Bodi ya Ligi: Kama Yanga wameenda CAS ni kichekesho, busara itumike sio kanuni

Nakala ni tangazo la Bodi kuwa match kupangiwa tarehe nyingine,una jingune
 
Simba walikoseaje?
Simba walikoseaje?
Simba walifahamu hii game hawataki kucheza Sababu key player ni majeruhi kina chemalone,camara ..... Kwahio wakatumia Sababu dhaifu kuwa wamezuiliwa kufika uwanjani (Siku zote MDA WA dabi hizi Timu zinajifichaga au niseme hawana utaratibu WA kwenda uwanjani Siku moja kabla ya game) na hata kama wangeenda utaratibu ni kuwa unatoa taarifa kwa mwenyeji kuwa nakuja uwanjani na yeye ataandaa mazingira yote vizuri special for you (Simba hapa hakufanya haya yote maana hata report ya kuahirisha mech ya TFF Ilisema hivo)

•Pia Kosa la kikanuni linaadhibiwa kikanuni kwamba umezuiliwa kufanya mazoezi basi Yanga anaadhabiwa na TFF ,Hauwezi kugomea mech kizembe hivo Kwani mara ngapi Simba na Yanga wanafanyiwa fujo uarabuni na mech zinacheza ,ila waarabu wanapigwa faini
 
Hakuna kanuni inayosema utoe taarifa kwa mwenyeji punguza uroporopo

Hiyo ya kusema kwamba hawakutaka kwa sababu ya key player pia ni uongo na kupiga ramli
 
Nilikuwa naiheshimu yanga kama mojawapo ya team kubwa lkn kwa yanayoendelea saiv naweza kusema yanga ina viongozi wa hovyo sana
Yani wanahangaika harafu ukifikilia kinachowatesa sana yanga ni ukubwa WA Simba hakuna kingine maana kwa afrika Simba ni team yenye status kubwa kuliko yanga
Na mi namini kabisa huu mgogoro ungetokea baina ya yanga na azamu au yanga na kmc Jamba lingemalizika kirahisi sana ila kwakuwa ni Simba ndiomana mambo yanakuwa mengi
Ila mwisho wa siku yanga ataishia kupata aibu hata akienda huko CAS coz hawana hoja za msingi uongozi unaendeshwa kwa hisia na sio uhalisia wa mambo
Kamdomo ndio usiseme mala leo utasikia Haji kasema lile mala kesho anaibuka kiongozi mwingine nae anaongea lile mwisho wa siku kupitia hayo maneno inajikuta imevunja kanuni
 
Msimu unaofuata itabidi tuwe na ligi mbili ligi itakayoongozwa na kanuni pia kuwepo ligi itakayoongozwa na busara
 
Muda ule Simba wamezuiliwa na mlinzi au na wahuni, hapakuwa na lines of communication kati ya SIMBA, BODI, TFF, Bosi wa mlinzi wa uwanja, WIZARA, YANGA, OCD na RPC ???????

Ulaya hilo jambo lisingetokea kwa saab wakuu wa vyombo kama hivyo wanapatikana muda wowote kufanya maamuzi ya kimamlaka kwa dharura muda wowote haswa kuelekea maandaliI ya tukio kubwa kuliko yote kwenye ligi.

Huku kwetu bendera ikishashuka na mamlaka zinaenda kulala na familia zao. Kwa wenzetu bendera haishuki jioni, himaya inasimama masaa 24.

Na Kagame anajua, akitaka urahisi aje jioni.
 
Hakuna kanuni inayosema utoe taarifa kwa mwenyeji punguza uroporopo

Hiyo ya kusema kwamba hawakutaka kwa sababu ya key player pia ni uongo na kupiga ramli
Hakuna kanuni eeh ,.... Kanuni inasema tatizo likitokea kwa mgeni WA mchezo ikiwemo kukosa Hali nzuri ya kimchezo mwenyeji WA mchezo Ndio anaadhabiwa huonagi kwa waarabu
 
Busara na hekima!?, kanuni waliweka za nini hawa wapuuzi, kwa timu nyingine kanuni zifuatwe lakini kwa simba ni busara?
Yanga lazima mtumie busara. CAS huko kutaenda kubumbuluka mambo hatere. Haitakua derby ya Machi 8 tu. Kutazuka penalti na red cards za mchongo, magoli ya offside wanayonufaika nayo timu moja pekee.
Ukizingatia tuna CHANI NA AFUKONI, msitake kututilia mchanga kitumbua chetu.
 
Leo crown kuna kiongozi wa TFF amekanusha kuwa hawajapokea barua yeyote ya Yanga na wala wao hawajajibu chochote.

Lakini kuna muda tena akasema wao kila siku wanafanya mawasiliano na vilabu kwa njia ya barua.

Kiukweli wanachanganya sana.
Wamechanganyikiwa kumbe kuna timu inatakiwa ishushwe daraja
 
Usiamini kila unachoona na kusikia. Huku mitaani na mitandaoni tunaparurana kumbe walioliseti hili jambo wamekaa wametulia tuli.
 
Kwani si mlitoka hadharani mkanadi adui wenu namba 1 ni YANGA anafuatiwa ni SINGIDA BIG STAR?
Haya sasa UBAYA UBWELA UBAYA UBWEGE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…