Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

Hiyo hoja ikikubaliwa mniite mbwa, niko nyuma ya keyboard nimekaa.
CCM ni waoga wa kila kitu.

Hata kitoto kidogo kikiongea kitu, ambacho hawakipendi utaanza kuona kimepelekewa mavifaru ya Jeshi.

Huu uoga wa CCM ndio unapeleka wanaogopa KILA KITU, KILA MTU na wana tahadhari muda wote.

Kinachokwamisha hili suala ni uoga tu.

Leo kuna Msanii wa nyiumbo za asili kafungwa miaka 6 huko Chato utafikiri ana uwezo hata wa kupindua serikali
 
Hiyo hoja ikikubaliwa mniite mbwa, niko nyuma ya keyboard nimekaa.
Tema mate chini usikalili dunia inabadilika usipobadilka itakubadilisha.
Kwa asili ya binadamu Hana mpaka Hilo ni suala la uitawala sio asili ya binadamu.
Ndiyo maana utakuta watu walitoka sehemu tofauti tofauti
 
Uwepo wa viongozi wazee wengi serikalini unachangia kupuuzia hii hoja.Rais teua vijana mazee hayo yana mawazo mufilisi hayajui hata tiktok wala instagram hayapo modern
Vijana hawafai ni wezi sana. Mfano Awesu na Biteku washaiba na kujitajitisha sana
 
Tema mate chini usikalili dunia inabadilika usipobadilka itakubadilisha.
Kwa asili ya binadamu Hana mpaka Hilo ni suala la uitawala sio asili ya binadamu.
Ndiyo maana utakuta watu walitoka sehemu tofauti tofauti
Suala la dunia kubadilika mimi sina shida nalo aise. Ila hoja hapa ni uraia pacha na ni kitu ambacho hakijaanza kuongelewa leo au jana.

Hilo suala lilishatolewa hoja mda sana na tena kama lingepita basi ingekuwa ni utawala wa Kikwete.

Kwa sasa tukitaka lipite basi lazima kuna kizazi kipotee kwanza, kije kizazi cha vijana. Tanzania protectionism ni kali sana kuanzia suala la ardhi mpaka uraia.
 
CCM ni waoga wa kila kitu.

Hata kitoto kidogo kikiongea kitu, ambacho hawakipendi utaanza kuona nkimepelekewa mavifaru ya Jeshi.

Huu uoga wa CCM ndio unapeleka wanaogopa KILA KITU, KILA MTU na wana tahadhari muda wote.

Kinachokwamisha hili suala ni uoga tu.
Hiyo hoja labda kuanzia 2040 ndio itaweza jadilika ila kwa sasa sijui na wakisema waikubali jua wako likely kuweka limit katika kujihusisha na siasa
 
Hiyo hoja labda kuanzia 2040 ndio itaweza jadilika ila kwa sasa sijui na wakisema waikubali jua wako likely kuweka limit katika kujihusisha na siasa
Wamesha sema Wana mpango wa kuwapa hadhi Maalum.

Tafsiri yake ni kuwaweka kwenye CAGE ili wawe na uwezo wa kuwadhibiti au kuwavua hiyo hadhi wakikataa mambo yao
 
Kuna mambo ambayo viongozi wanakaza fuvu tu ila hayakwepeki kwajinsi dunia inavyokimbia.tulitakiwa tukimbie nayo kwajinsi yanavyokuja ili tujue namna sahihi yakuenda nayo.badala yakukaza fuvu alafu yakaja kwa msukumo mkubwa bila sisi kujiandaa.matokeo yake unajikuta unafanya kitu cha ovyo wakati tulikua na uwezo wakulifanya vizuri kwa maandalizi sahihi sio kuyakwepa au kujifanya hayapo au kunifanya hatuna umuhim nayo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wamesha sema Wana mpango wa kuwapa hadhi Maalum.

Tafsiri yake ni kuwaweka kwenye CAGE ili wawe na uwezo wa kuwadhibiti au kuwavua hiyo hadhi wakikataa mambo yao
Hii naona ilinipita. Asante kwa kunifunua ubongo. Ngoja nifuatilie
 
Hatutaki uraia pacha hadi uwe accessible kwa wote. Tunataka Muuza vitumbua aweze kupata uraia pacha kama ambavyo anaweza kuupata mtu kama MO. Hapo ndiyo tutakubali.
 
Hii ndio tunaita ukimchekea mbwa atakufuata hadi msikitini,sasa huyu mzungu uchwara kaingia hadi chumbani, yeye si Mtanzania inakuwaje azungumzia mambo nyeti.
Ana watoto ambao wamezaliwa Tz, wanafikisha miaka kumi na nane ghafla wanatakiwa kukana uraia wao! Usiangalie nani kasema, angalia Nini kasema! Halafu Tz sio kwamba ndio Ina vitu vya maaaaaaaaana kuliko nchi zilizoruhusu uraia pacha
 
Kulingana na hoja za Bongo Zozo raia wa Tanzania waliopo ughaibuni wananyimwa fursa ya kuendeleza nchi yao. Aidha Tanzania inakosa fursa ya kupata huduma kutoka kwao

Tuna Jambo la kujadili ili tupate muafaka!

View attachment 2606631
Tatizo wanaolilia uraia pacha si watanzania tena. Ni kama bongo zozo, na wengine ambao walishaukana uraia wa Tanzania hali wakijua tz kwa sasa hairuhusu uraia pacha. Wameshakuwa foreigners hawawezi wakatuamulia wala kutusemea mambo ya ndani ya nchi yetu. Waheshimu sheria za kimataifa.

Walipaswa wapiganie uraia pacha wakiwa bado ni watanzania, ndipo sauti zao zingesikika.
 
Uwepo wa viongozi wazee wengi serikalini unachangia kupuuzia hii hoja.Rais teua vijana mazee hayo yana mawazo mufilisi hayajui hata tiktok wala instagram hayapo modern
Wameshindwa kutatua uchafu wa jiji na mifereji kuziba wataweza kujua diaspora mchango wao?
 
Angalia mchango wa wenzetu na sisi kwa ujinga wetu
Screenshot_20230502_075345_Google.jpg
Screenshot_20230502_075641_Google.jpg
Screenshot_20230502_075529_Chrome.jpg
 
Hii ni sawa na Mtoto aliyezaliwa katika familia yenye uwezo wa wastani au duni kiuchumi kutamani kuhamia kwa jirani kwasababu tuu ni matajiri na Wana uwezo mkubwa kiuchumi...mimi nashauri watanzania waichukue changamoto hii kama chachu ya kubuni namna ya kuzifanya fursa zilizoko Tanzania kuwa na manufaa kimapato na kuifanya Tanzania sehemu nzuri ya kuishi.

Hilo likifanyika ata akina Zozo watazikana nchi zao na kuomba uraia wa Tanzania ili wafaidi fursa anazozitaka...

Zozo anasema ukiwa na passport ya nchi yake unaweza kutembea Dunia nzima Bila kikwazo...kwa lugha nyingine anasema nchi zote ambazo wananchi wake wanapata taabu sana kupewa visa na nchi Tajiri, wajiunge na Nchi hizo ili wa-explore Dunia.

Zozo amesahau kutwambia kuna Waingereza wangapi Nchini mwake hawajawahi kutoka katika county walizozaliwa,na hiyo yote ni kutokana na maeneo yao kuwa na kila kitu kwa maana ya huduma za kijamii na maisha Bora .

Kwahiyo watanzania tupambanie kuiendeleza nchi Bila kutegemea sana benefis na fursa za nchi nyingine...Sisi wenyewe ni fursa..na ndio maana hujawahi kuwasikia Watanzania waishio Somalia, Ethiopia, au Burundi wakilalamikia Dual nationality.
 
Back
Top Bottom