Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Na tena anavyoendelea kuuza ndio anazidi kujitengenezea jina na kufanya awe na wateja wengi, yaani baada ya miezi mitatu utakuta anacheza na wateja 80+, kizembe zembe anaweza akatoka sawa na mbunge

Sent using unknown device
Au wakati anafanya hivyo na bado nachukua oda ya kupika hata kwenye kipaimara na shughuli ndogo ndogo kujenga jina na watu wanavyooa kila wiki baadae weekend anatoa huduma kwenye harusi maana nilivyomsikia biashara yake nadhani siku za kazi ndio inanoga zaidi hivyo ili aweze ku-shine wiki nzima inabidi na weekend akomae kwenye sherehe
 
Nigeria kua na degree ni kama kua na cheti cha lasaba

Ni nchi ambazo elimu imekuja saa moja jioni ndio tunajithaminisha kwa kutumia elimu na vidato ila nchi nyingine hiyo ni kawaida sana, hivi ulishawahi kusikia mzungu anaitwa kwa elimu yake mfano Dr Williams, professor Mcdonald? Ni Africa tu elimu inakubatiza upya.
Huku kiukweli elimu tunaitumia kuwananga watu na sio kuingiza pesa, ila ninachofurahi madogo wa siku hizi wanajitahidi kujichanganya pamoja na kwamba wachagua kazi wapo wengi (mie nimeshuhudia mtu ana degree yake lakini amekwenda kujifunza cherehani alafu anakula vichwa tu)
 
Mkuu Freelancer unakosea!

Hapa wadau hatutaelewa popoma ni nani kati ya wanaomsifia au wanaomkosoa,wewe unaona yupo sahihi kwa elimu yake hiyo kufanya biashala ya chakula?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Na hili ndio tatizo kubwa la graduates wa kibongo na hasa kutoka vijijini au maeneo ambayo watu wanaenda secondary kwa mchango wa kijiji na walioenda secondary wanahesabika

Jifunze kitu kinaitwa humble beginning, mtu ana ndoto zake na safari ndefu huanzia na hatua moja, njoo baada ya miaka 5 uone kama utamkuta hapo.

Nyie mnataka mkimaliza chuo ukutane na barua ya wito kazini mshahara million 5 take home, gari v8, nyumba ya muajiri, allowances na padiem holela, ofisi ghorofa ya 25 posta, mtakaa sana
 
Ukitaka watu wakupigie makofi basi wape wazo lako la kuendelea kuwa ndani ya Confort zone hapo utashangiliwa sana.

Dada wa MWANZA angekuja na Idea ya Kufungua Duka kali la Urembo angeshangiliwa sana, Duka la Nguoa watu wangeshangilia mno, Salooni kari ya kike watu wangeshangilia sana, Baa tungeshangilia sana.

Tungeshangilia kwa sababu ni vitu vya Confort zone zetu.


Ukitaka ukamwe basi waso lako la nje kabisa ya Confort zone wapelekee watu wa ndani ya Confort zone. Hahaaa hapo unakamwa milele

DADA MWENYE BIASHARA YA KANDE MWANZA nazani aliomba ushauri kutoka kwa watu wa walio kwisha toka kabisa nje ya Confort zone zao. la sivyo asingefanya ile biashara. yaani angeomba ushauri kutoka kwa watu kama sisi tungeishia kumwambia anajiabisha.


Nisha wahi kuleta Habari ya Dasa muuza Uji anaye soma Chuo watu waliponda sana wanaponda kwa sababu dada katoka nje ya Confort zone na si vinginevyo.


Wanao pondea Dada wa Mwanza ni kwa sababu yule Dada katoka nje ya Confort zone walizo zizoea wao. sasa hii ni tatizo kwetu watu wa Confort zone.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro umeeleweka ila unakitu kitu flani ambacho unaweza kuelezea vijana ukawaokoa, hebu elezea kidogo namna ya kutoka katika comfort zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NGOJA NAMI NICHANGIE KIDOGO...
Tusipende sana wasomi kufanya mambo tofauti na carrier zao...
AFRIKA NI MASIKINI KWA SABABU WASOMI WENGI HAWAFANYI VILE WALIVYOSOMEA.. UNAKUTA KASOMEA IT LKN ANAUZA NGUO...
TUKUBALI KUWA TUMEPOTEA....
KAMA ALISOMEA UJASIRIAMALI BASI AMEPATIA SANA NA ANAFANYA KILE AMBACHO ANAPASWA KUFANYA ILA KAMA KASOMEA TOFAUTI NA HAPO YUKO WRONG NA HII NI KWA SABABU YA UMASIKINI WETU.
WASOMI WETU WAANGALIWE VIZURI NA KAMA NCHI LAZIMA TUWE NA SERA MADHUBUTI ZA KUWAWEZESHA HAWA WASOMI... TUSICHEKELEE UPUUZI HUU.. MTU KATUMIA GHARAMA KUBWA AFU ETI UNAMSIFIA KUUZA KANDE?? SI BORA ANGEANZA KUUZA TANGIA ZAMANI?? HAKUNA MWENYE KUSOMA AKAWAZA HAYO MAMBO.. ALWAYS HUTOKEA MARA BAADA YA KUSHINDWA KWA SERA ZETU ZA KUIINUA WASOMI WETU...
NCHI YA HOVYO SANA HII.. NA NI AIBU KWA TAIFA KWA WATU KUFANYA VITU AMBAVYO HAWANA UTAALAMU NAVYO..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa watakwambia umechanganyikiwa! Mtu anasoma masters mpaka PhD anavuka na border, anarudi Tanzania kuuza makande. Pathetic.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angekuwa katokea familia masikini na kuonyesha jinsi alivyofight mpaka kuanzisha hiyo biashara ningemuona wa maana sana. Kumbe mtoto wenyewe wa kishuwa aaaargh hana hoja huyo wala hana motisha kwa watoto wa kimasikini.
 
Hapa watakwambia umechanganyikiwa! Mtu anasoma masters mpaka PhD anavuka na border, anarudi Tanzania kuuza makande. Pathetic.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha ukweli mchungu nchi haina dira ndio maana masters ya agro economy ni wakala wa M MPESA...
FOR SURE TUNA MAWAZO YA KIPUUZI KUTOKANA NA UMASIKINI WETU NA SERA MBOVU ZINAZOTUNGWA NA WASIO WASOMI LKN WAKUZITUMIA WAWE WASOMI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
images


Hiyo ndio Mcdonald ya kwanza 1948
Hakuna kitu hapo,yaani nitoke America na master yangu nije na cheap idea kama hiii.Halafu unakuja kumsifia hapa?Hatua aliyofikia alitakiwa aje na project kubwa zakusaidia Taifa sio vijiajira uchwara hivi.Hakuna kitu hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umepitia stori ya huyo binti!??
Kwanza hauzi makande peke yake, anauza vyakula aina nyingi sana, kila siku menu inabadilika na kande zikiwepo.
Kande zimepata headline watu hawazungumzii vingine anavyouza.
Alianza na mtaji mkubwa tu ambao mtu wa kawaida/maskini kuupata ni mbinde
makande yanahitaji mtaji kiasi gani?wabongo kwa visingizio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom