Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Nakumbuka sana miaka ya 60 na 70 wakati bado kulikuwa na harufu ya mkooloniChangamoto nyingine ni hili ulilolizungumzia.
Haswa changamoto kubwa ni viongozi wetu na watunga sera wetu.
Nadhani bado wapo kwenye ujima, na wapo bado kwenye usingizi, bado Kwenye fikra zao hakujapambazuka.
Labda ufahamu wangu ni mdogo sana lakini kwa kweli sijaweza kuona ubaya wowote kwenye uraia pacha.
Binafsi naona ilikua ni fursa adhimu sana kwa sababu aliyetoka nje kuna nuru fulani ameipata.
Ukiangalia taifa letu miaka hii ya 2020 na ile miaka 1970 unaweza ukaona ni heri miaka ile ambayo kulikua na viwanda vinavyozalisha kwa vingi na vingi vikiwa property ya Tanzania.
Tofauti na sasa, ambapo dunia inakimbia kwa kasi sana kwenda mbele kwa teknolojia na maarifa makubwa sisi badala yake tunakimbia kurudi nyuma tena kwa kasi sana .
Kama wasomi, na wataalamu waliopo hapa nchini wangekua na uthubutu na maono na nia pengine tungekuwa tunaongea vinginevyo, lakini kila mtu anaona.
Dhania yangu tungeweza sana kusaidiwa na diaspora kwa kiasi kikubwa kama tungekuwa na nia ya kupata msaada wao katika muktadha mzima wa maendeleo.
Nakumbuka kulikuwa na umeme wa kutosha hata katika ofisi za wilaya na hospitali zote hata baadhi ya barabara
Kulikuwa na maji mitaani ya bure na manyumbani tulikuwa na meters za kulipia kila mwezi
Yaani hela ilikuwa na thamani kiasi kuwaona wakulima wanaendesha gari ilikuwa jambo la kawaida sana
Leo mkulima anahangaika akivuna hata hata akiba zaidi ya madeni
Mkuu nalia kwa uchungu jinsi washenzi walivyoibadilisha nchi yetu kutoka kwenye uaminifu na kuleta Sera za rushwa na unyang'anyi nasema Sera kwa sababu ndio mfumo tuliofundishwa baada ya viwanda kufa na maisha kubadilishwa kuwa ya ubabe, wizi , dhulma na kutokuwa na uwajibikaji
Leo mwizi anahamishwa na kupelekwa sehemu nyingine
Hawataki kujua corruption officers katika jeshi la police wala uhamiaji
Kila mmoja anakula kwa urefu wa kamba yake
Je ndio maisha tulijiamulia haya?
Na je hawajiulizi ni maisha mazuri?
Leo kuna watu wanasema ooh nchi imeingiliwa na kupenyeza majirani
Usalama uko hatarini
Huwa nacheka sana
Hao wazalendo wako wapi wa kuilinda nchi na kuacha rushwa?
Hivi kuna siku mkulima atakuja kuendesha V8? Maana zamani gari zilikuwa Peugeot na walikuwa nazo
Aisee naona mradi siku ziende tu
Eti hawataki dual citizenship ni kwa sababu wanajifanya ujuaji na kusema wao wakisema hivi sisi tunasema hapana hata kama hakuna sababu