Bongo hakuna wenye sifa ya Uhadhiri? Re-Advertisments zimekuwa nyingi

Bongo hakuna wenye sifa ya Uhadhiri? Re-Advertisments zimekuwa nyingi

Hello members,

Nimestushwa sana na hii trend ya kutafuta wahadhiri kwa kurudia rudia matangazo kila siku.

Nilikua na mzee mwenzangu leo akanionesha tangazo la kazi za wanataaluma kutoka UDSM zaidi ya wanataaluma 300 huko lakini chakushangaza tangazo linarudiwa!!

Shida ni nini na wasomi wa masters sasa ni wengi mno tofauti na miaka yetu?

Shida ni umahiri? Uzoefu? Ufaulu au nini?

Nini kifanyike kurejebisha hili maana hii imenistua sana.
GPA ya 3.8 si kigezo tena. Serikali kupitia kwa Waziri wa Elimu Prof. Mkenda ashakataza watu kuchujwa kwa kigezo cha GPA badala yake washindane kwenye interview. Naona UDSM wamefanya hivo kwenye hizi kazi.
 
Unajidanganya! Hakufuta kigezo cha GPA alisema GPA peke yake isiwe kigezo vinginevyo tangazo lisingerudiwa!!
 
Wakitaka washushe shushe hadi 3.0 kwa shahada za awali watu wazigombanie kama repoti ya CAG. Vinginevyo sioni tatizo hili la kukosa wahadhiri likiisha hivi karibuni.
Kwanza huku mtaani elimu inakosa mashiko sana kwa wengi ambao wanawaona watu wenye elimu na hawana kazi au wanafanya kazi ambazo si za kitaaluma waliyosomea. Hii trend inavyokwenda wengi baada ya miaka kadhaa hawatatamani kwenda advance. Kusoma kwa ajili ya knowledge generation ila kwa capital material generation.

Naamini serikali itafanya kitu ka mdau mmoja alivyoshauri kuwe na "Attractive Package" huwezi kumfunza mtu chuoni, kesho anakuwa waziri anapokea 12 m ya ubunge na posho lukuki za uwaziri halafu uendelee kuwa na moyo. Unakuta mfanyakazi wa TPA anamzidi mbali senior lecturer halafu wakikutana ktk vikao vya bodi huyo lecturer anaidhinisha matumizi na mishahara hata ungekuwa wewe ungefanya hivyo hivyo tuuu...
 
Halafu kuna kitu kingine hakijatajwa humu...hamna usawa wa ufundishaji na assessment.
Unakuta kozi moja inatumia different assessment tools kutoka chuo kimoja na kingine...huyu yuko chuo A anabanwa mbavu na anapitishwa ktk moto kweli kweli matokeo yake nakuwa competent lakini GPA ndogo huyu wa chuo B habanwi ana GPA kubwa lakini hakidhi competency ktk kila eneo la kile alichobobeaa. Kesho unatumia kigezo sawa Cha GPA kwa watu wawili kutoka ktk mifumo miwili tofauti. This is insane.
 
Yes na ukilinganisha na mwalimu aliyepo sekondari afadhali mara 100 maana kama mtu unavuja jasho hivyo aisee ni hatari!

Nasikia PhD anakula 3.4M gross!!
Advantage moja ya uhadhiri ni kuwa, Kwa mtu anayetaka kujiendeleza kielemu ni rahisi na mapema sana anafanikiwa..

Kwenye hilo tangazo ukiangalia chini ya Duties and Responsibilities, mojawapo inasema:-
"To undergo postgraduate training for the Master’s degree/PhD.."
 
Wenye masters wengi GPA za under graduate hazifiki 3.8

Na pia ambao zinafika hawako vizuri kwenye presentations. Hivyo wanafeli interviews
Watu wengi wanakariri na kusaidiwa na google, ukiwapa wajieleze au waelezee jambo fulani kwa uelewa wao wanaeleza notisi
 
Mathalani, ukitaka undergraduate 3.5 gpa na masters 3.8gpa maana yake average ni 3.6125gpa kimahesabu umeongea hivyo.

Sasa unawaachaje waliopata undergraduate (3.3 &4.0, 3.4&3.9)respgpa,'s au wote wenye average hiyo hiyo?

Kwanza kufundisha wala sio GPA kubwa, kufundisha ni Exposure, Experience and Education ipo mwisho.

Tafuta waseminishaji wa kitaa au wawezeshaji kutoka NGO's au Mashirika mbalimbali mstari unachorwa hapo sio kuwa addicted na gpa

Watu wanaomba kazi wako tayari wana sifa tena wengine wapo na uzoefu wa field hizo hizo we unabaki kukomaa na gpa haya kula gpa zako
Duh!
Kuna vyuo vikuu duniani ukitaka kusoma tu unapitia mchujo mkali utafikiri unaenda kuajiriwa kabisa, halafu una suggest kupunguza standards Kwa wahadhiri wa vyuo?!!!

Ukitaka standards za chini siyo kesi, unaenda tu CBE, IFM, IAA, nk
 
Admission za vyuo vya Ivy league kama havard.

Lazima ufanyiwe interview ueleze kwa nini upewa nafasi ya kusoma chuo chao
 
Halafu kuna kitu kingine hakijatajwa humu...hamna usawa wa ufundishaji na assessment.
Unakuta kozi moja inatumia different assessment tools kutoka chuo kimoja na kingine...huyu yuko chuo A anabanwa mbavu na anapitishwa ktk moto kweli kweli matokeo yake nakuwa competent lakini GPA ndogo huyu wa chuo B habanwi ana GPA kubwa lakini hakidhi competency ktk kila eneo la kile alichobobeaa. Kesho unatumia kigezo sawa Cha GPA kwa watu wawili kutoka ktk mifumo miwili tofauti. This is insane.
Degree ya TEKU UALIMU ni bora kuliko ya UDSM, wanafunzi hawajua hata kuandaa teaching aids na learning materials, hajui kuandaa lesson plans, hawajui kuandaa scheme of work, yani hadi lesson notes kuandaa tu shda, chakungaza zaid Had dressing code ni mtihani. SASA utajiuliza akiingia darasani anafanya nn maana hata introduction ya somo hajui inakuaje, development inakuaje and so on. SASA huyo mtu unategemea atakua competent KWELI? WANABEBWA NA MAJINA YA CHUO TU KICHWANI EMPTY KABISA.

USHAIDI NINAO
 
GPA ya 3.8 si kigezo tena. Serikali kupitia kwa Waziri wa Elimu Prof. Mkenda ashakataza watu kuchujwa kwa kigezo cha GPA badala yake washindane kwenye interview. Naona UDSM wamefanya hivo kwenye hizi kazi.
GPA ya 3.8 ni kigezo mkuu. Pitia tangazo..

GENERAL QUALIFICATIONS:
a. Lecturer: Applicants for the post of Lecturer must possess a PhD, a minimum GPA of
4.0 or a B+ average at Master’s degree level and an undergraduate degree with an
overall GPA of 3.8 or higher from an internationally reputable higher learning
institution. They must be potentially good academically.

b. Assistant Lecturer: Applicants for the post of Assistant Lecturer must possess a
minimum GPA of 4.0 or a B+ average at Master’s degree level and an undergraduate
degree with an overall GPA of 3.8 or higher from an internationally reputable higher
learning institution. They must be potentially good academically.

c. Tutorial Assistant: Applicants for the post of Tutorial Assistant must possess a
Bachelor degree with a minimum GPA of 3.8 from an internationally reputable higher
learning institution.
 
Back
Top Bottom