Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

hili watu hawalioni........
na tunaweza kuwa na mawaziri nusu watanzania, nusu wamarekani...... sijui wata-serve interest za nani
Ujinga gani huu jamani kwani huwezi kuweka Sheria ya kuwazuia kugombea huo urais wenu! kwingine kukaachwa huru, waziri mkuu wa sasa wa uingereza Ana asili ya India,makamu wa rais wa marekani je?. Ni hasara Sana kuwa masikini Kisha ukawa masikini wa akili na mchoyo.
 
Hadi sasa bila hata kuwa na uraia pacha bado kuna mawaziri wana-serve interest zao na za wawekezaji!
Interest zao na ndugu zao hakuna mwekezaji mjinga atawekeza kwenye nchi yenye rushwa kwa sababu anakuwa anapoteza mali zake kwa hiyo usifikiri mwekezaji inabidi awe Mtanzania ndio awekeze hilo nalo ni maajabu ya Tanzania
 
Interest zao na ndugu zao hakuna mwekezaji mjinga atawekeza kwenye nchi yenye rushwa kwa sababu anakuwa anapoteza mali zake kwa hiyo usifikiri mwekezaji inabidi awe Mtanzania ndio awekeze hilo nalo ni maajabu ya Tanzania
Bila shaka hilo ni ajabu lako!
 
Waulize Wana siasa watakuambia madhara ya uraia pacha Ila ni Siri yao
Hao wanasiasa wanaogopa kuruhusu urai pacha kwani itabidi warudishe mali za watu waliowapora wakisingizia sio Watanzania hiyo ndio Siri kali kesi zitakuwa nyingi mno na wataumbuka
 
Tatizo wanaolilia uraia pacha si watanzania tena. Ni kama bongo zozo, na wengine ambao walishaukana uraia wa Tanzania hali wakijua tz kwa sasa hairuhusu uraia pacha. Wameshakuwa foreigners hawawezi wakatuamulia wala kutusemea mambo ya ndani ya nchi yetu. Waheshimu sheria za kimataifa.

Walipaswa wapiganie uraia pacha wakiwa bado ni watanzania, ndipo sauti zao zingesikika.
Kwani bongo zozo kasema anautaka? Anasemea wapwa zetu! Yeye hana shida nao.
 
Umakin
Hili swala la ununuzi wa ardhi litaleta shida sana. Kuna watu huko nje watakomesha kwa kununua maelfu ya heka halafu wanayahodhi kimya na kufanya wengine wakose hata sehemu ya kufanyia shughuli za kilimo na ufugaji na ndio mwanzo wa uharibifu wa mazingira.

Me nadhani wawezeshwe kuwekeza kwenye maeneo yaliyopo mfano real estate. Kununua hisa za makampuni ya real estate. Kuwekeza mitaji ya kampuni,kuwekeza kwenye elimu mfano kujenga shule za kisasa zenye teknolojia ya hali ya juu, uwekezaji kwenye miundo mbinu kama kupewa ruhusa ya kujenga barabara ambazo zitakuwa zinalipiwa watu kupita. Kuwekeza kwenye sekta ya umeme, etc


Hili swala linataka umakini sana.
U makini gani unatakiwa hapa? Bongo zozo anauliza, mtoto mtanzania wa kuzaliwa, au mtanzania wa kuzaliwa, kwa nini umnyang'anye uraia wake wa asili kwa kuwa kapata fursa huko Ulaya? Anachokisema, utanzania wake unabaki palepale. Anasema, mtoto wake ni mtanzania, anapenda kuwa mtanzania, lakini anachukua uraia wa Uingereza ili atumie fursa zilizopo huko kama matibabu, shule nk nk nk. kwa hiyo anachukua passport ys Uingereza ili kuchukua hizo fursa, lakini roho na moyo wake bado ni mtanzania. Kwa hiyo serikali inachotakiwa kufanya ni kutoa kile kipengele cha mtanzania akichukua uraia wa nchi nyingine kwa ajili ya fursa, asiukane utanzania wake. Basi. Mgogoro unakuwa umeisha.
Haya mawazo ya kijamaa jamaa, ushushu shushu na wivu yameshapitwa na wakati. Unadhani wanaochukua uraiaa huko ulaya, wanapenda sana huko? NO ni fursa tu. wangekuwa wanapenda kwanini hizi kelele haziishi.
 
Hivi ina maana kenya, ghana, bostwana, uk na spain hawaoni hayo madhara ya uraia pacha? Mpaka wakaruhusu?
Hawana sababu za maana ndio maana huwa wanakataa bila kutoa sababu
 
Awamu hii ni kokoro linabeba kila kitu.
 
Back
Top Bottom