Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
BORA TUFIKISHANE MBALI POTELEA POTE. LAKINI HUWEZI NITANDIKA MBELE ZA WATU. KISA WEWE KIONGOZI BILA SHERIA KUFUATWA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
1. Watibeli sio kwamba Sisi ni wajeuri. Hapana. Sisi ni watu wa principles, watu wa kanuni.
2. Ukishakuwa mtu wa principles watu wengi watakuona kama unaujeuri, kiburi, au unaringa. Hizo tafsiri za watu wala hatuzijali na hazijawahi kutusumbua. Tunawafahamu watu na Siku zote mbwa ukimjua jina hakusumbui.
3. Moja ya moja yanayotushangaza na kuiona Dunia inamaajabu Yake, NI pamoja na kuona mtu mzima akitandikwa mbele ya kamera, mbele ya watu alafu anayemtandika hajafuata Sheria, hana mamlaka ya kumtandika, hajaruhusiwa na Sheria kumtandika.
4. Kwamba, ati wewe Leo tumekupa cheo fulani, ukavaa nguo Fulani, ukakuta kesi Fulani, kisha ukaamuru wale walioonekana wanamakosa ati walale chini uwatandike. Nayo yalivyo majinga yanalala. Unayatandika. Aiseeh!
5. Yaani mwanaume mzima, utandikwe mbele za watu. Tena unaambiwa shika chini na wewe unashika. Unatandikwa viboko twa twa twa! Aiseeh! Huko ni kujidharau kwa kiwango cha juu Sana.
6. Hii dunia kuna mambo ukiyaendekeza watu watakudhalilisha Sana. Utafanywa mtumwa Sana.
7. Unaendekeza kazi kuliko Utu na heshima yako. Utadhalilishwa Sana.
Sio lazima ufanye kazi eneo hilo. Kazi zipo nyingi. Bora ufukuzwe kazi kuliko mtu akudhalilishe.
8. Bora mfike mbali kuliko mtu akudhalilishe. Bora tufike huko mbali. Hukohuko.
Hata kama nitapata madhara zaidi lakini yatakuwa madhara ya heshima kuliko kupata angalau yenye dharau.
9. Sheria zifuatwe, kama mtu kakosea twende polisi huko. Kisha tupelekane mahakamani.
10. Lakini sio unitandike viboko hata Kam ni kimoja mbele za Watu, tena bila kufuata Sheria.
11. Vijana msikubali mtu adharau ujana wenu.
12. Ninyi ndio nguvu kazi ya nchi. Nyie ndio walinzi wa nchi hii. Sasa kama hamjitambui, MTU anaweza kukudhalilisha kwa kukutandika viboko mbele ya halaiki mtaweza kulinda nchi yenu kweli nyie?
13. Mtaweza kulinda maslahi ya nchi yenu kweli kama heshima yenu wenyewe tuu mnashindwa kuilinda? Kweli?
14. Unaona Taifa la Iran?
Halipo vile kwa bahati mbaya.
Limejengwa na watu wenye misimamo na heshima zisizoyumba.
15. Kwamba, Mimi ndio sina cheo, Mimi ndio sina Mali, mimi ndio sina elimu kubwa, mimi ndio sina Mwili mkubwa lakini kamwe sitakubali MTU yeyote anishushie heshima Yangu, anidhalilishe tena mbele za watu.
16. Umaskini wako. Shida zako. Familia inakutegemea ndio sio sababu ya kuruhusu kiumbe yeyote akushushie heshima yako. Akudharau. Ni bora tufike huko mbali anakotaka yeye.
17. Vijana, haya maisha hayahitaji watu legelege. Dhaifu na waoga. Hasa ukiwa mwanaume.
Ni Bora ufe maskini ukiwa na heshima. Kuliko upewe dunia nzima alafu uwe dhalili. Umedharauliwa au kujidharau.
Wewe ni mwanaume.
18. Wazazi, wamama na wababa ni lazima muwafundishe watoto wenu heshima. Kuwafundisha watoto heshima ni pamoja na kuwafundisha kujiheshimu.
Kwamba asitokee mtu akamdharau mtoto wako kisa Hali, hadhi, kipato au chochote na mtoto naye akakubali.
19. Mzazi afundishe mtoto, asikubali kuvumilia kuvunjiwa heshima kisa sijui kazi sijui vitu gani. Hakuna kitu muhimu kama heshima. Heshima ndio inayokupa Amani ya moyo.
Maamuzi ya heshima.
20. Nataka nikuambia tuu. Maisha yanawezekana bila kazi unayoifanya. Utafanya KAZI pengine na mahali pengine.
Maisha yanawezekana bila boss au mwajiri anayekudharau.
21. Yeye sio Mungu.
Kazi hiyo sio Mungu.
Kazi zipo nyingi.
22. Maisha yanawezekana bila huyo Mumeo mpumbavu anayekupiga na kukudhalilisha mbele za watoto na watu.
Kuna wanawake wanateswa Sana na waume zao kisa wanawake hawana kazi na hawana pakwenda.
Sisi watibeli hatukosi pakwenda.
Ukifunga mlango huu Mungu atatufungulia mlango mwingine.
23. Ni Bora tuishi maisha kwenye chumba kimoja, kwenye nyumba ya nyasi ikiwezekana hata kulala nje lakini hatuvumilia ukandamizaji, na kudharauliwa.
24. Ndio maana Sisi watibeli hata tusipokuwa na Mali, elimu kubwa tukifika sehemu yoyote tunaheshimiwa kwa sababu heshima haitoki nje Bali inatoka ndani ya mtu mwenyewe.
25. Mkeo anakudharau unacheka cheka. Unacheka cheka nini mjinga wewe?
ATI unamvumilia. Unavumilia?
Sisi Watibeli sio wavumilivu kwenye baadhi ya masuala.
26. Ndio maana mahusiano yetu yanakuwa na furaha kwa sababu hatuvumilii mateso. Dharau ni mateso makubwa Sana kwa mwanadamu.
27. Ukishajidharau dunia inaku-label hivyo. Ukifika mahali popote unashangaa wanakudharau. Kwa sababu umebeba energy ya kudharauliwa. Na uliikubali.
Kile unachokivumilia kinaamua kiwango chako cha heshima.
Nimemaliza. Nawatakia jumapili Njema.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam