Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

Ana watoto ambao wamezaliwa Tz, wanafikisha miaka kumi na nane ghafla wanatakiwa kukana uraia wao! Usiangalie nani kasema, angalia Nini kasema! Halafu Tz sio kwamba ndio Ina vitu vya maaaaaaaaana kuliko nchi zilizoruhusu uraia pacha
Sio lazima waukane...kama wanapenda Tanzania wabaki na uraia wao na huko Uingereza watapewa permanent resident permit ambayo watapata almost similar treatment kama za raia wa UK Except passports
 
Sio lazima waukane...kama wanapenda Tanzania wabaki na uraia wao na huko Uingereza watapewa permanent resident permit ambayo watapata almost similar treatment kama za raia wa UK Except passports
Hofu ya uraia pacha ni Nini?
 
Urai pacha ni muhimu kwa maendeleo ya taifa, kwani kuna watanzania kibao wapo nje wanatamani kuleta uwekezaji Tanzania wanashindwa kwa sababu ya gharama za kuja kama wawekezaji bado masuala ya ununuzi wa ardhi
Nimegoma kuukana utanzania kwa zaidi ya miaka kumi nikisubiri uraia pacha sasa natoa mwaka mmoja nije kukabidhi uraia wenu. Utanzania una gharama kubwa aisee ndo maana hata mabeberu wakihitaji nguvu kazi wanachota nigeria na kenya. Sijui tunakwama wapi
 
Hatutaki uraia pacha hadi uwe accessible kwa wote. Tunataka Muuza vitumbua aweze kupata uraia pacha kama ambavyo anaweza kuupata mtu kama MO. Hapo ndiyo tutakubali.
Nyie ndio wale mliochelewesha uhuru eti tusipewe uhuru hadi wote tulielimike. Hopeless.
 
Sio lazima waukane...kama wanapenda Tanzania wabaki na uraia wao na huko Uingereza watapewa permanent resident permit ambayo watapata almost similar treatment kama za raia wa UK Except passports
Umemsikia lakini ? Passport ni moja ya checklist zake muhimu. I.have done the same na ushauri wako si regret .
 
Suala la dunia kubadilika mimi sina shida nalo aise. Ila hoja hapa ni uraia pacha na ni kitu ambacho hakijaanza kuongelewa leo au jana.

Hilo suala lilishatolewa hoja mda sana na tena kama lingepita basi ingekuwa ni utawala wa Kikwete.

Kwa sasa tukitaka lipite basi lazima kuna kizazi kipotee kwanza, kije kizazi cha vijana. Tanzania protectionism ni kali sana kuanzia suala la ardhi mpaka uraia.
Kuna kizazi chenye vimelea sugu hakipotei aisee unakuta kitukuu kinafanana copyright na vibabu.
 
Urai pacha ni muhimu kwa maendeleo ya taifa, kwani kuna watanzania kibao wapo nje wanatamani kuleta uwekezaji Tanzania wanashindwa kwa sababu ya gharama za kuja kama wawekezaji bado masuala ya ununuzi wa ardhi
Na nchi kama US sasa hivi wanafuatilia sana transactions za watu wanaofanya kazi kule. Kutumatuma hela kiwango kikubwa au mara tatu ndani ya mwezi lazima account yako waiminye na kukutaka ujielezee.
Hapo ndiyo mtaona watu wanakubali yaishe kwa kuamua kutotuma hela kuliko habari za kuonywa onywa
 
Hii ndio tunaita ukimchekea mbwa atakufuata hadi msikitini,sasa huyu mzungu uchwara kaingia hadi chumbani, yeye si Mtanzania inakuwaje azungumzia mambo nyeti.
haupo kweny field inayoguswa na hilo swala ndio maana ngumu kuelewa
 
Kulingana na hoja za Bongo Zozo raia wa Tanzania waliopo ughaibuni wananyimwa fursa ya kuendeleza nchi yao. Aidha Tanzania inakosa fursa ya kupata huduma kutoka kwao

Tuna Jambo la kujadili ili tupate muafaka!

View attachment 2606631
Jamaa nmemuelewa, uraia pacha usiwe kwa watu wa nje lakini uwe ni kwa ajili ya haya makundi mawili ya watanzania

1)Watoto walozaliwa na wazazi ambapo mzazi mmojawapo ni mtanzania

2)Watanzania ambao wapo nje (ughaibuni) waruhusiwe kuwa raia wa hizo nchi pamoja na kuwa bado watanzania.

Hio itazuia hofu iliopo kwamba mwekezaji wa nje ataomba uraia wa tz then aje abebe rasilimali za wazawa kwa sababu haki ya uraia pacha wanapewa wazawa tu.

Bongo zozo kwa hili ana point nzuri sana kiukweli.
 
Urai pacha ni muhimu kwa maendeleo ya taifa, kwani kuna watanzania kibao wapo nje wanatamani kuleta uwekezaji Tanzania wanashindwa kwa sababu ya gharama za kuja kama wawekezaji bado masuala ya ununuzi wa ardhi

Hamna bana, mbona kuna waTanzania kibao diaspora wanawekeza bila presha bongo?
 
Aende akatoe hoja yake huko Uingereza. Bado tunakumbuka jinsi walivyowatesa mababu zetu.

Mwaambie tunaukumbuka ukoloni wao
Peke yako ndiye uliyebaki na ujinga huo!
 
Tatizo wanaolilia uraia pacha si watanzania tena. Ni kama bongo zozo, na wengine ambao walishaukana uraia wa Tanzania hali wakijua tz kwa sasa hairuhusu uraia pacha. Wameshakuwa foreigners hawawezi wakatuamulia wala kutusemea mambo ya ndani ya nchi yetu. Waheshimu sheria za kimataifa.

Walipaswa wapiganie uraia pacha wakiwa bado ni watanzania, ndipo sauti zao zingesikika.
Bongo Zozo hajawahi kuwa raia wa Tanzania, yeye ni Mwingereza tangu azaliwe!
 
Na nchi kama US sasa hivi wanafuatilia sana transactions za watu wanaofanya kazi kuke. Kutumatuma hela kiwango kikubwa au mara tatu lazima account yako waiminye.
Hapo ndiyo mtaona watu wanakubali yaishe kwa kuamua kutotuma hela kuliko habari za kuonywa onywa

Kwa hiyo unataka kusema remittance ya diaspora itaanza kupungua worldwide?
 
Bongo Zozo hajawahi kuwa raia wa Tanzania, yeye ni Mwingereza tangu azaliwe!
kwani nimesema ni mtanzania au aliwahi kuwa mtazania?

msisitizo wangu ni kwamba mtu asiye raia wa tz hawezi akasema jambo kisha serikali ikamsikiliza. Hata hao walioukana uraia kisha wanataka serikali iwasikilize, serikali haiwezi ikamsikiliza mtu asiye raia kuhusiana na masuala ya ndani ya nchi.
 
Back
Top Bottom