuisha tu dini za Watu, hivi hamuoni jinsi gani hamna maarifa?
 
Back
Top Bottom