BM Coach kuanza safari saa 10 alfajiri

BM Coach kuanza safari saa 10 alfajiri

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Majuzi kati hapo wasimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini Latra walitoa taarifa za kuruhusu mabasi kusafiri kuanzia saa 9 usiku👇🏾.

Hadi kufika leo naona kampuni moja ya kuelekea Arusha ambayo ni BM Coach imetoa tangazo 👇🏾.


20230531_133026.jpg

 
Majuzi kati hapo wasimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini Latra walitoa taarifa za kuruhusu mabasi kusafiri kuanzia saa 9 usiku[emoji1484].

Hadi kufika leo naona kampuni moja ya kuelekea Arusha ambayo ni BM Coach imetoa tangazo [emoji1484].

View attachment 2641312
Kama gari zinazuiwa saa sita usiku, na kuruhusiwa saa kumi alfajiri,

Tofauti yake ni masaa manne, kutoka saa sita mpaka saa kumi,

Swali langu ni, je mamlaka zindhani haya masaa manne ndio muda wa ajali na majambazi, ndio maana wanazuia kusafiri masaa 24?
 
Hata basi za kichina zinaweza kwenda na kurudi.
Sawa kabisa ila wataalam wa hizo gari wanasema ili hudumu na hiyo gari kwa muda fulani inapaswa isiwe na route ndefu au league kama zile anavofanya Ally's na yule katarama au Golden Deere na Sauli.

Kwa kifupi angalia huyo Ally's na Golden kila baada ya miezi fulani wanaangiza gari mpya hadi Ally's kachoka kupuliza rangi ya body za gari zake.
 
... Swali langu ni, je mamlaka zindhani haya masaa manne ndio muda wa ajali na majambazi, ndio maana wanazuia kusafiri masaa 24?
Sidhani kama lengo la masaa hayo ni ajali na ujambazi, bali nahisi ni kuwapumzisha kwa lazima madereva kwa masaa hayo.

Mfano, unatoka Musoma au Bukoba kuja Dar ukifika pale njia panda ya kilosa mnasimamishwa, kwa mtizamo wako unadhani eneo lile kuja Morogoro mjini kuna hatari yoyote?.

Jibu ni NO.
 
Unakuwa usafiri kama wa ndege sasa mtu hulali inabidi kuanzia saa 6 usiku uanze kujiandaa iwapo una watoto ndio kabisa!
Uwaogeshe, uwavalishe, upike uji wao, uwalishe, ipaki chakula chao, ujiandae mwenyewe halafu saa 9 na nusu iwe stand Upande basi la kuondoka saa 10 alfajiri?!

Sema kupanga ni kuchagua.

Watapanda wale ambao ni convenient kwao.
 
Back
Top Bottom