Bingwa wa kusilimisha Wakristo ameingia Qatar Wakristo wengi wahofiwa kusilimu. Eneo la FIFA lapambwa kwa maneno ya Mtume Muhammad S.A.W

Mi nimekupa tafsiri maana ya neno Allah usijikoroge. Ukisema Jehova sio Allah kwa lugha maana Jehova sio Mungu.
Ungeniambia labda Mungu kwenye biblia ameelezwa tofauti na Mungu kwenye Qur'an hapo ningekuelewa.
Ukichunguza pia Mungu wa agano la kale ni tofauti na agano jipya.
Usisahau wayahudi wa sasa neno wanalotumia kuwakilisha Mungu ni Hashem.
Utakuja kusema Hashem sio Jehova. Hiyo ni katika muundo wa majina. Nilikupa aya kukuonesha kwamba hakika wamekufuru wanaosema Allah/Mwenyezi Mungu masihi mtoto wa Mariamu. Ukiangalia wakristo wengi waliokufuru wanamchukulia Yesu kama Mungu. Wachache sana sidhani hata kama 5% inafika.

Wewe naona hatuelewani.
Kitu kinachofanya miungu kuwa tofauti mbali na majina ni sheria, amri, na kanuni zao.
Yehova alijiita Alfa na omega, akijiita Niko ambaye Niko, alijiita majina mengi lakini Sheria zake hazijawahi kubadilika.

Swali unalotakiwa kujiuliza sheria za Yehova na Allah ni zilezile?
Jibu likiwa ndio basi Allah na Yehova ni mungu mmoja katika majina tofauti.
Ikiwa jibu ni hapana basi ni miungu wawili tofauti.

Ndio maana kuna mwenzako mmoja nimemuambia anitajie amri 10 za Allah alizompa Musa pale Mlimani Kwa mujibu wa Quran ili tuanzie hapo kuona Yehova ndiye Allah?

Hata unaweza kutupa hizo Aya ili mjadala uwe Mzuri na watu waelewe
Ikiwa Allah atakuwa ndiye Yehova basi Mimi kama Muumini wa Yehova nitakuwa Muislam tangu leo hii.
Ila ukishindwa na Mimi nikikuonyesha tofauti za msingi za miungu HAO basi watu wataelewa Allah na Yehova ni miungu wawili tofauti wasiojuana wala wasio na mahusiano
 
Waisalamu wanaongoza kufekenyuliwa mtaro,hata zenjibaa karibu kila mwanamke alishaonjwa huko manyu vibibi navyo havina lock Tena, wanatunza ya mbele
Ila chaajabu kiongozi wetu mkuu wakanisa katoliki yuko mbioni kuruhusu ushoga, hiyo inaonyesha wazi kuwa wanao fukuliwa mtaro ni watu wa kanisani, ambao ni wakristo.
 
Ukiangalia Uzi wako harak haraka waeza ona umeandika Kwa Nia Safi na kuappreciate Uislamu lakini ndani yake kuna ukakasi mwingi Sana na ufahamu mbaya juu ya Uislamu

Anyways

Siku hizi sipendi Sana kushiriki mijadala ya mabishano ya Dini unless otherwise ningekuja na kuchallenge hoja zako.

Tatizo la waislam wengi mnapenda sifa tuu pasipokupenda ukosoaji pale yanaonekana madhaifu na mapungufu yenu.

Hapo ndipo mnakwama.
Mimi nimeeleza jinsi nilivyovutiwa na uislam na tamaduni za kiarabu kupitia Kombe la dunia hapo Qatar alafu kuna watu mnaona ninania ovu kisa nimewakosoa kidogo.
Ajabu Sana.

Mbona Wakristo wakikosolewa wao wapo normal.
Ninyi shida yenu inakuwaga wapi?

Au mnaona dini yenu ipo perfect?
Kitu chochote kinachohusiana na binadamu hakiwezi kuwa Perfectly.
Hiyo tosha ingewafanya mtuelewe Sisi wapenda ukweli, haki na wenye upendo bila kuangalia dini za watu zinasemaje
 
Nakupa tofauti moja unidadavulie hapa,
Msikilize Yehova kwenye Torati hapa;

Kutoka 20:8
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

Kutoka 20:9
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;

Kutoka 20:10
lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

Kutoka 20:11
Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Embu tupe Aya kutoka Kwa Allah inayoamrisha watu waabudu na kuitunza Sabato.

Alafu tutakuja kwenye utofauti wa pili
Sabato ilikuwa ni siku ya Ibada kwa Musa na watu wake

Sheria za Ibada huwa zinabadirika na maana Nuhu, Ibrahim na Luti hawakuwa na Sabato wao walikuwa na Ibada zao jinsi ambavyo Mungu aliwaamrisha na hata Yesu aliifanya kazi siku ya Sabato ni kwa sababu Kila mtume anapewa Sheria zake za ibada

Quran 22:67.
Kila umma tumewajaalia na ibada zao wanazo zishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwendea kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye Uwongofu Ulio Nyooka

Ila je Allah alieleza nini ndani ya Quran kuhusu siku ya Sabato

Quran 7:163.
Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu.

164.
Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu.

165.
Basi walipo yasahau waliyo kumbushwa, tuliwaokoa walio kuwa wakikataza maovu, na tukawatesa walio dhulumu kwa adhabu mbaya kwa vile walivyo kuwa wakifanya upotovu.

166.
Walipo jifakharisha katika waliyo kanywa tuliwaambia: Kuweni manyani wa kudharauliwa.

Allah anasema Sabato ilikuwa siku ya Ibada kwa Musa na watu wake na wale walipinga yani kufanya kazi siku ya Sabato badala ya kufanya Ibada aliwadhibu kwa kuwageuza manyani

Hadi hapo tunaona Yehevo ndio huyo huyo Allah

Lete hoja nyingine
 
Tatizo la waislam wengi mnapenda sifa tuu pasipokupenda ukosoaji pale yanaonekana madhaifu na mapungufu yenu.

Hapo ndipo mnakwama.
Mimi nimeeleza jinsi nilivyovutiwa na uislam na tamaduni za kiarabu kupitia Kombe la dunia hapo Qatar alafu kuna watu mnaona ninania ovu kisa nimewakosoa kidogo.
Ajabu Sana.

Mbona Wakristo wakikosolewa wao wapo normal.
Ninyi shida yenu inakuwaga wapi?

Au mnaona dini yenu ipo perfect?
Kitu chochote kinachohusiana na binadamu hakiwezi kuwa Perfectly.
Hiyo tosha ingewafanya mtuelewe Sisi wapenda ukweli, haki na wenye upendo bila kuangalia dini za watu zinasemaje
Ukosoaji unaruhusiwa Sana katika Dini yetu na ndio maana hata Allah alitoa RUHUSA Kwa watu kuikosoa Qur'an,lakini alisema Kama ingeandikwa na binadamu ungeona makosa mengi.

Lakini

Kwakuwa imetoka kwake Katu huwezi ona makosa yoyote Yale,na mpaka Leo hakuna aliye mprove wrong Allah

Sasa nyie mnakuja na hoja za ovyo kabisa halafu mnajifanya mko Sawa then mnategemea tukubali Tu huo upuuzi wenu?

Ndio maana Siku hizi huwa ni msomaji zaidi na pale itakapo bidi ndio nitachangia kwakuwa upuuzi ni mwingi mno.
 
Sabato ilikuwa ni siku ya Ibada kwa Musa na watu wake

Sheria za Ibada huwa zinabadirika na maana Nuhu, Ibrahim na Luti hawakuwa na Sabato wao walikuwa na Ibada zao jinsi ambavyo Mungu aliwaamrisha na hata Yesu aliifanya kazi siku ya Sabato ni kwa sababu Kila mtume anapewa Sheria zake za ibada

Quran 22:67.
Kila umma tumewajaalia na ibada zao wanazo zishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwendea kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye Uwongofu Ulio Nyooka

Ila je Allah alieleza nini ndani ya Quran kuhusu siku ya Sabato

Quran 7:163.
Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu.

164.
Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu.

165.
Basi walipo yasahau waliyo kumbushwa, tuliwaokoa walio kuwa wakikataza maovu, na tukawatesa walio dhulumu kwa adhabu mbaya kwa vile walivyo kuwa wakifanya upotovu.

166.
Walipo jifakharisha katika waliyo kanywa tuliwaambia: Kuweni manyani wa kudharauliwa.

Allah anasema Sabato ilikuwa siku ya Ibada kwa Musa na watu wake na wale walipinga yani kufanya kazi siku ya Sabato badala ya kufanya Ibada aliwadhibu kwa kuwageuza manyani

Hadi hapo tunaona Yehevo ndio huyo huyo Allah

Lete hoja nyingine
Unaposema sabato ilikuwa siku ya Ibada ya Musa ni Kwa maoni yako au kulingana na maandiko ya Quran?

Kwa mujibu wa Quran na Allah, amri za Mungu zinabadilika? Au je Torati inabadilika?

Nasubiri Aya wakati unajibu maswali hayo.
Kisha tunaomba utupe Aya katika Quran zenye amri 10 alizopewa Musa Kule Mlimani.

Unapojibu maswali yangu uwe Mwerevu maana kila ninachokuuliza huko mbele kinaweza kukusumbua kama hauko well informed
 
Ila hawafanyi ushoga kwenye mataifa ya kiislam, na Kama watafanya ni Kwa siri kutokana na sheria Kali za mataifa hayo
Hiyo pekee inaweza Kueleza uislam ni Dini nzuri ambayo kama itaongoza dunia basi dunia itakuwa na maadili na Haki.

IMG_0364.jpg
 
Ukosoaji inaruhusiwa Sana katika Dini yetu na ndio maana hata Allah alitoa RUHUSA Kwa watu kuikosoa Qur'an,lakini alisema Kama ingeandikwa na binadamu ungeona makosa mengi.

Lakini

Kwakuwa imetoka kwake Katu huwezi ona makosa yoyote Yale,na mpaka Leo hakuna aliye mprove wrong Allah

Sisi nyie mnakuja na hoja za ovyo kabisa halafu mnajifanya mko Sawa then mnategemea tukubali Tu huo upuuzi wenu?

Ndio maana Siku hizi huwa ni msomaji zaidi na pale utakapo bidi ndio nitachangia kwakuwa upuuzi ni mwingi mno.

Quran inamakosa mengi Mkuu.
Sema tuu wewe upo ndani hivyo huwezi elewa
 
Mimi na Wewe Nani analazimisha?
Nimekuambia nitajie amri 10 alizopewa Musa na Mungu Kwa mujibu wa Allah(Quran).
Alafu linganisha na Amri 10 alizopewa Musa Kwa mujibu wa Yehova.
Hiyo ni moja ya tofauti Kati ya Allah na Yehova.

Pia angalie Yehova anaabudiwaje tangu zamani mpaka sasa kisha angalia Allah anaabudiwaje tangu zamani mpaka sasa?

Angalia mchakato wa Yehova kutolewa dhabihu na mchakato wa kusamehe dhambi tangu zamani na sasa, kisha muangalie Allah mchakato wake wa kusamehe dhambi tangu zamani na sasa upoje, kisha utaelewa HAO ni miungu tofauti wasio na ukaribu hata kidogo.
Sema kuna mmoja kaiba taarifa za mwingine.

Nitaanzisha Uzi utakaojadili utofauti mkubwa uliopo baina ya Yehova Mungu wa Wayahudi na Allah mungu wa waarabu

Naona tutazunguka hapa hadi Qiyama kifike.

Hivi kiongozi mmoja kulingana na muda na mahali akimuamuru mtu fulani asile mkate halafu kiongozi huyo huyo akatoa amri kwa mtu mwingine kulingana na mazingira ya mahali na wakati ale mkate, je utofauti wa amri hizo unatosha kusema kwamba huyo sio kiongozi yule yule??!!,

Kumbuka Musa (as) alikuwa ni Nabii kwa Bani Israeli hivyo sheria za Taurati zilikuwa sorely for Isralites katika zama hizo hivyo sio necessary kwamba lazima sheria za Musa zilingane kila kitu na sheria za Qur'an , zipo sheria na makatazo yanayofanana katika Qur'an na Taurati, mfano Usizini, Usiibe, uharamu wa nguruwe nk, Sisi Waisilamu kulingana na Qur'an Musa alitumwa na Allah kwa Waisraeli hivyo Wayahudi wanamuita Allah Yehova, tofauti ni jina tu lakini ni Mungu yule yule, tofauti ni Joho tu lakini Padri ni yule yule.🤣

Jenga hoja conceivable kama kweli umeenda shule, mimi sijaenda shule🤣.
 
Sasa hapo ndo unatakiwa ulete hoja yako na kifungu then useme makosa yako wapi

Then hapo

Nitapenda kujadiliana

Uongo wa Quran upo sehemu nyingi mno;

1. Quran inasema, mtoto aliyetakiwa kutolewa kafara na Ibrahim ni Ishamael.
Jambo ambalo sio Kweli, ni uongo wa mchana. Isaka ndiye aliyetaka kutolewa Kafara.

2. Quran inasema, Issa alizaliwa mchana chini ya mtende, na hakusulubiwa.
Jambo ambalo ni Uongo.
Quran haijui hata dhima na mission kubwa aliyoijia Yesu/Issa Duniani ni ipi?

Hii mada inaweza kujitegemea hivyo ingefaa mtu ainzishie Uzi alafu watu tuje tutoe hoja.
Maana hoja zipo nyingi.
 
Naona tutazunguka hapa hadi Qiyama kifike.

Hivi kiongozi mmoja kulingana na muda na mahali akimuamuru mtu fulani asile mkate halafu kiongozi huyo huyo akatoa amri kwa mtu mwingine kulingana na mazingira ya mahali na wakati ale mkate, je utofauti wa amri hizo unatosha kusema kwamba huyo sio kiongozi yule yule??!!,

Kumbuka Musa (as) alikuwa ni Nabii kwa Bani Israeli hivyo sheria za Taurati zilikuwa sorely for Isralites katika zama hizo hivyo sio necessary kwamba lazima sheria za Musa zilingane kila kitu na sheria za Qur'an , zipo sheria na makatazo yanayofanana katika Qur'an na Taurati, mfano Usizini, Usiibe, uharamu wa nguruwe nk, Sisi Waisilamu kulingana na Qur'an Musa alitumwa na Allah kwa Waisraeli hivyo Wayahudi wanamuita Allah Yehova, tofauti ni jina tu lakini ni Mungu yule yule, tofauti ni Joho tu lakini Padri ni yule yule.🤣

Jenga hoja conceivable kama kweli umeenda shule, mimi sijaenda shule🤣.

Nimekuambia, nukuu Aya kutoka kwenye Quran ndio ujadili.
Kama kwenye Quran haipo sema hazipo hizo amri alizopewa Musa.

Unasema usizini, usiibe, sijui nguruwe, hayo umeyatoa wapi?
Nipe andiko kutoka kwenye Quran inayoeleza hizo amri kumi alizopewa Musa.
 
Ndio maana kuna mwenzako mmoja nimemuambia anitajie amri 10 za Allah alizompa Musa pale Mlimani Kwa mujibu wa Quran ili tuanzie hapo kuona Yehova ndiye Allah?
Shida yako kumbe ulitaka zitajwe kwa mlolongo kama kwenye agano la kale ndiyo kuonekane sawa.
Kama unasema utofauti huo kwa maandiko ya vitabu mbona tofauti zitakuwa kwa wote kuanzia Adam na manabii wote. Bila kusahau malaika na shetani kuna utofauti pia.
Hata ukija kwa Luka, Marko, Mathayo na Yohana.
Kuna wengine wameelezea vitu tofauti kiasi cha kwamba tunapata Yesu tofauti.
 
Kwa mujibu wa Uelewa wako, Torati au sheria au amri au sheria za Mungu zinabadilika?

Maana hapo ndio hoja yangu ilipo.
Kama haibadiliki, eleza iweje Torati ambayo Muhammad anaiamini moja ya amri kuu ni kushika Sabato lakini Quran na Allah hajawahi na hatawahi kuwaasa umma wake washike amri hiyo.

Zaidi tunamuona Muhammad na Allah wakiutukuza zaidi utamaduni wa Wakurdi ambao tangu awali ulikuwepo kabla ya Muhammad kuzaliwa, mfano siku ya ijumaa kwenda kuabudu katika Alkaaba, desturi hiyo ikahamishiwa kwenye uislam.
 
Uongo wa Quran upo sehemu nyingi mno;

1. Quran inasema, mtoto aliyetakiwa kutolewa kafara na Ibrahim ni Ishamael.
Jambo ambalo sio Kweli, ni uongo wa mchana. Isaka ndiye aliyetaka kutolewa Kafara.

2. Quran inasema, Issa alizaliwa mchana chini ya mtende, na hakusulubiwa.
Jambo ambalo ni Uongo.
Quran haijui hata dhima na mission kubwa aliyoijia Yesu/Issa Duniani ni ipi?

Hii mada inaweza kujitegemea hivyo ingefaa mtu ainzishie Uzi alafu watu tuje tutoe hoja.
Maana hoja zipo nyingi.
Labda hata kabla ya kwenda mbele zaidi

Huo uongo unaosema je kwakuwa ni tofauti na Biblia au kuna chanzo kingine cha taarifa nje ya Biblia?

Na kama ni kutokana na Biblia je huoni kwamba utakuwa na majibu yako tayar ambayo ni Kwa mujibu wa Imani yako?
 
Iwe Kwa Quran au kitabu chochote, huo ni Uongo.

Tunaweza kuiuliza Quran maswali katika Mada hizo mbili ikabainika kuwa ni Uongo.
Yaani Quran ikakosa majibu yenye mantiki.
 
Unaposema sabato ilikuwa siku ya Ibada ya Musa ni Kwa maoni yako au kulingana na maandiko ya Quran?

Kwa mujibu wa Quran na Allah, amri za Mungu zinabadilika? Au je Torati inabadilika?

Nasubiri Aya wakati unajibu maswali hayo.
Kisha tunaomba utupe Aya katika Quran zenye amri 10 alizopewa Musa Kule Mlimani.

Unapojibu maswali yangu uwe Mwerevu maana kila ninachokuuliza huko mbele kinaweza kukusumbua kama hauko well informed
Mbona umeanza kuruka ruka wewe ulisema Yehova na Allah ni miungu miwili tofauti nikakuambia lete ushahidi ukatoa mandiko yako yanayo elezea siku ya Sabato

Mimi ili kukuonyesha kuwa Yehova ndio Allah Nikakujibu kuhusu hiyo Sabato kama ifuatavyo

Sheria za Ibada huwa zinabadirika na ndio maana Nuhu, Ibrahim na Luti hawakuwa na Sabato wao walikuwa na Ibada zao jinsi ambavyo Mungu aliwaamrisha na hata Yesu aliifanya kazi siku ya Sabato ni kwa sababu Kila mtume anapewa Sheria zake za ibada

Quran 22:67.
Kila umma tumewajaalia na ibada zao wanazo zishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwendea kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye Uwongofu Ulio Nyooka

Ila je Allah alieleza nini ndani ya Quran kuhusu siku ya Sabato

Quran 7:163.
Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu.

164.
Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu.

165.
Basi walipo yasahau waliyo kumbushwa, tuliwaokoa walio kuwa wakikataza maovu, na tukawatesa walio dhulumu kwa adhabu mbaya kwa vile walivyo kuwa wakifanya upotovu.

166.
Walipo jifakharisha katika waliyo kanywa tuliwaambia: Kuweni manyani wa kudharauliwa.

Allah anasema Sabato ilikuwa siku ya Ibada kwa Musa na watu wake na wale walipinga yani kufanya kazi siku ya Sabato badala ya kufanya Ibada aliwadhibu kwa kuwageuza manyani

Hadi hapo tunaona Yehevo ndio huyo huyo Allah

Lete hoja nyingine

Pia sijaelewa kwanini unataka Aya ndani ya Quran inayoelezea amri 10 za Musa?
 
Kwa mujibu wa Uelewa wako, Torati au sheria au amri au sheria za Mungu zinabadilika?

Maana hapo ndio hoja yangu ilipo.
Kama haibadiliki, eleza iweje Torati ambayo Muhammad anaiamini moja ya amri kuu ni kushika Sabato lakini Quran na Allah hajawahi na hatawahi kuwaasa umma wake washike amri hiyo.

Zaidi tunamuona Muhammad na Allah wakiutukuza zaidi utamaduni wa Wakurdi ambao tangu awali ulikuwepo kabla ya Muhammad kuzaliwa, mfano siku ya ijumaa kwenda kuabudu katika Alkaaba, desturi hiyo ikahamishiwa kwenye uislam.
Naona kuna vitu unaongea kwa kuropoka. Hiyo ijumaa kwenda kuabudu alkaaba umeitoa wapi?
Kuna baadhi ya sheria zilikuwa zinawahusu baadhi ya 'Jews'.
Hilo suala la sabato kwenye Qur'an limezungumziwa pia.
Kuna baadhi ya maagizo mengine kwenye agano la kale yametiwa chumvi kupewa maagizo Musa kama kuua watoto wa changa na kuwabakisha hai wasichana walio bikra.
Jitahidi usome biblia kuanzia mwanzo hadi mwisho kuliko kusoma kwa kudokoa hadi uhadithiwe na mtu.
Qur'an soma kama story sio lazima uiamini. Hakikisha unaelewa kwanza dhumuni la sura na ilishuka wakati gani. Anza na sura fupi kwanza.
 
Back
Top Bottom