Bongo hakuna wenye sifa ya Uhadhiri? Re-Advertisments zimekuwa nyingi

Bongo hakuna wenye sifa ya Uhadhiri? Re-Advertisments zimekuwa nyingi

Sio ukubwa wa qualifications tu. Kazi ni highly demanding, time consuming, energy consuming abd relatively poor rewarding. Unaenda kufundisha chuo na MaGPA yako makubwa, uwe unabukua na kuandaa masomo kila wakati lkn mwishowe malipo ni kiduchu ukilinganisha na wenzako waliopambana au watakaopambana kuingia kwingine ndani ya serikali. Na Masters yako, unakuja vijana wa Bachelor wanakuzunguka mara kibao. Wana safari za kilakukicha wakato weww unakomaa kuandaa slides kozi kama 3 hivi au hata kupitia za wenzako. Mara usahibishe mitihani ya wanafunzi wengi. Pointi yangu ni kwamba package za wahadhiri zipitiwe na kuboreshwa. Hata kwa kuhamia hakuna mtu atataka kwemda. Maisha ya wahadhiri nayo yawe bora kama huko TCRA, TRA, BOT, PSSF, NSSF, NHIF na kwingine.
Hamna Serikali hapa Duniani inaweza ikawalipa watu wote mishahara mikubwa,utasababisha matatizo katika uchumi wa Nchi.

Hizo taasisi ulizozitaja ndio zipo miongoni mwa taasisi 200 za Serikali zinazolipa vizuri but napo mishahara yao sio mikubwa kama watu wanavyoaminishwa.

Hata mishahara ya hao ma lectures in mikubwa tena sana uki compare na walimu wengine.
 
Hello members,

Nimestushwa sana na hii trend ya kutafuta wahadhiri kwa kurudia rudia matangazo kila siku.

Nilikua na mzee mwenzangu leo akanionesha tangazo la kazi za wanataaluma kutoka UDSM zaidi ya wanataaluma 300 huko lakini chakushangaza tangazo linarudiwa!!

Shida ni nini na wasomi wa masters sasa ni wengi mno tofauti na miaka yetu?

Shida ni umahiri? Uzoefu? Ufaulu au nini?

Nini kifanyike kurejebisha hili maana hii imenistua sana.
Tatizo ni Kiinglishi 😀
 
Mtoa mada,kuna matatizo yaliibuka mwaka au miaka 2 iliyopita katika kutafuta Walimu wa kufundisha vyuoni-Kati ya Serikali na Uongozi wa vyuo katika kuwapata walimu.
hali hiyo ndio imepelekea chanzo cha hayo yote.
Nitaelezea vizuri nikipata muda.
 
Sio mbaya. Kinachowatofautisha wao na waalimu wa A-level ni hiyo GPA tu. Mshahara hautoshi kila sehemu. Watumie vizuri faida ya kukopesheka kufanya mambo mengine. Kinyume na hapo watazidi kulaumu tu. Hata hawa wabunge wangekuwa wanapata mishahara tu bado sio nyingi kivile kwa sababu ya wahitaji wengi walio nao. Wahadhiri wajiongeze kwasababu pia wana faida kubwa ya vyuo vingi kuwa mijini.
Kwanza katika watu wanalipwa vizuri na hao,Walimu wa vyuo hawana kazi ngumu kama wale wa O-level,primary na advance.
 
Mtoa mada,kuna matatizo yaliibuka mwaka au miaka 2 iliyopita katika kutafuta Walimu wa kufundisha vyuoni-Kati ya Serikali na Uongozi wa vyuo katika kuwapata walimu.
hali hiyo ndio imepelekea chanzo cha hayo yote.
Nitaelezea vizuri nikipata muda.
Mkuu njoo uelezee aisee sababu huwa najiuliza kwanini TAs wengi hawaajiliwi wakati ni msingi Wa kuwa na wabobezi wengi,ni aibu unakuta kuna vyuo maprof wanafundisha certificate students.
 
Hello members,

Nimestushwa sana na hii trend ya kutafuta wahadhiri kwa kurudia rudia matangazo kila siku.

Nilikua na mzee mwenzangu leo akanionesha tangazo la kazi za wanataaluma kutoka UDSM zaidi ya wanataaluma 300 huko lakini chakushangaza tangazo linarudiwa!!

Shida ni nini na wasomi wa masters sasa ni wengi mno tofauti na miaka yetu?

Shida ni umahiri? Uzoefu? Ufaulu au nini?

Nini kifanyike kurejebisha hili maana hii imenistua sana.
UFAULU

Elimu ya chuo kikuu Ili upate upper second au first class....
Ina bidi sacrifice sana...kujitoa sana na Mwenyezi MUNGU awe upande WAKO daily.....

Na huo msako wa first class na upper second unatakiwa uuanze tangu First semester ya mwaka wa kwanza.....

Mm nilikuja kupata awereness mwaka wa kwanza semester ya pili....mtanange ukawa mgumu pambania sana KOMBE...

Nika fall in love na masomo nikawa BOOK MONGERS...

Yaan NDIO Nika ishia 3.5 nakumbuka Kuna watu wakinionaga nao wanapata mshituko am 4 real am 4 real Duniani 🌍 hakunaga mtu mwembamba😎
am 4 real hatukuwai kujua utakuja kunenepa....

Hapa sijazungumzia Favoritism huko masomo vyuoni....
All in all Kupata first class au upper second class need dedication....

Hata Kwenye course za social science sio lelemama usipo kua makini unaishia pass na lower second class
 
Si ndio maana hawaombi.
Hozo fani ukiangalia ni kali sana mitaani wachache sana huenda kusoma.masters

Sababu first degree tu.huwa zinawawezasha kuajiriwa au kujiajiri

Wakishaingia soko la ajira wengi huwa hawana mpango wa kurudi kusoma Masters

Chuo waombe kibali waajiri toka nje ya nchi nchi za Sadc watawapata
 
Hello members,

Nimestushwa sana na hii trend ya kutafuta wahadhiri kwa kurudia rudia matangazo kila siku.

Nilikua na mzee mwenzangu leo akanionesha tangazo la kazi za wanataaluma kutoka UDSM zaidi ya wanataaluma 300 huko lakini chakushangaza tangazo linarudiwa!!

Shida ni nini na wasomi wa masters sasa ni wengi mno tofauti na miaka yetu?

Shida ni umahiri? Uzoefu? Ufaulu au nini?

Nini kifanyike kurejebisha hili maana hii imenistua sana.
walikuwa too ambitious kuset GPA! GPA ya 3.8 undergraduate ni kubwa sana na haina msingi wowote. Gpa ya undergraduate ingetakiwa iwe upper second ambayo inaanzia 3.5 - 3.99 na kwa upande wa masters ndiyo iwe 3.8 and above. kisha wafanye udahili mwingine kuhakikisha mhusika anaweza kudeliver kulingana na GPA yake. Too much is harmful sasa tunajenga mazingira ya kutafuta wahadhiri wa nje angali vijana wetu hawana ajira
 
Kuna shida kuamini kuwa GPA ndio kila kitu na kwa mujibu wao hicho ndicho kigezo cha Msingi

Mambo yanabadilika sana humu duniani lakini wanaojiita wana taaluma wana-assume dunia ipo static

Mathalani, ukitaka undergraduate 3.5 gpa na masters 3.8gpa maana yake average ni 3.6125gpa kimahesabu umeongea hivyo.

Sasa unawaachaje waliopata undergraduate (3.3 &4.0, 3.4&3.9)respgpa,'s au wote wenye average hiyo hiyo?

Kwanza kufundisha wala sio GPA kubwa, kufundisha ni Exposure, Experience and Education ipo mwisho.

Tafuta waseminishaji wa kitaa au wawezeshaji kutoka NGO's au Mashirika mbalimbali mstari unachorwa hapo sio kuwa addicted na gpa

Watu wanaomba kazi wako tayari wana sifa tena wengine wapo na uzoefu wa field hizo hizo we unabaki kukomaa na gpa haya kula gpa zako
Kwa mantiki hiyo unataka kusema mwenye GPA za gentleman aje awafundishe watu Chuo kweli haki kweli.

Wako sahihi kabisa first uwe na GPA kubwa then tuoneshe uwezo wa kufanya presentation na ukaeleweka
 
walikuwa too ambitious kuset GPA! GPA ya 3.8 undergraduate ni kubwa sana na haina msingi wowote. Gpa ya undergraduate ingetakiwa iwe upper second ambayo inaanzia 3.5 - 3.99 na kwa upande wa masters ndiyo iwe 3.8 and above. kisha wafanye udahili mwingine kuhakikisha mhusika anaweza kudeliver kulingana na GPA yake. Too much is harmful sasa tunajenga mazingira ya kutafuta wahadhiri wa nje angali vijana wetu hawana ajira
Sure. Walegeze kidogo hadi 3.5. Usikute kuna wa 3.5, 3.6, 3.7 wanatamani kuomba.
 
Wengi tumesoma hapo mlimani. Na unakuta wenye hizo GPA kwa darasa hawazidi 5 hasa kwa natural science, technology and engineering.
Sasa hao ndio vyuo vigawane na soko lingine la ajira private and public. Na mtu mwenye uwezo akishazama private au central gvt, kutoka inakuwa ngumu sana.
 
Naweza kukuelewa sasa, nini kifanyike?
GPA ya 3.8 undergraduate haina uhalisia. kigezo kiwe uppersecond class kuanzia 3.5 na kwa masters iwe kuanzia 3.8. SUA zamani walikuwa na vigezo hivi ila harmonized scheme imepandisha. na wahadhiri wa SUA waliokuwa wanapatikana walikuwa wazuri tu kupitiliza! makerere gpa wanaanzia 3.5 kwa first degree na masters
 
Back
Top Bottom