PONGEZI; QATAR IMEUPA HESHIMA UISLAM NA UTAMADUNI WA KIARABU
Anaandika, Robert Heriel
Shahidi.
Historia Jana imeandikwa. Tukio la kihistoria katika ukanda wa mashariki ya Kati sio tu limeipa heshima Nchi ya Qatar bali limeupa uislam utukufu na heshima kubwa Duniani. Waislam na jamii zote za kiarabu siku ya Jana wameionyesha dunia kuwa inawezekana dunia ya maadili na ustaraabu/uungwana Kwa kuunganisha tamaduni nzuri zenye manufaa zinazolinda utu wa binadamu.
Uislam hauna mvuto katika mawaidha au mahubiri katika majukwaa ya kutangazia dini au katika propaganda. Lakini Jambo la hakika ambalo uislam unaweza kujivunia na ambalo ndio mvuto wa uislam ni Desturi, sheria na matendo yao.
Qatar wameonyesha mfano Bora Wakuigwa sio tuu na Waislam wengine ulimwenguni bali pia hata na siye tusio Waislam.
Michezo ya mwezi mmoja haiwezi kubadilisha na kuvunja sheria na utamaduni wetu, hivyo ndivyo Qatar walivyofanya.
Ingawaje wapo wenye chuki na Waislam kwa kuwashutumu mambo mabaya kama ugaidi, roho mbaya, ukatili n.k. Lakini hayo mambo hatuyaoni katika ulimwengu halisi wa Kiislam.
Uislam umejengwa katika kufuata Muongozo Mkuu ambao ni Quran, ingawaje niliandika kuwa Quran ilikopi na kuiba maandiko ya kiyahudi Jambo ambalo ni kweli kabisa lakini ninachowasifu Waislam ni uwezo na msimamo wao wa kufuata yale yaliyoandikwa humo kwenye kitabu Chao bila kujali yaliibiwa au hayakuibiwa.
Na wanaweza kutuambia Sisi Wakristo au Mayahudi kuwa ni kweli Sisi Waislam tuliwaibia maandiko yenu kwa sehemu, lakini tunayafuata Kwa 100% hayo maandiko, vipi nyie (Mayahudi na Wakristo) ambao ndio wamiliki halali wa hayo maandiko mnafuata yaliyoandikwa humo yaani kwenye Torati, Zaburi na Injili?
Swali hilo ndilo Waislam wangeweza kujivunia nalo. Ni Sawa na Wazungu au wachina kuiba Teknolojia ya mataifa mengine na kuibadilisha kidogo sio kosa, huo ni ujanja, na Akili. Hivyo ndivyo waislam walivyofanya Kwa upande wa Dini.
Niwapongeze Qatar na Waislam wote Duniani Kwa kuonyesha msimamo thabiti. Na hicho ndicho kinahubiri na kuwasilimisha watu zaidi kuliko kupigapiga kelele kwenye maredio au Television kama Sisi Wakristo.
Matendo ni muhimu zaidi kuliko kelele kelele.
Kataa ushoga hadharani hasa viongozi wa kitaifa.
Kataa mapombe kunywewa hadharani,
Kataa watu kukaa nusu uchi au kutokuvaa Kwa adabu.
Na Sheria Kali zimewekwa.
Wakristo na mataifa mengine tunayomengi ya kujifunza kutoka kwa Waislam. Hata kama tunawaona kama Watoto wa Kambo, au watoto wa hawara lakini wanamazuri yao mengi tu.
Kuhusu tabia mbaya za mtu binafsi ambazo zinachafua Uislam hiyo ni kawaida kuwepo lakini haimaanishi Uislam ni mbaya au dini mbaya.
Hata Shetani alitoka mbinguni kwa Mungu Baba, hivyo haimaanishi mbinguni kuna wadhambi. Isipokuwa zinatokea Error.
Hongereni Sana Watoto wa Mama Mdogo, hongereni Waislam.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam