Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Nilikuwa nakaribia kuanza kuandika polisi wakaanza kutupiga mabomu ya machozi. Ikabidi tukimbie.
Yaani mkuu sehemu imelipuka bomu na polisi nao wanakuja kupiga mabomu ya machozi?Hii kali ya mwaka, sasa hayo mabomu ya machozi yanasaidia vipi kwenye kuokoa maisha ya walioathirika na hilo bomu amabalo limelipua watu?Kweli shetani ana njia tofauti za kufanya kazi.
 
duuu!huo udiwan tu bado uraisi....afu wanadai chadema ni magaidi asa nan gaidi kat yao na chadema!
 
Too bad!
Nchi inaingia katika Historia ya aina yake katika nyanja ya siasa.

sijui kwanini ccm hawafanyi siasa za kistaarabu huu ni upuuzi kutega bomu ili ionekane chadema wanalipuwa mabomu...mbona haiuziki sababu wananchi wanaenda kusympathy na chadema kwamba wanaonewa ......wale watu wenye hoja ccm wameishia wapi mpaka tunawekeana mabomu kama mbadala wa sera za kumkomboa mwananchi.
 
ccm hawawezi kutega hayo mabomu ,ili waachive nini?tena siku ya mwisho wa kampeni...mbona unakua na haraka kulaumu kabla,au unahusika mkuu?

CCM wameshajua kuwa Arusha wanaambulia patupu hii ni mbinu ya mwisho ya kutisha wapiga wasijitokeze kesho ila ku chance kuiba kura!!
 
Tunaomba jeshi la polisi liachwe lifanye kazi yake pia polisi wawe fair wasiegemee upande wowote hii ni hatari sana..!
 
Kwa akili ya haraka ni

kuvuruga uchaguzi
pili ni uhasama wa vyama
tatu hapo ni kutafuta sababu ya kutoelewana kati ya wananchi
hii ni hali ya watu kuwa na njaaa nalitamka hili kwa mara ya pili tena njaa nchi hii itatuua na chanzo ni kutokuwepo na msimamo wa utawala wa nchi hii kila mtu ni anasauti
 
Ni mapema mno kuanza kulaumu mtu!

Cha maana kwa sasa ni kusaidia kurescue situation.

Mtu aliyerusha bomu hilo nia yake ni moja tu, kwamba anataka watu waogope mikusanyiko, aidha wasiende kwenye upigaji kura kesho kutokana na hofu iliyojengwa... je ni kwa faida ya nani?
 
Majeruhi wanapelekwa hospitali muda huu.Watu wengi wamezirai.Mlipuko ulitokea mbele karibu na eneo walilokua wamekaa viongozi akiwepo mwenyekiti wa Taifa Kamanda Freeman Mbowe na ulitokea baada ya Mkutano kufungwa na hakukua na vurugu zozote.
 
Watu 7 wamejeruhiwa vibaya na kitu kinachoaminika kua ni bomu katika mkutano wa CHADEMA jijini Arusha katika viwanja vya Soweto.

Source ITV.

Mwenye data zaidi mwaga hapa.

Wishing quick recovery kwa waathirika wote
 
Too bad!
Nchi inaingia katika Historia ya aina yake katika nyanja ya siasa.

Mwigulu umri mdogo lakini ananuka damu,wanachadema mjue mwigulu si binadamu wa kawaida,kunathread ilikuja hapa ikielezea CHADEMA KUWA MAKINI KWA MIPANGO INAYOSUKWA NA MWIGULU,JK MWIGULU ATAKUSABABISHIA MAKUBWA,KAA CHONJO.
 
MH!! hata sielewi Polisi wanarusha mabomu kwa sababu ipi? je hayo mabomu mnayosema yamejruhi watu ndio yamerushwa na polisi? hebu tuliaeni mtupatie taarifa sahihi!!
 
Hii ni zaidi ya vyama, siamini kama kuna siasa hapa..kwa bahati mbaya sana hatuna wapelelezi wazuri
 
Ni mapema mno kuanza kulaumu mtu!

Cha maana kwa sasa ni kusaidia kurescue situation.

Mtu aliyerusha bomu hilo nia yake ni moja tu, kwamba anataka watu waogope mikusanyiko, aidha wasiende kwenye upigaji kura kesho kutokana na hofu iliyojengwa... je ni kwa faida ya nani?
kuna watu wameshindwa, sasa wameamua kuvuruga uchaguzi ili usifanyike

mbinu waliyotumia ya kumwaga damu si sahihi kabisa

ila naamini kabisa kwamba watapatikana tu
 
Back
Top Bottom