Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

Jamaa nmemuelewa, uraia pacha usiwe kwa watu wa nje lakini uwe ni kwa ajili ya haya makundi mawili ya watanzania

1)Watoto walozaliwa na wazazi ambapo mzazi mmojawapo ni mtanzania

2)Watanzania ambao wapo nje (ughaibuni) waruhusiwe kuwa raia wa hizo nchi pamoja na kuwa bado watanzania.

Hio itazuia hofu iliopo kwamba mwekezaji wa nje ataomba uraia wa tz then aje abebe rasilimali za wazawa kwa sababu haki ya uraia pacha wanapewa wazawa tu.

Bongo zozo kwa hili ana point nzuri sana kiukweli.
Hakika kabisa! Kuliko hivi sasa tumebaki kujisifia watu ambao tayari walikwisha ukana uraia wa Tanzania kama Sunak Waziri Mkuu wa UK wa sasa ni Mtanzania, au huyu mwafrika ambaye amechaguliwa kuwa seneta huko Ujerumani ni Mtanzania kwa kuwa tu wazazi wake ni wa asili ya Tanzania au yule Mzanzibari mwandishi wa vitabu ambaye sasa ana uraia wa Uingereza.

Tunapaswa kubadilika!
 
kwani nimesema ni mtanzania au aliwahi kuwa mtazania?

msisitizo wangu ni kwamba mtu asiye raia wa tz hawezi akasema jambo kisha serikali ikamsikiliza. Hata hao walioukana uraia kisha wanataka serikali iwasikilize, serikali haiwezi ikamsikiliza mtu asiye raia kuhusiana na masuala ya ndani ya nchi.
Mbona masuala ya ushoga na ndoa za jinsia moja serikali ilinywea baada ya nchi za magharibi kuijia juu na kukanusha maneno Makonda?
 
Mbona masuala ya ushoga na ndoa za jinsia moja serikali ilinywea baada ya nchi za magharibi kuijia juu na kukanusha maneno Makonda?
anzisha uzi kuhusiana na ushoga na usagaji, huu uzi unahusu masuala ya uraia pacha
 
CCM ni waoga wa kila kitu.

Hata kitoto kidogo kikiongea kitu, ambacho hawakipendi utaanza kuona nkimepelekewa mavifaru ya Jeshi.

Huu uoga wa CCM ndio unapeleka wanaogopa KILA KITU, KILA MTU na wana tahadhari muda wote.

Kinachokwamisha hili suala ni uoga tu.
Umemaliza !!
 
Na nchi kama US sasa hivi wanafuatilia sana transactions za watu wanaofanya kazi kule. Kutumatuma hela kiwango kikubwa au mara tatu ndani ya mwezi lazima account yako waiminye na kukutaka ujielezee.
Hapo ndiyo mtaona watu wanakubali yaishe kwa kuamua kutotuma hela kuliko habari za kuonywa onywa
Pesa unatuma hata mara kumi kwa siku hakuna mtu wa kutaka ujieleze labda kama ni pesa za magumashi.
 
Wanasiasa wanawaza kutawala tu, hawawezi kuikubari.
Nchi kubwa na ndogo duniani ambazo zinajali mataifa yao na yanajali utaifa wao tena ni wazalendo kweri kweri wala hawaziibii Nchi zao na wameruhusu Uraia pacha !! Sisi tuna uzalendo gani wa kutufanya tuukatae Uraia pacha ??!! Eti tunalinda utaifa wetu !! Khaa !! Tumuulize CAG kama kweli hao watu ni wazalendo wenye kujali Utaifa wao 😅😅🙏
 
Back
Top Bottom