Maisha yetu ni mafupi sana hapa duniani, hivyo tunapaswa kufurahia maisha muda wote. Hii habari ya kuoana na mtu eti mchume wote baadaye mtafurahia maisha haikubaliki. Maana hakuna aliye na mkataba na Mungu, unaweza ukafa the next morning.
Na kwa taarifa yako furaha na umaskini havikai pamoja, ni kama maji na moto. Ukiolewa na maskini maana yake ni kwamba umeipiga teke furaha ktk maisha yako. Asikwambie mtu, pesa ndiyo sabuni ya roho.
Kama huna hela utalala sehemu yenye uvundo kama banda la beberu la mbuzi. Huyo mume wako maskini anakuwa amelala huku akikoroma maana amechoka utadhani yuko ICU (ndiyo maana ya mlalahoi). Mate
yanamtoka na kulowesha godoro unaweza kudhani kakojolea.
Utajikuta tu unaamka na kuanza kulia kwa uchungu huku ukimuuliza Mungu; why me? Maisha haya mpk lini?
Na kuna ndharia mpya kuwa maskini hatauona ufalme wa Mungu. Kwasabb kila siku anatenda dhambi ya manung'uniko. Maskini hana shukurani kwa Mungu wake. Kila siku akijisogeza mbele za mola wake anaorodhesha maombi zaidi ya mahitaji yake kwa Mungu. Lkn tajiri kila siku anamtukuza na kumshukuru kwa hatua aliyopiga. Ndiyo maana hisikii tajiri akiangushwa na pepo wachafu.
Umaskini ni ugonjwa. Kwann ? Umaskini hisababisha magonjwa ya kizembe na ku.pelekea mtu kufa kizembe.
Usikubali kuolewa na maskini.