Bondia Hassan Mwakinyo afungiwa kujihusisha na mchezo wa ngumi mwaka mmoja

Bondia Hassan Mwakinyo afungiwa kujihusisha na mchezo wa ngumi mwaka mmoja

Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) imemfungia Bondia Hassan Mwakinyo kujihusisha na mchezo wa ngumi nje na ndani ya Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni 1

Hatua hiyo imekuja kutokana na kugomea pambano lake lililokuwa lifanyike septemba 29.2023, Dar es Salaam dhidi ya mpinzani wake Julius Indongo kutoka nchini Namibia,

Siku moja kabla ya maamuzi hayo kutolewa, kupitia mitandao binafsi ya kijamii ya Hassan Mwakinyo aliandika maneno yafuatayo:

"Nilielewa mapema sana huu mchezo mchafu, nia ovu pamoja na dhamira zenu na hatma iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa, nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi wazi hadharani kwenye hili, ili inapotokea tena ishu kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu, ni kweli pesa inaweza nunua haki na utu wa mtu lakini hio ni kwa mtu 'boya' asiyejuwa thamani na haki zake za msingi..., see you soon..."
Mwakinyo ni bondia mtata sana.
 
Mwakinyo ni mshenzi sana anatafta mabondia mwenyewe then anaweka cha juu hataki bondia wa kupangiwa anataka anae muweza mbaya zaidi anataka apange yeye watakao pigana supporting fights na promotion company apange yeye ngumi gani hizo?
Hiyo tena wapi?
 
huyuu mwakinyo si walishamfungia uingereza tena.
...Hivi anajua Ngumu kweli ? SI Huyu Huyu alifika Uingereza Kwa ajili ya Pambano.na akadai kuwa begi lake lenye Viatu vyake vyw kupigania lilipotea Airport ikabidi aazime vingine vilivyokwa vikitereza ???
Jamaa anapigana Sana Nje ya Ringo kuliko Ndani ya ringi !! [emoji57][emoji57][emoji57]
 
Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) imemfungia Bondia Hassan Mwakinyo kujihusisha na mchezo wa ngumi nje na ndani ya Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni 1

Hatua hiyo imekuja kutokana na kugomea pambano lake lililokuwa lifanyike septemba 29.2023, Dar es Salaam dhidi ya mpinzani wake Julius Indongo kutoka nchini Namibia,

Siku moja kabla ya maamuzi hayo kutolewa, kupitia mitandao binafsi ya kijamii ya Hassan Mwakinyo aliandika maneno yafuatayo:

"Nilielewa mapema sana huu mchezo mchafu, nia ovu pamoja na dhamira zenu na hatma iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa, nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi wazi hadharani kwenye hili, ili inapotokea tena ishu kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu, ni kweli pesa inaweza nunua haki na utu wa mtu lakini hio ni kwa mtu 'boya' asiyejuwa thamani na haki zake za msingi..., see you soon..."
bondia hassan mwakinyo hakua ma mkataba wala hakusaini mkataba wa kupigana na Julius Indongo,adhabu hii ipo totally biased.
 
Ukitaka uonekane m'baya hapa Tanzagiza jifanye unazijua haki zako. Ndio maana Mimi nasema hivi hii nchi sio sehemu salama kuishi watu wanao jielewa🤣🤣🤣🤣 ukishaonyesha unajielewa TU Kuna mawili wakuue au wakufunge 😭😭😭
 
Busara na circular education ni muhimu sana, HUYU Jamaa hana busara kabisa
Mimi nadhani yeye ametambua vizuri haki zake kuliko wenye hayo ma phd ya kupeana kwenye hiyo sekula education,
Busara pia anayo ndio akatahadharisha kabla ya pambano

Jamaa yuko vizuri kuliko,
Labda kama unachomekea udini
 
Hata kama mtu una talent adabu na exposure ya sheria na taratibu zinazosimamia unachofanya ni muhimu.Haka kajamaa kanavimba sana kichwa sidhani kana washauri au kanazingatia ushauri.
Acheni kumlaumu,
Vaeni viatu vyake na ngumi za uso ndio mtajua kwanini maslahi ya kutosha ni muhimu,
Hachezi mpira huyu, huyu anpigana ngumi mjueeeee
 
Back
Top Bottom