Binti ninayemtongoza anataka nimuazime Tsh. 100,000/-

Binti ninayemtongoza anataka nimuazime Tsh. 100,000/-

Wakuu habari za muda huu,

Nisiwachoshe na mambo mengi ngoja nije moja kwa moja kwenye mada. Wiki iliyopita katika harakati zangu za kutafuta nilikutana na binti mrembo kiasi.

Kama mjuavyo hulka ya mwanaume anapokutana na pisi lazima utesti mambo. Kwangu pia ilikua hivi toka siku nilipokutana na huyo mrembo niakaaza kumtongoza kwa sababu tayari nilishachukua namba yake licha ya yeye kuto toa jibu la kunikubalia.

Leo kanitumia meseji ya kuniomba shilingi 100,000 kwa masharti ya kumuazima na atarudisha baadae ya wiki 2 Mara baada ya kupokea mshahara kwa kuwa ni mfanyakazi.

Binafsi sijamjibu na sijajua mpaka sasa namjibu nini, nimeamua kuandika hapa ili kuomba ushauri kwamba pisi unayoitokea inapokuomba uiazime pesa itaweza kurejesha kweli? Lakini pia kama ikitokea nikamwazima hiyo pesa ataweka uzito wa kuirejesha kweli?
Ukituma tu umepigwaaaaaa na uterezi hupatiiii
 
Aisee usije thubutu kumpa hio hela uyo dem hakutaki anataka tu mpunga wako na unaweza shangaa hata mzigo asikupe na asikulipe
 
Kama unayo mpe tu mkuu,huyo amekubali lakini anataka kupima urefu wa pumzi yako. Ila hiyo haitorudi hata so usije sema hatukukwambia, na Kama huna mpotezee tu
 
We mpe tu. Sijuhi huyo mimi sikuwah kurudishiwaga. Sasa hivi demu akija na gia ya mkopo, kama ninayo Nampa tu. Akirudisha sawa asiporudisha sawa
 
Wanawake wa siku hizi wanna akili saana kuliko wa zamani

Zamani binti kama hakutaki alikuwa hataki hata kukutana na wewe
Hawa awamu hii wakakaa kikao wakajadili kwamba kumwambia mtu mzima mwenzio kwamba sikutaki siyo ustarabu

Wengi wao wakaona iwe fursa yaani ukiona mtu hujamwelewa lakini yeye kang'ang'ana wewe shusha nyavu zako vua kadri ya uwezo wako
Vijana wengi mmejikuta mko njia panda kwa kukosa maarifa

"MWANAMKE MWENYE NIA NZURI HAKUOMBI HELA"
Labda awe amebanwa kwelikweli

100000 kwa hapa uswahilini kwetu ni kodi ya miezi 5
Point hii
 
Tafuta hela laki sio pesa ya kuja kuandika paragraph jf[emoji28]ukiombwa million si ndo utaenda mahakamani
 
Ushachukua namba halafu unatongoza tena hii formula ya wapi,
Na kwa nn ulimwambia kwamba unafanya kazi ya kulipwa mwisho wa mwezi badala ya kumwambia ww ni mjasiria mali matatizo mengine mnayataka wenyewe.
 
Back
Top Bottom