Wakati wa ukombozi ni sasa.
Mbinu chafu zilizotumiwa na makaburu zilifika mahali zikagota.
Mtatutesa, mtatufunga, mtatutoa kucha na meno, mtatoboa watu macho, mtatuua.
Lakini neno la Mungu litasimama upande wa haki.
Ole wenu magamba, saa yaja, tena iko karibu sana.
Ukweli wote utadhihirika.
Poleni sana wana Arusha.
Poleni sana makamanda.
Poleni sana wote mlioguswa, mliojeruhiwa na mliopoteza ndugu kwenye tukio hili.
Damu yao haitamwagika bure.
Huu tuliofikia sasa ndiyo ule uchungu wa mwisho, mama anakaribia kupata mtoto.
Ninaamini sasa Ukombozi wa wanyonge umefika!
Mungu Awalaze mahali pema wote waliopoteza maisha!