Binti wa miaka 17 ajinyonga baada ya kuachika mara tatu kwenye ndoa

Miaka 17 ndoa 3? Huyu kuna roho mbaya ilikuwa inamuwinda kupitia mapenzi na imefanikiwa.
 
Uko sahihi kabisa Dada
Nashkuru nimepata mzazi (baba tofauti kidogo)ananiambiaga hivi ndoa ni mapenzj na huruma kama hakuna usiruhusu kunyanyasika sikukusomesha uwe mjinga na kukubali kua mtumwa be responsible woman but not stupid!
 
Wasukuma wanaolewa na miaka 12 mbona
 
Kuna mama kaolewa mara 5 zote kaachika sasa anataka ndoa ya sita sasa mtu mara zote hizo si bora utulie ufanye mambo yako, kuna watu hawawezi kabisa kuishi wenyewe inasikitisha
 
please say u r joking
Wala sitanii ni ukweli kabisa! Nina uzoefu nishafundisha usukumani kule mtoto wa kike akiwa mweupe kusoma atakusikia kwenye bomba tu, nishawahi ishi na watoto wawili wa kike Shinyanga hukoo walitelekezwa na wazazi wao kwa kuwa wamefaulu std 7 na waliambiwa wasifaulu std 7 wakafaulu hivyo wazazi wakasusa kusomesha maana walikuwa washakula mahari za ng'ombe tayari..nawakumbuka mpk majina!

Kinachosaidia sasa hivi ni hii kuwa mtoto akifaulu lazima aende shule la sivyo mzazi unashtakiwa ila mwanzo hali ilikua mbaya mnooo!!
 
Miaka 17 ameolewa mara tatu huku akiachika mara tatu, tuseme alianza kuolewa na miaka mingapi,

Sema kijijini inaleta maswali huku mjini ni sawa tu
 
Wasukuma wanaolewa wakiwa na miaka 12 wengine hata period inakuwa bado, anapata akiwa ndoani.
 
Sasa katika tukio hili jamii imehusikaje?! Yaani mtu awe depressed kwasababu zake binafsi lawama tupewe wanajamii?!

Hebu mtupumzishe muda mwingine wanajamii tunalaumiwa hata na vitu visivyotuhusu. Miaka kumi na saba sio umri wa kulaumiwa kwa kukosa ndoa baada ya kutalikiwa.
 
Bila shaka umeamka na marue rue ukakimbilia kujibu bila kutafakari.

Mnaambiwa muamke kwanza japo mpige mswaki akili zikae sawa mnabana pua, bando letu wenyewe.
 
Ukoa sahihi kabisa DadaNashkuru nimepata mzazi (baba tofauti kidogo)ananiambiaga hivi ndoa ni mapenzj na huruma kama hakuna usiruhusu kunyanyasika sikukusomesha uwe mjinga na kukubali kua mtumwa be responsible woman but not stupid!
Usione anakusaidia hapo anakuandaa kuwa kiburi kwenye ndoa mwisho wake utaishia kuwa single mama, ndoa ni utumwa huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…