Bongo fleva top 5 yangu ya muda wote

Bongo fleva top 5 yangu ya muda wote

Naijua ila ni nzuri huko kwa Mario, huyo Paulo kafunikwa vibaya, halafu hiyo kucheza na cucumber mara kula wali imeipunguzia ladha umekaa kitoto toto kisicho na adabu
Hahhahahaha mimi ni mzee ila kwenye ngoma sijui kwanini sizeeki😛😛
 
Kuna wimbo wa Bob Ludala unaitwa Julie kimsingi unanikumbusha CBE sehemu niliyopata heartbreak ya kwanza kwa mtoto wa kichaga
 
Baadhi ya nyimbo zinakuwa zina capture moments...yaani nyakati Fulani hivi ...na mood ya Taifa au ya walio Wengi wakati huo...

1. Nipe Tano - Daz nundaz..
Huu Wimbo unawakilisha nyakati ..kama birth hivi ...ndo kwanza Taifa linapata TV special Kwa bongo flava na vijana ...Nani angejua channel 5 ingekuwa chanzo cha TV zote zilizozagaa now?golden era..

2. Dushelele - Ally Kiba
Wengine wanamuona Ally Kiba kama the best ever bongo fleva singer ...huu Wimbo Una kitu unique sana...mashairi ambayo hayana lugha za vijana au matusi ..umeandikwa vizuri umeimbwa vizuri...kinacho ufanya uwe special ni kudhani kuwa kungekuwa na nyimbo kama hii nyingi ..but cha kushangaza ni kama imeshindikana kabisa kupata uandishi kama huu na Wimbo kama huu...umebaki Tu wa aina yake..

3. Mfalme -Mwana Fa
Wimbo unahusu Mungu kwenye bongo fleva na ndani ambae baadae anakuja kuwa waziri wa sanaa... something unique...

4. Muziki-Darasa..
Wakati ilionekana kama ngumu kutamba kwenye mziki bila kupitia wasafi au kupata sapoti ya Diamond...jamaa aliibuka na kutawala vibaya mno na Wimbo ambao unaitwa "mziki"...hakuna aliedhania wala kutegemea....

5.Single Again - Sikuwahi kupenda nyimbo yeyote ya Harmonise wala kumtegemea atakuja kutoa Wimbo utatamba Hadi nje ya Tz ..ila huu Wimbo alionesha ana kipaji.. na inawezekana kufika juu Sana ukiamua...

Wengine mnaweza taja za kwenu na sababu
List nzuri kama ulivyosema ya kukumbuka moments ila kwa mimi nyimbo zote zitaimbwa ila mtazamo itabaki kuwa nyimbo bora ya bongo fleva upande wa hip hop.

Na wakali kwanza natamani utabaki kuwa wimbo bora wa RnB wa muda wote.

Chochote popote huu kwangu utabaki kuwa wimbo bora wa hip hop unaozubgumzia mapenzi (Joh makini aliuwa sana humo ndani).

Collaboration yangu bora ya bongo fleva naitupa kwenye dhahabu, ebhana e Dully, Blue na Joselin waliua sana mule ndani.

Prof na series yake ya ndio mzee ni moja ya ngoma zenye ubunifu na idea ya kipekee ambayo ilifanywa kuwa nyepesi na ya kuvutia sana na mwanalizombe.
 
Kabisa , ila ngoma nyingi za sasa hivi haswa za bongo zipo hivyo ,ila za mbele zinaishi hata miaka 100
Hata za mbele ladha inaenda inapungua, kizazi cha 70-90 katikati tumefurahia sana ujana wetu kwa midundo ya maana iliyoacha historia, nyimbo za kina Celine Mariah care, Whitney nk, mpk watoto wa afu 2 bado wanajiliwaza nazo
 
List nzuri kama ulivyosema ya kukumbuka moments ila kwa mimi nyimbo zote zitaimbwa ila mtazamo itabaki kuwa nyimbo bora ya bongo fleva upande wa hip hop.

Na wakali kwanza natamani utabaki kuwa wimbo bora wa RnB wa muda wote.

Chochote popote huu kwangu utabaki kuwa wimbo bora wa hip hop unaozubgumzia mapenzi (Joh makini aliuwa sana humo ndani).

Collaboration yangu bora ya bongo fleva naitupa kwenye dhahabu, ebhana e Dully, Blue na Joselin waliua sana mule ndani.

Prof na series yake ya ndio mzee ni moja ya ngoma zenye ubunifu na idea ya kipekee ambayo ilifanywa kuwa nyepesi na ya kuvutia sana na mwanalizombe.
Kuhusu wakali kwanza Kuna Ngoma ya makamua na enika Rudi nyumbani, Joseline na ticha, niite bas, umewezaje ukija kwa Q jay Sifai.

Hii inatoa tafsiri kwamba wakali kwanza kweli walikuwa wakali
 
Hata za mbele ladha inaenda inapungua, kizazi cha 70-90 katikati tumefurahia sana ujana wetu kwa midundo ya maana iliyoacha historia, nyimbo za kina Celine Mariah care, Whitney nk, mpk watoto wa afu 2 bado wanajiliwaza nazo
Celine Dion - new day as come
Shwania twain - Forever and always

Hizi nyimbo nilikuwa na headphones 🎧 utamu wake ilikuwa ni sayari nyingine
 
Back
Top Bottom