Bongo aliyenunua gari na kujenga nyumba anajiona ametoboa maisha

Bongo aliyenunua gari na kujenga nyumba anajiona ametoboa maisha

Nadhani Pitia maana ya Maneno Maisha; Kujipata, Umasikini na ukishatumbua kwamba watu wapo tofauti ndio utagundua kwamba kuna masikini mwingi kingi na tajiri mwenye vichache..., Na ukishatambua hivyo utaona kwamba mtu aliyeridhika sio limbukeni bali yule asiyeridhika ndio limbukeni....

To each their Own...
Ulimbukeni tu
 
Kujenga na kumiliki usafiri ni sehemu ya success Kwa Tanzania

Maana hali ya Umasikini ni kubwa miongoni mwetu.

Baadhi ya Wazee wetu, hadi wametangulia mbele za haki hawakufanikiwa kununua hata Kiwanja cha 20x30

Kwanini usitembee kifua mbele Kwa kufanikisha hilo??
Kununua Gari MTU unaayetegemea mshahara pekee ni kupunguza umaskini au kuongeza umaskini mkuu
 
Mafanikio ni swala pana. So inategemea hali uliokua nayo awali na ulipo kwa wakati husika.
Kwa mfano unaweza kuta mtu kwao kakulia kwenye nyumba ya udongo na shule amesomea 2km umbali kutoka nyumbani na anaenda kwa miguu kila siku, sasa mtu kama huyo akijenga nyumba ya milion 30 na kagar ni mafaniko makubwa sana kwake ila kwa mtoto wa mengi au bakhresa kwao mafanikio ni vitu tofauti na hivyo.
Yaani watu tunadhani maisha ni kama ni uniform wote tuwe sawa kitu ambacho sio sahihi.
Kwanza fikira tunazo tofauti kwenye mambo mbalimbali, mfano mafanikio ni kama ulivyo eleza hapo juu.
Kuna mtu anaweza akasoma akipata PhD akahesabu mafanikio lkn kuna mwingine akilima ekari 60 za mahindi au mpunga ni mafanikio na kuna mwingine atafanya biashara akafikisha mtaji wa 100M atasema mafanikio, na kuna mwingine akioa au kuolewa atasema kafanikiwa.
Kwahiyo mafanikio ni kufikiwa kwa malengo ya mtu aliyo kuwa amejiwekea.
Pia tujifunze kuheshimu mawazo ya watu wengine, hii dunia hatuwezi kuwa na mutazamo na uwezo sawa
 
Huku Bongo (TZ) ukijenga nyumba ya 30mil kisha ukinunua gari la kutembelea (i.e: Carina, IST, Mazda, wish, Rav4, Dualis, Spacio, Crown Athlete, Vitz, Runnex, n.k) tayari unaonekana umetoboa maisha. Pengine hata wewe mwenyewe utajiona una akili ya maisha kuliko kiumbe chochote hapa nchini ambacho hakikufanya hivyo.

Ukisimama mbele ya masikini wenzako wanakuita TAJIRI. Hata kama haikuwa desturi yako kuvaa mkanda nje (kuchomekea sharti), sasa utaanza kuvaa hivyo ili watu waone ufunguo wa gari ukiwa umeuning'iniza kwenye suruali.

Right Marker
Dar es salaam​
Wanasahau kwamba maisha ni zaidi ya hizo basic needs and life keeps on rolling .

Hujamaliza kuishi Hadi utakavyojufa,so acheni ujinga,ulimbukeni na unyumbu.
 
Kwa hiyo hata unachofanya hujui mkuu ?
1. Kuna wakati Mtanzania ni sawa na mbuzi wa kuchinja

2. Hayo maswali ukaulize wanao kuhusu nini nafanya na nini nawaza kufanya haikuhusu...niwe sina maono au niyo hayakuhusu na hayakusaidii wewe na ndg zako.

3. Kila mtu ana maono yake.

Labda nikufungue macho kidogo.

Tanzania ni nchi isiyo na sera na maono ya Taifa zinazoeleka na yaliyopo hayafanyiwi kazi kwani kila rais huja na utopolo wake...yapo kwenye makaratasi lkn utekelezaji ni zero.

Ushahidi ni huu;
1. Kulikuwa na matajiri uongozi wa Mwinyi lkn alipoingia BM, JK, JPM na sasa Samia kila mmoja huja na kuibua waliofanikiwa kibiashara katika uongozi wake huku wale wa awali hupotea..

Maana yake ni nini?
2. Nchi hii biashara haitabiriki hutevemea nani yupo juu.

Nataka kusema nini?
A) Hskikishs una nyumba na ardhi kwanza, tena ardhi ya maana na ukiweza iwe maeneo au mkoa wenye thamani nzuri ya ardhi eg. Arusha, Dar na Mwanza ( mikoa hii ni muhimu na nimeitaja kwa mpangilio)
2. Uwe sasa na biashara yako eidha bidhaa, huduma au kilimo na ufugaji.
3. Gari ifuate...kama moja ya nyenzo ya kuboost biashara eidha kwa usafirishaji au usafiri.

Kununua gari bila malengo ni kujiletea ufukura totoro.

Sijui niongezd nini
 
Huku Bongo (TZ) ukijenga nyumba ya 30mil kisha ukinunua gari la kutembelea (i.e: Carina, IST, Mazda, wish, Rav4, Dualis, Spacio, Crown Athlete, Vitz, Runnex, n.k) tayari unaonekana umetoboa maisha. Pengine hata wewe mwenyewe utajiona una akili ya maisha kuliko kiumbe chochote hapa nchini ambacho hakikufanya hivyo.

Ukisimama mbele ya masikini wenzako wanakuita TAJIRI. Hata kama haikuwa desturi yako kuvaa mkanda nje (kuchomekea sharti), sasa utaanza kuvaa hivyo ili watu waone ufunguo wa gari ukiwa umeuning'iniza kwenye suruali.

Right Marker
Dar es salaam​
Kutoboa kimaisha ni utamaduni. Sasa kama wewe huna hivyo vitu utaitwaje?
 
Kwamba wasio na magari wanakosa mahitaji muhimu sio

Kwa kutegemea mshahara pekee
Gari inaongezea kipato au unatumia na kipato ulichanacho ?
Kila mtu anapata mahitaji yake kulingana na kipato chake. Kwangu mimi gari sio luxury, maisha yangu ili yaende nahitaji kuwa na gari nyumbani😀
 
Huku Bongo (TZ) ukijenga nyumba ya 30mil kisha ukinunua gari la kutembelea (i.e: Carina, IST, Mazda, wish, Rav4, Dualis, Spacio, Crown Athlete, Vitz, Runnex, n.k) tayari unaonekana umetoboa maisha. Pengine hata wewe mwenyewe utajiona una akili ya maisha kuliko kiumbe chochote hapa nchini ambacho hakikufanya hivyo.

Ukisimama mbele ya masikini wenzako wanakuita TAJIRI. Hata kama haikuwa desturi yako kuvaa mkanda nje (kuchomekea sharti), sasa utaanza kuvaa hivyo ili watu waone ufunguo wa gari ukiwa umeuning'iniza kwenye suruali.

Right Marker
Dar es salaam​
Watanzania wengi hawana elimu ya fedha mimi kila siku nawapiga spana inakuwaje mtu unanua gari tena kwa hela ya mkopo halafu unaenda ku pack ofisini kuanzia asubuh mpaka jioni haliingizi hata cent halafu akitoka kazini anapitia kwenye biashara yake ya juice yenye mtaji wa laki moja na matunda kuna madogo wamekuja juzi hapa wameshachukua mkopo wa gari cha ajabu wanapiga mizinga balaa mara nikopeshe elfu kumi mimi gari labda nikistaafu nakuwa kama CEO wa NALA anatumia bajaji.
 
Wengi wanapiga hatua kuzidi uwezo unajua ukipiga hatua kubwa kuzidi uwezo unachana msamba au haujui? sasa ndio yanayowakuta wengine, kuna mtu analazimisha kuonekana na watu kwamba na yeye hajaachwa nyuma sasa hapo ndipo maamivu yanapokuja ukitaka kuwaonyesha watu kwamba na mimi sipo nyuma nimenunua gari zaidi ya milioni 10 nimejenga nyumba milioni 100 kasoro sasa jiulize huyo mtu je ni mtu mwenye hadhi ya kushika hio milioni 100 kwa mkupuo ameshinda bingo? Hakuna basi jua behind kuna maumivu makali mno mno mno ambayo wewe hauyajui usione anatabasamu akiingia chumbani hujui mlio anaolia
Kwa kila aliyefanikiwa nyuma yake kuna story chungu ila aina ya story ndiyo zinatofautiana tu.
 
Nafikiri umeelewa ndo maana umepaniki
Labda nikuongezea swali lingine

Hiyo Ist uliyonunua million 10 unafikiri baada ya miatano utaweza kuiuza hiyo Bei ?
Na unafikiri itakuwa imepanda thamani au imeshuka thamani ?

Kama imeshuka thamani , unafikiri umejiongezea utajiri au umaskini ?
Si kila unachonunua na investment mengine unayanunua kukurahisishia maisha. mfano wewe hapo una smartphone, ukitaka kuiuza sasa utaiuza kwa faida au hasara? Je, kwa fikra hiyo hukupaswa kununua smartphone? Bila shaka hapana uliinunua ikirahisishie mawasiliano.
Gari ni usafiri ni basic need. Sometimes unaenda kusecure deal mwenye deal anaanza kukuvalue kutokana na mwonekano wako wa mara ya kwanza. Nina experience na kitu hiki wakati miaka hiyo na deal na masuala ya aluminum na pvc. mtu unaenda chukua deal kwa boss, anataka pvc madirisha, gharama milioni 14, anakutazama hivi huyu kaja na bodaboda nikimpa milioni 14 si ataingia mitini kweli.
Pia gari kwa sababu ya umasikini wetu bado tunachukulia kama ni kitu cha starehe. Hizi ist ni usafiri tu magari ambayo ni kwa starehe ni hayo ma G wagon.
 
Back
Top Bottom