Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko


Mkuu umeongea yote!

Kuna kipindi ilikuwa ukisema mi sisikilizagi bongo fleva nasikiliza mziki wa nje unaonekana mjanja sana. Sasa hiyo hali ndo inatokea kwa bongo movie sa hiii.

Yaani ili uonekane modern ni lazima useme "siangaliagi bongo movie".

Siangalii bongo movie alafu hapo hapo anatoa makosa kibao yaliyotokea kwenye filamu. Sasa unajiuliza kama haangaalii amejuaje hayo makosa.

Tuna safari ndefu sana.
 

Comedy inafanya vipi vizuri? Kwa mwaka 2020 nitajie filamu tano za comedy zilizouza sana Tanzania?

Yaaani mizengwe unaweza kufananisha na Huba au Shilingi ya dstv

Ringo na Pembe wameingiza how much kutokana na filamu walizotoa mwaka jana?
Filamu gani ya comedy kutokea Tanzania kwa sababu ya ubora wake imeingia NETFLIX, HULU, DISNEY + au any major streaming platform.

Na unamaanisha nini watu wa comedy wanafanya vizuri? Au kwa sababu unacheka?

Alafu mbona hayo mambo ya wadada warembo mlikuwa hamyasemi kipindi cha kanumba? Wema sikatokea huko huko? Priyanka hajasomea filamu alikuwa ni miss world mbona ni muigizaji mzuri tu? Ebu nijibu mkuu nikuelewe
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu hawa watu lazima wawe na utaalamu kuhusu fani husika.

Kama mtu anaigiza udaktari basi aigize kweli aelewe mambo muhimu ya udaktari juu ya script anayocheza.

Sio unaigiza daktari alafu umevaa nguo za nesi.

Kama mtu anaigiza polisi kweli awe na taaluma kuhusu upolisi,sio polisi wa kituoni na nguo zake za kaki ati ana ndevu wakati polisi wale hawatakiwi kufuga ndevu.

Sio polisi wawili wameenda kukamata kila polisi anamwita mwenzie afande wakati kijeshi lazima kuna mmoja atakuwa senior na mwingine mdogo

Sio mtu anaigiza movie ya kijeshi ati private wa jeshi anampigia saluti coplo wa jeshi jambo ambalo halipo na ni upuuzi.

Kiufupi wanaigiza kama watoto wadogo vile wakati wenzetu huko nje unajiuliza ni kweli ama maigizo wakati huo hapa bongo unaona kabisa hapa ni changa la macho.

Wanachofanya bongo movie ni kutudanganya hata juu ya wanachoigiza,yaani huwezi kujifunza kitu cha ukweli kwenye movie za bongo

Coplo kumpigia saluti coplo ni uongo kiuhalisia haipo hivyo kwa hiyo movie zetu wanatudanganya na ndo wanazidisha ujinga kwenye jamii kwa kuwaigizia watu jambo ambalo silo.

Kwenye mapenzi oooooh wanajua kuigiza sana hasa ukikuta mwanaume the way anareact akiona demu mwenye chura utaona kabisa ni kama wamekuona wewe lakini wapii they are experts katika hiyo sector ya mapenzi na ngono.

Nilishawahi kuwaza na mimi nije kuwa muigizaji ili nielimishe jamii juu ya mambo mbali mbali ya Nchi hii kwa kuigiza kitu cha ukweli kutokana na wao kuharibu tasnia hii lakini ndo nina malengo mengine tofauti na uigizaji.
 
Hizo ndizo fikra zenu za kimaskini, unauliza watamuuzia nani, Kuna mtu haangalii kitu kizuri?, hebu fanyeni hivyo muone kama hamtopata wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi,

Kama mnaweza kukopeshana pesa hadi kufikia hatua ya kutukanana matusi ya nguoni kwanini msiungane mkachukua mkopo bank na kufanya mambo makubwa?

Angalieni wenzenu wa Bongo flavor wanavyojitahidi, sasa hivi hadi Wamarekani wameanza kufanya collabo na Waafrica baada ya kuona hatusikilizi tena miziki yao tupo busy na ya kwetu, kwanini Bongo movies msibadilike kama Bongo flavor? Na kama hamuwezi basi mtuachie fursa sie wapya tufanye mapinduzi lakini bado mnatubania,

Aibu yenu.
 
Vionjo kama hivyo havikosi,wabongo wanataka sana kufanya hivyo lakini hata teknolojia hiyo hawana watababaisha babaisha.

Wabongo wanataka sana wawe na utaalamu ule lakini hawawezi.

Vile vionjo vinanogesha movie hapa bongo ovyo kaka,tusijifiche kwenye kivuli cha kupenda vya kwetu wakati ni vya ovyo.

Ili tuvipende lazima tuvikosoe
 


Mkuu naomba unitajie jina la hiyo muvi ambayo koplo anampigia saluti koplo au ni mwigizaji gani aliigiza kwa hiyo movie ili niitafute.

Tusije tukawa tunaongelea vitu ambavyo havipo ili tu tufurahishe umma
 
Kuna yule mama anaact kama waziri, khaa yale ndio maisha ya waziri kweli? Si bora hata wangesema ni mfanyabiashara mkubwa basi ikatosha,

Wanasingizia bajeti, lakini wanakopeshana pesa hadi kutukanana matusi mazito mazito,
Hayo madanga wanayopasiana wanashindwa kuwaomba wawafadhili wafanye movie moja matata yenye story nzuri ya kusisimua,

Shida directors wao, producers wao, Editors wao, halafu ushikaji mwingi wanafanya kazi kimazoea sana.
 
Sasa kama hauna huo muda mchafu na hujawahi kuangalia umejuaje hawana ubunifu na movie zao zote wanaigiza mapenzi?

Unaijua movie ya safari ya Gwalu ya Gabo? Kuna mapenzi mule?

Yaaani umejuaje ka huangalii?
Oi dingi usinichoshe na mautopolo yenu. Kiujumla hamna ubunifu yani hamna jambo jipya yani mmefulia.
 
Wenzako wamesomea sanaa unajua elimu ya Priyanka au unacomment tu, unajua elimu ya madirector wao
 

Hao wanunuzi wa ndani na nje ya nchi wanapatikana vipi? Kwenye nchi zilizoendelea hamna anayeuza physical copies tena KAMA STEPS kwa sababu ya uharamia.
Movie duniani kote zinauzwa kwa kutumia MOVIE TICKETS kwenye Cinemas. Bongo kuna cinemas ngapi? Unataka JB ajengee sinema?

Hollywood, Bollywood, Nollywood na Han Cinema ya Korea kila sehemu kuna Cinemas kuonyesha movie. Enheeee bongo unatengeneza movie ya 1 B umechukua mkopo bank hela yako unarudishaje?

Na kamwe usifananishe bongo fleva na bongo movie.

Bongo fleva wamepata mkombozi mtu ana uhakika akitoa album ANAUZIA WAPI Youtube, audio mack apple music na march hapa spotify amekuja bongo kuuza kazi za wasanii?
Niambie Unatengeneza big budget movie utaweka youtube? Hela yako itarudi?

Mnalamika bure. Ishu ni mfumo na CCM.

Acha kulalamika.
 
Tatizo hamjui halafu hamtaki kukosolewa, mnasingizia bajeti wakati kila mara mnatoa moviee wenzenu movie moja wanaweza kutoa baada ya miaka mitatu wakati nyinyi mwaka mmoja mmeshatoa movies zaidi ya nne.
Muda wa kufanya research hamna wala kutathimini namna gani movie imefanyaje kwenye soko.
 
Toeni basi movie ya kuonyesha mfumo na ccm wanavyowaatiri vinginevyo mtabaki kuchangishana rambirambi na kuibiana maana hicho ndio mnakiweza
 
Wenzako wamesomea sanaa unajua elimu ya Priyanka au unacomment tu, unajua elimu ya madirector wao


Daaah yaaani wewe wa kuniuliza mimi elimu ya priyanka chopra? Wenzio hayo mambo ndo tunafanyia presentation.

Priyanka hajasomea film. Alikuwa mrembo na baada ya kushinda tu miss world Abbas akumuita kufanya nae movie 2002. Yaaani infact hakwenda ata chuo.
 
Yees ni unafki tu nakufata mkumbo wengi wao humu kujifanya wako educated sana ,,etii ooh ulaya hakuna muigizaji asie na degreee,,.

ooh me kwangu nimepiga marufuku bongo movie, lakini wasanii wote wa bongo movie anawajua sa sijui amewajulia wapi[emoji23][emoji23]
 
Umeulizwa elimu yake unaleta maneno mengine kumbe na wewe ni walewale
 
CCM ndio wanawafundisha nyie kuigiza? Mbona ngono mnazipatia? Nchi hii ni kubwa sana yaan mmeshaizunguka koooote mkatafuta hata stories za makabila flan mkaigiza? Kuna locations chungu nzima mnashindwa kwenda huko mkaigiza muachane na locations za mahotelini? Big budget gani, watu wanasema hamna ubunifu, stories zenu ni zile zile za mapenzi na uchawi, waigizaji hawana viwango, mnajali makalio na hereni za kuning'inia na make ups kama clowns,

Mpishe wasomi waliosomea tasnia hiyo wapige kazi na wao, sura zenu haziuziki tena.

Tunalalamika sie au nyie? Mngekua mnafanya kitu cha kuonekana hata serikali ingewekeza.
 
Nafikiri hoja yako sijui kama ina maana la zaidi ni post ya udhalilishaji. Kuna vitu ni talent. Kuwa akili ya kujibu physics hakukupi talent ya kuwa muigizaji nzuri. Nafikiri unashindwa kuheshimu kwamba uigizaji unahitaji kipaji na sio kila mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…