Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Mi nimekupa tafsiri maana ya neno Allah usijikoroge. Ukisema Jehova sio Allah kwa lugha maana Jehova sio Mungu.
Ungeniambia labda Mungu kwenye biblia ameelezwa tofauti na Mungu kwenye Qur'an hapo ningekuelewa.
Ukichunguza pia Mungu wa agano la kale ni tofauti na agano jipya.
Usisahau wayahudi wa sasa neno wanalotumia kuwakilisha Mungu ni Hashem.
Utakuja kusema Hashem sio Jehova. Hiyo ni katika muundo wa majina. Nilikupa aya kukuonesha kwamba hakika wamekufuru wanaosema Allah/Mwenyezi Mungu masihi mtoto wa Mariamu. Ukiangalia wakristo wengi waliokufuru wanamchukulia Yesu kama Mungu. Wachache sana sidhani hata kama 5% inafika.
Wewe naona hatuelewani.
Kitu kinachofanya miungu kuwa tofauti mbali na majina ni sheria, amri, na kanuni zao.
Yehova alijiita Alfa na omega, akijiita Niko ambaye Niko, alijiita majina mengi lakini Sheria zake hazijawahi kubadilika.
Swali unalotakiwa kujiuliza sheria za Yehova na Allah ni zilezile?
Jibu likiwa ndio basi Allah na Yehova ni mungu mmoja katika majina tofauti.
Ikiwa jibu ni hapana basi ni miungu wawili tofauti.
Ndio maana kuna mwenzako mmoja nimemuambia anitajie amri 10 za Allah alizompa Musa pale Mlimani Kwa mujibu wa Quran ili tuanzie hapo kuona Yehova ndiye Allah?
Hata unaweza kutupa hizo Aya ili mjadala uwe Mzuri na watu waelewe
Ikiwa Allah atakuwa ndiye Yehova basi Mimi kama Muumini wa Yehova nitakuwa Muislam tangu leo hii.
Ila ukishindwa na Mimi nikikuonyesha tofauti za msingi za miungu HAO basi watu wataelewa Allah na Yehova ni miungu wawili tofauti wasiojuana wala wasio na mahusiano