Bora tufikishane mbali potelea pote. Lakini huwezi nitandika Mbele za watu kisa wewe kiongozi bila Sheria kufuatwa

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
BORA TUFIKISHANE MBALI POTELEA POTE. LAKINI HUWEZI NITANDIKA MBELE ZA WATU. KISA WEWE KIONGOZI BILA SHERIA KUFUATWA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Watibeli sio kwamba Sisi ni wajeuri. Hapana. Sisi ni watu wa principles, watu wa kanuni.

2. Ukishakuwa mtu wa principles watu wengi watakuona kama unaujeuri, kiburi, au unaringa. Hizo tafsiri za watu wala hatuzijali na hazijawahi kutusumbua. Tunawafahamu watu na Siku zote mbwa ukimjua jina hakusumbui.

3. Moja ya moja yanayotushangaza na kuiona Dunia inamaajabu Yake, NI pamoja na kuona mtu mzima akitandikwa mbele ya kamera, mbele ya watu alafu anayemtandika hajafuata Sheria, hana mamlaka ya kumtandika, hajaruhusiwa na Sheria kumtandika.

4. Kwamba, ati wewe Leo tumekupa cheo fulani, ukavaa nguo Fulani, ukakuta kesi Fulani, kisha ukaamuru wale walioonekana wanamakosa ati walale chini uwatandike. Nayo yalivyo majinga yanalala. Unayatandika. Aiseeh!

5. Yaani mwanaume mzima, utandikwe mbele za watu. Tena unaambiwa shika chini na wewe unashika. Unatandikwa viboko twa twa twa! Aiseeh! Huko ni kujidharau kwa kiwango cha juu Sana.

6. Hii dunia kuna mambo ukiyaendekeza watu watakudhalilisha Sana. Utafanywa mtumwa Sana.

7. Unaendekeza kazi kuliko Utu na heshima yako. Utadhalilishwa Sana.
Sio lazima ufanye kazi eneo hilo. Kazi zipo nyingi. Bora ufukuzwe kazi kuliko mtu akudhalilishe.

8. Bora mfike mbali kuliko mtu akudhalilishe. Bora tufike huko mbali. Hukohuko.
Hata kama nitapata madhara zaidi lakini yatakuwa madhara ya heshima kuliko kupata angalau yenye dharau.

9. Sheria zifuatwe, kama mtu kakosea twende polisi huko. Kisha tupelekane mahakamani.

10. Lakini sio unitandike viboko hata Kam ni kimoja mbele za Watu, tena bila kufuata Sheria.

11. Vijana msikubali mtu adharau ujana wenu.

12. Ninyi ndio nguvu kazi ya nchi. Nyie ndio walinzi wa nchi hii. Sasa kama hamjitambui, MTU anaweza kukudhalilisha kwa kukutandika viboko mbele ya halaiki mtaweza kulinda nchi yenu kweli nyie?

13. Mtaweza kulinda maslahi ya nchi yenu kweli kama heshima yenu wenyewe tuu mnashindwa kuilinda? Kweli?

14. Unaona Taifa la Iran?
Halipo vile kwa bahati mbaya.
Limejengwa na watu wenye misimamo na heshima zisizoyumba.

15. Kwamba, Mimi ndio sina cheo, Mimi ndio sina Mali, mimi ndio sina elimu kubwa, mimi ndio sina Mwili mkubwa lakini kamwe sitakubali MTU yeyote anishushie heshima Yangu, anidhalilishe tena mbele za watu.

16. Umaskini wako. Shida zako. Familia inakutegemea ndio sio sababu ya kuruhusu kiumbe yeyote akushushie heshima yako. Akudharau. Ni bora tufike huko mbali anakotaka yeye.

17. Vijana, haya maisha hayahitaji watu legelege. Dhaifu na waoga. Hasa ukiwa mwanaume.
Ni Bora ufe maskini ukiwa na heshima. Kuliko upewe dunia nzima alafu uwe dhalili. Umedharauliwa au kujidharau.
Wewe ni mwanaume.

18. Wazazi, wamama na wababa ni lazima muwafundishe watoto wenu heshima. Kuwafundisha watoto heshima ni pamoja na kuwafundisha kujiheshimu.
Kwamba asitokee mtu akamdharau mtoto wako kisa Hali, hadhi, kipato au chochote na mtoto naye akakubali.

19. Mzazi afundishe mtoto, asikubali kuvumilia kuvunjiwa heshima kisa sijui kazi sijui vitu gani. Hakuna kitu muhimu kama heshima. Heshima ndio inayokupa Amani ya moyo.
Maamuzi ya heshima.

20. Nataka nikuambia tuu. Maisha yanawezekana bila kazi unayoifanya. Utafanya KAZI pengine na mahali pengine.
Maisha yanawezekana bila boss au mwajiri anayekudharau.

21. Yeye sio Mungu.
Kazi hiyo sio Mungu.
Kazi zipo nyingi.

22. Maisha yanawezekana bila huyo Mumeo mpumbavu anayekupiga na kukudhalilisha mbele za watoto na watu.
Kuna wanawake wanateswa Sana na waume zao kisa wanawake hawana kazi na hawana pakwenda.
Sisi watibeli hatukosi pakwenda.
Ukifunga mlango huu Mungu atatufungulia mlango mwingine.

23. Ni Bora tuishi maisha kwenye chumba kimoja, kwenye nyumba ya nyasi ikiwezekana hata kulala nje lakini hatuvumilia ukandamizaji, na kudharauliwa.

24. Ndio maana Sisi watibeli hata tusipokuwa na Mali, elimu kubwa tukifika sehemu yoyote tunaheshimiwa kwa sababu heshima haitoki nje Bali inatoka ndani ya mtu mwenyewe.

25. Mkeo anakudharau unacheka cheka. Unacheka cheka nini mjinga wewe?
ATI unamvumilia. Unavumilia?
Sisi Watibeli sio wavumilivu kwenye baadhi ya masuala.

26. Ndio maana mahusiano yetu yanakuwa na furaha kwa sababu hatuvumilii mateso. Dharau ni mateso makubwa Sana kwa mwanadamu.

27. Ukishajidharau dunia inaku-label hivyo. Ukifika mahali popote unashangaa wanakudharau. Kwa sababu umebeba energy ya kudharauliwa. Na uliikubali.
Kile unachokivumilia kinaamua kiwango chako cha heshima.

Nimemaliza. Nawatakia jumapili Njema.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mwaka 2012, nilikuwa mratibu wa sensa halmashauri moja, sasa dc alikuwa mwenyekiti wa kamati ya sensa wilaya, katika harakati za kuajiri akaja na maelekezo yake fulani, nikayapga chn, tuko kwenye kikao akaniambia nitakupga makofi kama hautii, nilimtazama, nikamwambia siyo kupga tu, nyoosha hata kofi kuja kwangu uone...nikamwamby kila mmoja atapata haki yake humu na nitakupokea utakavyokuja.
-akamuamuru ocd anisweke ndani, aliyekuwa mkuu wa mkoa kaingilia kati...

Yule jamaa mwishowe, akahmishwa na akatemeshwa mzigo, mwaka 2020 tulikutana dodoma kwenye harakati za uchaguzi mkuu, ni mjumbe wa mkutano mkuu, kanitazamaa, kaniambia wewe unakiburi cha wakurya..nikarudia maneno yangu "NINGEKUNYOOSHA"

MM SIPENDI DHARAU.
 
Ulifanya Maamuzi ya Heshima Sana.
Kiasi kwamba hata ukikumbuka mpaka Leo unajiheshimu na kujipongeza.
Ni legacy ambayo ukimhadithia mtoto au mjukuu wako anajivunia kuwa na Baba/Babu kama wewe. Na anajifunza ujasiri.

Fikiria ungenywea au wangekuchapa bakora. Wala usingetamani kukumbuka Leo hii kilichotokea.
Mbaya zaidi watoto, mkeo na wajukuu stori hii wangeipata tuu na kujiona wametoka kwa Mzee ambaye ni dhaifu.
 
Waziri mkuu wa kipnd hcho alipata taarifa...mzee yule kila tukiongea kwenye simu au tukakutana kwenye pitapita mwishowe huniamby yaishe usije leta hasira zako za kikurya kama 2012.
 
BORA TUFIKISHANE MBALI POTELEA POTE. LAKINI HUWEZI NITANDIKA MBELE ZA WATU. KISA WEWE KIONGOZI BILA SHERIA KUFUATWA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

5. Yaani mwanaume mzima, utandikwe mbele za watu. Tena unaambiwa shika chini na wewe unashika. Unatandikwa viboko twa twa twa! Aiseeh! Huko ni kujidharau kwa kiwango cha juu Sana.

Nimemaliza. Nawatakia jumapili Njema.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Sisi wengine hii ilitupita please share link
P
 
Mwanaume kulimwa makofi au bakora mbele ya umati hapana bora ujitete ukizidiwa tutakuelewa

Mi ke tu sikubari hata kwa dawa bora nizidiwe ila nimeonesha kujilinda
 
Nikowa kampuni flani ya ulinzi pale DDCA karibu na chuo cha maji kunasiku niliwahi kufua sare za kazi nikawa napasha mwili na ilikuwa jioni ya weekend na kamvua flani hivi,alikuja supervisor na gari hadi getini ghafla kupiga horn nikatoke na bunduki yangu kiunoni ila alishangaa nguo ya juu sina na nipo na vest tu,aliwaka sana nikawa namwangalia at the end akataka kunipiga picha ili akanioshee makao makuu mwamba nikaweka na pause la kigangster kumbe kile kitendo hakikumfurahisha.akataka kunirushi mkono,nilirudi nyuma kama meter tatu hivi halafu nikamwambia “rusha ngumi nirushe risasi”.alipoa kiasi kisha alarudi kwenye gari.asubuhi walati navunja shift niashtuka simu ngeni inaniamuru nireport makao cha ajabu kufika pale yeye hyohuto anajifanya kunipa adhabu,nilimjibu mbele ya officer mkubwa sana kuwa sipo teyyari theni afficer akadakia kwanini nimegoma nikamjibu sioni sababu ya mimi kufanya adhabu.Ikabidi officer yule atale kujua chanzo ni nini ikagundulika nilimtishia risasi,basi bila kutumia nafasi yake vibaya officer yule akaendelea kuhoji hadi kufikiavkutishiana risasi na ikagundulika nimevua nguo ya juu na kivaa uraia chanzo ni mazoezi.hakuna alichokisema catain yule zaidi ya POLE ASKARI UNAWEZA KWENDA NYUMBANI UKAPUMZIKE KWA MAJUKUMU YA WAKATI UJAO.
 
BORA TUFIKISHANE MBALI POTELEA POTE. LAKINI HUWEZI NITANDIKA MBELE ZA WATU. KISA WEWE KIONGOZI BILA SHERIA KUFUATWA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Watibeli sio kwamba Sisi ni wajeuri. Hapana. Sisi ni watu wa principles, watu wa kanuni.

2. Ukishakuwa mtu wa principles watu wengi watakuona kama unaujeuri, kiburi, au unaringa. Hizo tafsiri za watu wala hatuzijali na hazijawahi kutusumbua. Tunawafahamu watu na Siku zote mbwa ukimjua jina hakusumbui.

3. Moja ya moja yanayotushangaza na kuiona Dunia inamaajabu Yake, NI pamoja na kuona mtu mzima akitandikwa mbele ya kamera, mbele ya watu alafu anayemtandika hajafuata Sheria, hana mamlaka ya kumtandika, hajaruhusiwa na Sheria kumtandika.

4. Kwamba, ati wewe Leo tumekupa cheo fulani, ukavaa nguo Fulani, ukakuta kesi Fulani, kisha ukaamuru wale walioonekana wanamakosa ati walale chini uwatandike. Nayo yalivyo majinga yanalala. Unayatandika. Aiseeh!

5. Yaani mwanaume mzima, utandikwe mbele za watu. Tena unaambiwa shika chini na wewe unashika. Unatandikwa viboko twa twa twa! Aiseeh! Huko ni kujidharau kwa kiwango cha juu Sana.

6. Hii dunia kuna mambo ukiyaendekeza watu watakudhalilisha Sana. Utafanywa mtumwa Sana.

7. Unaendekeza kazi kuliko Utu na heshima yako. Utadhalilishwa Sana.
Sio lazima ufanye kazi eneo hilo. Kazi zipo nyingi. Bora ufukuzwe kazi kuliko mtu akudhalilishe.

8. Bora mfike mbali kuliko mtu akudhalilishe. Bora tufike huko mbali. Hukohuko.
Hata kama nitapata madhara zaidi lakini yatakuwa madhara ya heshima kuliko kupata angalau yenye dharau.

9. Sheria zifuatwe, kama mtu kakosea twende polisi huko. Kisha tupelekane mahakamani.

10. Lakini sio unitandike viboko hata Kam ni kimoja mbele za Watu, tena bila kufuata Sheria.

11. Vijana msikubali mtu adharau ujana wenu.

12. Ninyi ndio nguvu kazi ya nchi. Nyie ndio walinzi wa nchi hii. Sasa kama hamjitambui, MTU anaweza kukudhalilisha kwa kukutandika viboko mbele ya halaiki mtaweza kulinda nchi yenu kweli nyie?

13. Mtaweza kulinda maslahi ya nchi yenu kweli kama heshima yenu wenyewe tuu mnashindwa kuilinda? Kweli?

14. Unaona Taifa la Iran?
Halipo vile kwa bahati mbaya.
Limejengwa na watu wenye misimamo na heshima zisizoyumba.

15. Kwamba, Mimi ndio sina cheo, Mimi ndio sina Mali, mimi ndio sina elimu kubwa, mimi ndio sina Mwili mkubwa lakini kamwe sitakubali MTU yeyote anishushie heshima Yangu, anidhalilishe tena mbele za watu.

16. Umaskini wako. Shida zako. Familia inakutegemea ndio sio sababu ya kuruhusu kiumbe yeyote akushushie heshima yako. Akudharau. Ni bora tufike huko mbali anakotaka yeye.

17. Vijana, haya maisha hayahitaji watu legelege. Dhaifu na waoga. Hasa ukiwa mwanaume.
Ni Bora ufe maskini ukiwa na heshima. Kuliko upewe dunia nzima alafu uwe dhalili. Umedharauliwa au kujidharau.
Wewe ni mwanaume.

18. Wazazi, wamama na wababa ni lazima muwafundishe watoto wenu heshima. Kuwafundisha watoto heshima ni pamoja na kuwafundisha kujiheshimu.
Kwamba asitokee mtu akamdharau mtoto wako kisa Hali, hadhi, kipato au chochote na mtoto naye akakubali.

19. Mzazi afundishe mtoto, asikubali kuvumilia kuvunjiwa heshima kisa sijui kazi sijui vitu gani. Hakuna kitu muhimu kama heshima. Heshima ndio inayokupa Amani ya moyo.
Maamuzi ya heshima.

20. Nataka nikuambia tuu. Maisha yanawezekana bila kazi unayoifanya. Utafanya KAZI pengine na mahali pengine.
Maisha yanawezekana bila boss au mwajiri anayekudharau.

21. Yeye sio Mungu.
Kazi hiyo sio Mungu.
Kazi zipo nyingi.

22. Maisha yanawezekana bila huyo Mumeo mpumbavu anayekupiga na kukudhalilisha mbele za watoto na watu.
Kuna wanawake wanateswa Sana na waume zao kisa wanawake hawana kazi na hawana pakwenda.
Sisi watibeli hatukosi pakwenda.
Ukifunga mlango huu Mungu atatufungulia mlango mwingine.

23. Ni Bora tuishi maisha kwenye chumba kimoja, kwenye nyumba ya nyasi ikiwezekana hata kulala nje lakini hatuvumilia ukandamizaji, na kudharauliwa.

24. Ndio maana Sisi watibeli hata tusipokuwa na Mali, elimu kubwa tukifika sehemu yoyote tunaheshimiwa kwa sababu heshima haitoki nje Bali inatoka ndani ya mtu mwenyewe.

25. Mkeo anakudharau unacheka cheka. Unacheka cheka nini mjinga wewe?
ATI unamvumilia. Unavumilia?
Sisi Watibeli sio wavumilivu kwenye baadhi ya masuala.

26. Ndio maana mahusiano yetu yanakuwa na furaha kwa sababu hatuvumilii mateso. Dharau ni mateso makubwa Sana kwa mwanadamu.

27. Ukishajidharau dunia inaku-label hivyo. Ukifika mahali popote unashangaa wanakudharau. Kwa sababu umebeba energy ya kudharauliwa. Na uliikubali.
Kile unachokivumilia kinaamua kiwango chako cha heshima.

Nimemaliza. Nawatakia jumapili Njema.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Iwe mbele za watu au Kwa kujificha,kutandikwa hakufai Kwa mtu nzima na hata mtoto!
 
Ni kweli usikubali kudharauliwa ila pia ujicontrol na mihemko.

Mfano boss wako anakuambia lala chini, unatakiwa ugome kulala chini na kuondoka eneo la tukio na sio kusubiri boss wako akurushie fimbo ukiwa umesimama na wewe ukaanza kumpiga mangumi eti kuonyesha umwamba ambao unaweza kupelekea ukamuua.
 
Back
Top Bottom