Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko


Sasa tunaenda sawa.

Movie zilikuwa mbaya na zilikuwa zinapendwa kwa sababu ya jamii kuwa gizani, elimu duni, na mitandao ilikuwa bado haijachanganya.

Wasanii walipaswa wabadilike kulingana na nyakati, waligundue hili mapema kabla haijala kwao, wao wakazubaa.

Kipindi kile ishu sio kuigiza, ishu ilikuwa ni kuonekana kwenye TV bila kujali unaongea nini, nchi ilikuwa ushambani, sasa kila mtu ni mjanja kasoro tuu waigizaji ambao wanadhani jamii yao ni ile ile.
 
Huwezi fananisha Bongo Flavor na Bongo movie, Movie industry ni tasnia inayohitaji taaluma na uekezaji mkubwa, tofauti na masuala ya music.

Mkuu tunachozungumzia hapa, ni kuwa hata huo uwekezaji mdogo uliofanywa mbona hatuoni la maana?
Ndio nikasema shida shule ndogo kwa wasanii wengi na wahusika wa filamu.

Filamu nyingi zimelenga mambo ya kitoto.

Yaani Watu wazima wanaigiza kama watoto, kimama mama na kibaba baba bhana!!!!!!!!!!!!
 
Serekali haijawahi kuwa serious na masuala ya filamu, hawaelewi kama ni moja ya sehemu inayoweza kuwaingizia kipato kikubwa tu, India film Industry inachangia asilimia 12 ya pato la nchi kila mwaka.
 
Steps hakufungiwa bali aliondoka mwenyewe baada ya kuona amebanwa kodi
 

Mambo ya maana yanahitaji bajet kubwa. Vipaji vipo. Madairekta wapo mnaweza kukodi hata nje. Mbona wakina Campos na Ogopa videos wamekula sana mipunga ya kina AY?

Yaaani serikali waanze kuichukulia hii industry seriously uone kama movie za mkwawa hazijatengenezwa.
 
Serekali haijawahi kuwa serious na masuala ya filamu, hawaelewi kama ni moja ya sehemu inayoweza kuwaingizia kipato kikubwa tu, India film Industry inachangia asilimia 12 ya pato la nchi kila mwaka.

Serikali unataka iwe sirius ili watu wapoteze vitumbua vyao?

Serikali ikiitambua Fani ya uigizaji itaweka vigezo lazima uwe na Diploma au degree moja unafikiri wangapi watabaki hapo?
Kisha watu wapewe leseni
 

Wamekula mpunga kwenye Filamu ipi?
Au unazungumzia hizi video za muziki boss?

Hizi hiz movie wanazoigiza za bajeti ndogo mbona ni kama wanaigiza kimama mama na kibaba baba. Mtu na akili zake hawezi ketisha masaburi yake akaangalia

Watunzi wana stori za kitoto toto, yaani filamu haina hata sehemu ya kutafakarisha, sehemu ya Watch part 2 ndio vituko vituko
 

Sio Priyanka tu, Aishwarya Rai, Sushmita Sen, Juhi Chawla wote waliingia Bollywood kwa njia hiyo hiyo, kuna wengi walikua ni mamodel wakatisua pia, akina Arjun Rampal, Deepika.
Kareena Kapoor aliishia darasa la 12 tu, hata college hajafika, hivi sasa ni katika Most Successful FIlm Actress ever pale Bollywood.
 
Steps hakufungiwa bali aliondoka mwenyewe baada ya kuona amebanwa kodi

Mkuu ni kwamba hujui au free market works? Ushasema walibanwa kodi sasa ulitegemea wangeendelea kufanya biashara?

Okay fine walikuja na mechanism gani kuhakikisha the movie industry inapata distributor mwengine?

Serikali yenu imeshindwa hata kuita kampuni kama SILVER BIRD ya nigeria itengeneze sinemas watu wauze movie? JB angepata faida si ndo angeendelea kutengeneza movie nzuri zaidi?.

Sasa JB atatengenezaje movie nzuri kama hana hata sehemu ya kuuzia movie zake
 
Anzeni kutengeneza movies nzuri hizo foleni zitakuwepo sasa mwataka tupange foleni kuangalia vile mnavyongonoka?
Mpo serious kweli na kazi? Mbona tunapanga foleni kuingia kwenye shows za Music?
point umeshindwa kuifahamu, Rome haikujengwa kwa siku moja, Leo Bollywood wanatengeneza filamu zenye ubora wakukaribiana na Hollywood , hili halikuja kirahisi, ni support waliokua wanaipata kutoka kwa watu ndio iliwawezesha wao kuweza kusogea kiubora.
Ni ngumu kujitokeza kwa financers wakaekeza fedha zao bila ya kuwa na Imani alau ya kurudi fedha zao achilia kupata faida, hivi mtu aje atoe milioni zake 200, aekeze kwenye filamu zitarudi kwa njia gani hapa bongo?
 
Kizuri hujiuza ndo maana wakina Vandame wanaweza kuwa hawajui hata kuna nchi inaitwa TANZANIA ila huku ana ma role model kibao ukiacha mashabiki.TUACHENI VISINGIZIO SASA WE LI MTU(JENGUA)LINAIGIZA LINAPENDWA KICHIZI MPAKA DEMU ANAJIUA UKIANGALIA SURA YA JENGUA KAMA PALAMAGAMBA KABUDI JUMLISHA NA MIJICHO YAO we unaona watu wa TASNIA YA BONGO MOVIES WAPO SERIOUS
 

Mkuu umeelezea vizuri sana. Watu hawaelewi haya mambo. Na sio india tu korea kuna dada mmoja anaitwa IU ameigiza series ya Hotel De Luna as leading actress . Yule ni mwimbaji pure hakuingia darasani ila alikuwa na kipaji na mapenzi lakini namna anavyofanya vitu vyake ndani yacile series ni hatari.

Bongo badala tuangalie mzizi wa tatizo ni nini tunaanza kusema kisa wasanii hawajasoma, mara sijui kuna majungu sana, hivi kweli kuna industry ambayo hamna chokochoko na mabifu?

Kiukweli Tuna safari ndefu sana mkuu.
 
Hiyo sio hoja mkuu, hatua inayokua refu kwenye kutengeneza filamu ni script writing, ila ukishakua na script mkononi shooting na post production hata miezi mitatu yaweza tosha inategemea na scale ya filamu yenyewe, filamu zinazochukua mda ni zile za science fiction, lakini drama na romance hazina shida kabisa.
 
Bro VICENT KIGOSI mbona umekuja juu hivyo
 
Nyinyi kila kitu mnasema serikali, serikali ndio inawaambia mtengeneze filamu za ovyo, kuna filamu kama Neria ya Zimbabwe, sinema kama hizo mnaweza kupata hata sponsor US aid na taasisi nyingine kutokana na maudhui yake
 
Kweli hii n fursa kwa vijana. Wakaka wanachibua tu badala ya kupiga kazi. Wadada wapo sokoni nao.
 
Hapo ndio mnakosea, kuna muda sinema inatakiwa ikae sokoni lakini wewe kila miezi 3 unatoa filamu hapo unategemea nini
 

Unaninisikitisha sana mkuu. Kuna kitu kinaitwa GLOBALIZATION.

Sasa hivi watu mnataka movie za kibongo ziwe na quality za hollywood ndio muangalie. Foreign movies ziko everywhere ni mb tu unashusha. Mkiangalia mnafananisha na movie zetu huku bongo mnaconclude tuna movie zisizo na kiwango (which is true)

Mnachosahau ni kuwa kipindi kile soko lilikuwa ni la bongo movie tu hivyo ni lazima uangalie tu. Hakukuwa na netflix wala youtube.
 
eti watu kwenye bongo flavor wanaongea muda wote wanafoka najiulizaga maisha ndo yalivyo hivyo kweli
 
Nyinyi kila kitu mnasema serikali, serikali ndio inawaambia mtengeneze filamu za ovyo, kuna filamu kama Neria ya Zimbabwe, sinema kama hizo mnaweza kupata hata sponsor US aid na taasisi nyingine kutokana na maudhui yake

Hamna aliyesema serikali idairekt movie au ifanye recruitment ya actors. Kwanini wasanii wakitaka msaada wa serikali mnashangaa?, kwani wao hawahitaji usimamizi kwenye kazi zao?

Ishu ni kuwa hujawahi kuwa kwenye kiwanda cha filamu. Swali dogo tu tumetengeneza movie hiyo tumeita sponsors n.k JE BONGO.... FILAMU INAUZWA VIPI? HATUNA SINEMAZ. WEWE UNAWEZA KUSTREAM FILAMU NETFLIX? na bando lako buku jero mkuu?

Its not about quality au waigizaji au sponsors ao wapo tu. Kwani sponsors hawapo? Faida inarudi vipi? Mna sinemaz? Mna stream?

Mkuu naomba ukasome how film industry works ndo tuje kuendelea na mjadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…