BM Coach kuanza safari saa 10 alfajiri

BM Coach kuanza safari saa 10 alfajiri

Unakuwa usafiri kama wa ndege sasa mtu hulali inabidi kuanzia saa 6 usiku uanze kujiandaa iwapo una watoto ndio kabisa!
Uwaogeshe, uwavalishe, upike uji wao, uwalishe, ipaki chakula chao, ujiandae mwenyewe halafu saa 9 na nusu iwe stand Upande basi la kuondoka saa 10 alfajiri?!

Sema kupanga ni kuchagua.

Watapanda wale ambao ni convenient kwao.
NAKAZIA.
 
Niliona na ABC za kwenda Njombe zina ruti ya saa 04:00. Hii itaturahisishia watu wa kuunga magari kufika kwenye destination siku hiyo hiyo.
Sio mtu unataka kuunganisha magari, unafika unaambiwa gari zilishaondoka zote na inabidi ulale tu kuongeza gharama.
 
Happy national kutoka Dar - mwanza na bukoba.
Ally's dar - mwanza
Katarama dar - mwanza

Zote hizo ratiba take kutoka ni SAA. 3:00 Am alfajiri
Na kanda ya kaskazini ni nani na nani?
 
Acha maneno mengi wewe, Katarama na Scania zake kule kanda ya Ziwa anakalishwa na Mchina vizuri tu tena Golden Dragon, Higer na Asia Star

Piga picha angekuwa anashindana na Zhong Tong au Yutong

Ally's ana hela na ana routes nyingi huwezi kumfananisha na huyo Katarama hivyo kuingiza basi mpya kawaida

Si mlikuwa mnatamba Mchina majiko hayachelewi kuungua, mnakalishwa sasa hivi mmeanza maneno tulieni dawa iwaingie

Halafu wanazi tulishakubaliana ukipigwa gap kausha mwaga moto
View attachment 2642009
Hizi ndizo ligi wanazoziweza wabongo wengi. Ubishi usiokuwa na msingi wowote. Nilidhani mambo ya kusifia ni gari gani inakimbia zaidi yalishaisha ile miaka 1970 kumbe bado yapo?
 
Safi hii kitu imeniokolea nauli za ndege ,mwendo wa saa kumi alfajiri na saa saba mchana dar -arusha ,ila dar-mza hakuna namna.
 
4am siyo saa 4, tafuta std 7 akufundishe hayo masaa.
20211018_105849.jpg

Std 7 anamsubiri huyo mtu wa kumfundisha 🤣
 
Huku tuachieni tujimwaemwae na wale hamsha popo pale Lake Oil Urafiki, mkuu.
Baada ya serikali kutoa mkono wa night shift, hao jamaa zako waanze kutafuta njia nyingine.

Kampuni zimesha anza kuomba route ya hamsha popo mojawapo ni Kilimanjaro.
 
Baada ya serikali kutoa mkono wa night shift, hao jamaa zako waanze kutafuta njia nyingine.

Kampuni zimesha anza kuomba route ya hamsha popo mojawapo ni Kilimanjaro.
Hamsha popo watakachofanya ni kushusha nauli tuu...so kama kawa yaani....saa moja asubuhi upo mndenyi unagonga supu.
 
Hamsha popo watakachofanya ni kushusha nauli tuu...so kama kawa yaani....saa moja asubuhi upo mndenyi unagonga supu.
Wakishusha nauli hata mimi nitasafiri nao.
 
Back
Top Bottom