Binti usitoe utamu (K) mpaka mwanaume amewekeza kikubwa kwako... Girl Code 2

Binti usitoe utamu (K) mpaka mwanaume amewekeza kikubwa kwako... Girl Code 2

sasa wanawake maskini ulitaka wakaolewe na nani?
wewe au?
Watafute cha kufanya, ndoa sio kazi wala biashara..

Unakuta binti kamaliza chuo fresh Ila hataki kazi wala biashara, 24/7 anajipost mtandaoni kimitego na kwenda sehemu classic kuwinda wazungu. Hii ni aibu

Wafundisheni wadogo zenu kuwa financially independent maana bila hivyo wataburuzwa na kunyanyaswa
 
Kutumia mwili wa mwanamke, hasa sehemu za siri, kama kitega uchumi cha kupata fedha na mali kutoka kwa wanaume badala ya kujali heshima, utu, na hadhi kunaathiri vibaya afya ya akili, mwili, na jamii kwa ujumla. Hali hii inamfanya mwanamke kuishi maisha yasiyo na utulivu wa kisaikolojia, kwani anakuwa katika hali ya wasiwasi na msongo wa mawazo kutokana na utegemezi wake kwa mahusiano ya kimwili. Kukosa uhusiano wa kihisia na wa dhati kunasababisha upweke na hisia za kutengwa. Mwanamke pia anaweza kujidharau na kuona hana thamani ya kiutu zaidi ya mwili wake, jambo linaloshusha kiwango chake cha kujiamini na kumfanya kuwa na hatari ya kuathiriwa na sonona na huzuni ya muda mrefu.

Kwa upande wa afya ya mwili, mwanamke anayejihusisha na tabia hii yuko kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya zinaa kama UKIMWI, kaswende, kisonono, na maambukizi mengine. Hali hii huzidishwa zaidi na mahusiano yasiyo na mipango salama, yanayopelekea mimba zisizotarajiwa ambazo zinaweza kuhatarisha afya ya mama na mtoto. Aidha, matumizi ya mwili kupita kiasi husababisha uchovu wa mwili na matatizo ya mifumo ya uzazi, huku akihatarisha kupata saratani ya shingo ya kizazi kutokana na maambukizi sugu. Vilevile, mwanamke huyu anaweza kukumbana na unyanyasaji wa kimwili kutoka kwa wanaume ambao hawamheshimu, wakiona mwili wake kama bidhaa ya biashara badala ya utu wa mtu.

Kijamii, tabia ya kutumia mwili kama chanzo cha kipato huathiri hadhi na heshima ya mwanamke katika jamii. Jamii kwa kawaida humhukumu na kumpunguzia nafasi ya kuaminiwa au kushirikishwa katika masuala muhimu ya kijamii. Aidha, tabia hii huathiri uwezo wa mwanamke kuanzisha ndoa na familia imara inayojengwa kwenye upendo na maadili mema. Mwanamke aliyezoea kutegemea mahusiano ya kimwili mara nyingi hukosa msingi wa kujenga familia yenye mshikamano. Hali hii pia inasababisha kuvunjika kwa maadili ya kijamii, kwani vijana na kizazi kijacho wanaweza kuiga tabia hiyo na kuendeleza mzunguko wa maisha usiofaa.
Umemaliza mkuu!Kule kwetu kulikuwa na chama Cha ushirika kiliitwa KYERUCU(Kyela_Rungwe cooperative).Basi mwanamke mgawa mnyandua aliitwa hivyo ,kijiweni!
 
Watafute cha kufanya, ndoa sio kazi wala biashara..

Unakuta binti kamaliza chuo fresh Ila hataki kazi wala biashara, 24/7 anajipost mtandaoni kimitego na kwenda sehemu classic kuwinda wazungu. Hii ni aibu

Wafundisheni wadogo zenu kuwa financially independent maana bila hivyo wataburuzwa na kunyanyaswa
Kabisa mkuu mimi pia nina binti yangu , kama baba sitatamani awe namna hii ndio maana napambana sana angalau aje asimamie miradi ya baba yake, binti yangu mpka sasa hawezi kuja kuwa na mtazamo kama huu hata nikifa leo.
 
Attachments

  • IMG_3675.jpeg
    IMG_3675.jpeg
    30.9 KB · Views: 1
Kabisa mkuu mimi pia nina binti yangu , kama baba sitatamani awe namna hii ndio maana napambana sana angalau aje asimamie miradi ya baba yake, binti yangu mpka sasa hawezi kuja kuwa na mtazamo kama huu hata nikifa leo.
Ni kumuombea Mungu tu aweze kuivuka mob psychology. Kuna mabinti wanadanga na kuwinda lakini kwao hakuna shida ya pesa Ila tu ni kufuata mkumbo wa kampani.

Ila kama umemtengeneza vizuri kujitegemea na kujitambua. Sio rahisi kuingia kwenye mitego kirahisi
 
Back
Top Bottom